TAARIFA KWA UMMA
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni leo Alhamis, March 14, 2019 katika Mkutano wake wa kawaida wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni, pamoja na mambo mengine imethibitisha matumizi ya jumla ya Tshs. 3,675,202,443.90 zilizotumika kutekeleza Miradi ya Maendeleo robo ya pili kwa kipindi cha kuanzia mwezi Octoba hadi Disemba, 2018.
Kwa mujibu wa Mchanganuo wa Taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo robo ya pili, kati ya fedha hizo Tshs. 2,678,384,151.30 ni fedha za Mapato ya ndani ya Manispaa, Tshs. 510,438,100.00 ni fedha za Mfuko wa pamoja wa Afya, Tshs.176,006,913.6 ni fedha za Elimu bila malipo Msingi, Tshs. 176,053,020.00 ni fedha za Elimu bila Malipo Sekondari, Tshs. 41,050,000.00 ni fedha za Mfuko wa kuchochea Maendeleo ya Jimbo na Tshs. 93,270,259.00 ni fedha za Michango ya Jamii.
Aidha Baraza la Madiwani katika Mkutano huo wa kawaida limethibitisha taarifa za utekelezaji wa kazi za Kamati za kudumu za Halmashari yaani Kamati ya Huduma za Uchumi Afya na Elimu, Kamati ya Mipangomiji na Mazingira, Kamati ya Maadili, Kamati ya Kuthibiti Ukimwi na Kamati ya Fedha na Uongozi zilizofanyika katika robo ya pili kuanzia Mwezi Oktoba hadi Disemba 2018.
Imetolewa na kitengo cha Habari na Uhusiano, Manispaa ya Kinondoni.
Home
»
»Unlabelled
»
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment