KINONDONI YAPOKEA UJUMBE TOKA JIJI LA ARUSHA
NI KWA LENGO LA KUBADILISHANA UZOEFU KATIKA UTEKELEZAJI WA MKOPO WA ASILIMIA KUMI
Manispaa ya Kinondoni imepokea ujumbe wa watu watano kutoka Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika utendaji wa shughuli za Serikali hasa utekelezaji wa mikopo ya asilimia kumi kwa
vijana walemavu na wanawake.
Ujumbe huo uliohusisha Naibu Meya wa Jiji la Arusha, wataalamu kutoka Idara ya maendeleo ya Jamii akiwemo mkuu wa Idara hiyo, Afisa vijana, Mratibu wa dawati la uwezeshaji Wananchi kiuchumi na Afisa maendeleo ya jamii kata umepata fursa ya kutembelea vikundi vilivyopata mikopo na kujionea wanavyotekeleza majukumu yao na suala la urejeshaji wa mikopo hiyo.
Vikundi vilivyotembelewa ni kikundi cha usindikaji wa viungo mbalimbali cha vijimambo group kilichopo Kigogo pamoja na kikundi cha EZEMA watengenezaji wa bidhaa z ngozi kilichopo Mbezi Makonde.
Jiji la Arusha limefurahishwa na elimu waliyoipata ya utekelezaji wa mikopo ya asilimia kumi na jinsi Kinondoni inavyotoa mikopo ya mashine za kufanyia kazi zinazowezesha utekelezaji wa kuingia uchumi wa Kati wa viwanda.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
0 comments:
Post a Comment