Top ad

Top ad

KINONDONI YASAINI MIKATABA NA MAKAMPUNI MAWILI YA TAKRIBANI BILIONI 58

Posted On: June 13th, 2019
NI KWA AJILI YA UJENZI NA MABORESHO YA MTO  NG'OMBE NA BARABARA YA SHEKILANGO KWA KIWANGO CHA NJIA NNE.
Akisaini mikataba hiyo, kati yake na makampuni hayo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Ndg.  Aron Kagurumjuli amesema, mradi wa mto ng'ombe utakaogharimu bilioni 32, utajengwa na kampuni ya China Henan International Cooperation Group CO. LTD na mradi wa barabara ya shekilango wa njia nne utakaogharimu shilingi 26 bilioni, utajengwa na Kampuni ya China road and bridge Cooperation hali itakayosaidia si tu kuboresha maeneo hayo bali pia kuyapandisha hadhi kwa kiwango kusudiwa.
Amesema katika mikataba hiyo pia yatajengwa mabwawa  ya kukusanyia maji eneo la karibu na chuo cha maji kutoka maeneo mbalimbali na maji hayo yataruhusiwa kuingia taratibu mto ng'ombe hali ambayo itasaidia kupunguza mafuriko.
Akishuhudia utilianaji sahihi mikataba hiyo, Mstahiki Meya Wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamini Sitta amesema,  Serikali ya awamu ya tano ni Serikali sikivu yenye lengo la kuboresha makazi duni na kuwatoa wananchi kwenye kifungo cha mateso ya mafuriko,  na ujenzi huu wa mto ng'ombe utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kadhia hiyo iliyokuwa ikisumbua wananchi wa  maeneo ya Tandale na kijitonyama.
Aidha Meya Sitta pia amewataka makandarasi wanaojenga miradi hiyo  kujenga kwa wakati na kwa ubora stahiki ili waweze kumaliza kero iliyokuwa inawasumbua wananchi kwa muda mrefu.

Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.

0 comments:

Post a Comment

 
Top