Top ad

Top ad

SEMINA ELEKEZI KWA WAGAWA DAWA ZA KINGATIBA YA MABUSHA, MATENDE NA MINYOO YATOLEWA KINONDONI

Posted On: December 14th, 2018
Semina hiyo iliyohusisha wagawa dawa za kingatiba za magonjwa ya mabusha na matende kutoka kata zote 20 za Manispaa ya kinondoni, imefanyika leo katika ukumbi wa Roman Catholic ulioko Manzese.
Akieleza malengo ya semina hiyo, mratibu wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele katika manispaa ya Kinondoni Dr. Neema Mlole amesema, lengo ni kuhakikisha elimu iliyosahihi juu ya kampeni hii inatolewa kwa usahihi na kueleweka,  lakini pia ni katika kuzingatia baadhi ya vipengele vinavyompasa binadamu yeyote yule kumeza dawa vinafuatwa, kadhalika na kuhakikisha pia malengo yaliyokusudiwa ya kufikia wananchi takribani milioni 1.2 kwa kampeni hii pia yanafikiwa.
"Ili tuweze kufikia malengo madhubuti, ni lazima elimu sahihi itolewe, lakini pia tunahitaji kuimarisha na kuhakikisha  tunalinda nguvu kazi ya wananchi,na  namna pekee ni kuboresha afya zao pale inapobidi kwa kuhakikisha wanashiriki kampeni hizi kwa uhakika a ufasaha mkubwa. Amesisitiza Dr Neema.
Ameongeza kuwa kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto kitengo cha magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele itaendesha  kampeni  kuanzia tarehe 15/12/2018 na kuisha tarehe 20/12/2018 ,,hivyo wagawa dawa hawa ni watu muhimu sana katika kuhakikisha ufanisi huo unakuwepo na unazingatiwa.
Katika semina hiyo pamoja na zoezi la usambazaji kingatiba kwa ajili ya kampeni hiyo iliyoambatana na ugawaji wa vifaa vitakavyotumika, pia wamejifunza namna thabiti ya utoaji huduma hiyo, vitu vya kuzingatia kabla na baada ya utoaji wake, na upi umri sahihi wa mtu kumeza dawa ikiwa ni pamoja na kupima urefu.
Katika hatua nyingine, wagawa dawa hao wameishukuru Wizara pamoja na Halmashauri kwa kuendesha kampeni hii yenye manufaa kwa afya za wanadamu, na kuahidi ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha hilo linafanikiwa.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.

0 comments:

Post a Comment

 
Top