HATI 93 ZA VIWANJA KWA NJIA YA ELEKTRONIKI ZAKAMILIKA KINONDONI
Posted On: December 14th, 2018
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa kamati ya Mipangomiji na mazingira ambaye pia ni diwani wa kata ya Mwananyamala Mhe. Songoro Mnyonge alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kamati yake katika kikao cha baraza la madiwani robo ya kwanza kilichofanyika leo .
Amesema Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi imeanza utaratibu huo mpya uliorahisi na unaotumia mfumo maalumu wa kuandaa hati na kukamilika kwa siku moja, hali iliyoondoa bugudha na kero kwa wananchi.
"Tunaishukuru Wizara ya ardhi kwa kuandaa mfumo rahisi kwa suala zima la uandaaji wa hati, mfumo huo wa elektroniki umesaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa bugudha kwa wananchi, kwani ni mfumo wezeshi, na unatumia muda mchache hali iliyoondoa kero kwa wananchi" Amesisitiza Songoro.
Awali akiwakaribisha wajumbe kwenye kikao hicho cha baraza, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Msasani Mhe. Benjamini sitta alisema katika kikao hiko zitapokelewa na kujadiliwa agenda zitakazotokana na taarifa za kamati tano za kudumu za Halmashauri.
Agenda hizo ni utekelezaji wa taarifa za kamati ya huduma za uchumi, afya na elimu, kamati ya Mipangomiji na mazingira, Kamati ya maadili, kamati ya kudhibiti ukimwi na kamati ya fedha na uongozi.
Katika hatua nyingine baraza hilo pia limempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuwajali wamachinga na kuwatengenezea mazingira wezeshi ya ufanyaji kazi zao kwa kuwapatia vitambulisho.
Imeandaliwa na
Kitengo cha habari na uhusiano
Manispas ya Kinondoni.
0 comments:
Post a Comment