WANANCHI KINONDONI WAMETAKIWA KUJENGA MAZOEA YA KULIPA KODI KILA MWAKA
Posted On: February 3rd, 2019
NI KATIKA KUHAKIKISHA UTAMADUNI WA KULIPA KODI UNAJENGEKA NA KUEPUKA KUJILIMBIKIZA MADENI YASIYO YA LAZIMA.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo alipofanya ziara katika Kata za Manispaa ya Kinondoni, na kuongea na wanachi Katika maeneo mbalimbali inapotekelezwa miradi ya maendeleo.
Amesema uzalendo ndio jambo la msingi katika kuhakikisha kodi zinalipwa na miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa kiwango cha ubora uliokusudiwa.
"Wananchi jengeni tabia ya kulipa kodi za majengo kila mwaka, jengeni utaratibu na mazoea ya kushiriki utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kwa pamoja tuijenge nchi yetu" Amesisitiza Mh.Chongolo.
Ameongeza kuwa yapo madhara yanayoweza kujitokeza kwa mwananchi kutokulipa Kodi hiyo ya jengo kwa muda mrefu anapotakiwa kufanya hivyo kuwa ni pamoja na nyumba kupigwa mnada.
Katika ziara hiyo, Mkuu huyo wa Wilaya ametembelea ujenzi wa Shule ya msingi na sekondari za Mivumoni zilizopo kata ya Wazo, Eneo linalotarajiwa kujengwa soko na stendi ya mabasi ya abiria ( daladala) Katika eneo la madale.
Miradi mingine ni eneo la soko la Kisanga, Ujenzi wa Bwalo la chakula Katika shule ya sekondari Mbweni teta, Eneo la soko lililopo Mbweni Mpiji pamoja na Ujenzi wa hospitali ya Mabwepande.
Katika maeneo yote aliyotembelea Mkuu wa Wilaya, amewahimiza wananchi kushiriki katika kuchangia shughuli za kimaendeleo zinazoendelea Katika maeneo yao.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
0 comments:
Post a Comment