KOREA YA KUSINI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA MAHUSIANO KATI YAKE NA MKOA WA DAR ES SALAAM Posted On: May 30th, 2019 NI ULE WA MIAKA MITATU UNAOHUSU KUWAJENGEA UWEZO WATAALAM WA KILIMO KATIKA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA ZA KILIMO CHA MJINI CHA KISASA . Korea ya Kusini jimbo la Gyeongsanam imeoneshwa kuridhishwa na utekelezaji wa makubaliano yalioingiwa kati yake na Mkoa wa Dar és salaam, yahusuyo utoaji wa huduma ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam wa kilimo, kuhusiana na teknolojia za Kilimo chá kisasa cha mjini ili kukabiliana na changamoto zilizopo kama ufinyu wa ardhi na magonjwa ya mimea. Hayo yamedhihirika leo wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya ujumbe kutoka korea ya kusini, waliozuru kwa lengo la kufanya majadiliano ya namna ya kuingia upya mkataba mwingine, wenye lengo la kuboresha zaidi sekta hiyo ya kilimo hasa upande wa matumizi ya teknolojia ya vifaa vya kisasa kwa matumizi madogo ya ardhi yenye tija, baada ya ule wa awali kuisha. Akipokea ujumbe huo kutoka Korea ya Kusini, ulipozuru kituo cha kilimo Malolo Kinondoni, Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Mhe. Benjamin Sitta amesema Dar es salaam hususani Kinondoni leo imefungua ukurasa mpya wa maendeleo katika sekta ya kilimo cha mjini kwani mkataba huo uliodumu kwa miaka mitatu umeibua ari mpya ya maendeleo na kuleta mapinduzi katika sekta hii kwa kuiniua pato lá mkulima pindi atumiapo utaalam huo ulio rahisi na wamatumizi madogo ya eneo. "Hakika mapinduzi ya kilimo cha mjini yameneemeshwa vilivyo kupitia uhusiano wetu na Korea kusini maana tumejifunza mambo mengi sana kupitia wao na tunaamini hatutaishia hapa tutaenda mbele zaidi"ameeleza Msitahiki Meya. Naye Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji wa Mkoa Dar es salaam Dkt. Elizabeth Mshote amesema kuwa Manispaa za jiji la Dar es salaam zimenufaika vilivyo kupitia uhusiano huo na Korea kusini na kuanishia kuwa awamu ijayo itakuwa nzuri zaidi kwani ushiriki utajikita zaidi katika miundombinu ya kilimo tofauti na ule wa awali uliokuwa na lengo la kujengea uwezo wataalam hao wa kilimo. Kwa upande wao Mr. Lee, Do Wan ambaye ni Mkurugenzi wa Division ya Ushirikiano na nchi za nje kutoka Jimbo la Gyeongsangnam na Dkt Lim Chae Shin kutoka Kituo cha mafunzo ya technologia ya kisasa ya kilimo ATEC kilichopo Mjini Jinju Korea kusini, amesema kuwa anaamini Tanzania inaweza kabisa kufikia Korea kusini maana mwitikio uliooneshwa ndani ya miaka mitatu ni wa kipekee sana na unadhirisha hamu ya mapinduzi ya kilimo ndani ya mioyo yao. Hafla hiyo imeshirikisha wataalamu wa sekta ya kilimo kutoka Halmashauri zote tano za mkoa wa Dar es salaam, pamoja na KOICA. Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. KOREA YA KUSINI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA MAHUSIANO KATI YAKE NA MKOA WA DAR ES SALAAM Posted On: May 30th, 2019 NI ULE... + Read more »
KINONDONI YAENDESHA SEMINA ELEKEZI KWA WENYEVITI NA MAKATIBU WA KAMATI ZA USIMAMIZI WA MAAFA ZA KATA. Posted On: May 25th, 2019 NI KUHUSIANA NA UTEKELEZAJI WA SHERIA YA MAAFA YA MWAKA 2015 NA JINSI YA KUKABILIANA NA MAJANGA KATIKA SEKTA HIYO. Akifungua semina hiyo leo katika ukumbi wa DMDP jijini Dar es salaam, Mkuu wa idara ya Mendeleo ya Jamii Bi.Halima Kahema amesema, lengo ni kuzijengea uwezo kamati za kata kwani ndio msingi mzima katika kutekeleza sera na usimamizi wa sheria hii ya maafa ya mwaka 2015, ngazi ya Kata na Mitaa. Ameongeza kuwa ili uweze kutekeleza Jambo ni lazima ulijue, na katika hili ni dhahiri kabisa mana kunapokosekana usimamizi mzuri unaoenda sambamba na utekelezaji wowote wa sheria hakika zoezi linakuwa gumu, na hata uchukuaji wa hatua stahiki katika sekta hiyo pia unakuwa mgumu. Bi. Halima amesema "wenyeviti na makatibu wa Kamati mnatakiwa kwanza kuijua sheria vizuri ili muweze kuwa na maamuzi na mamlaka kamili katika kutafuta njia nzuri zaidi za kukabiliana na maafa pale yatakapojitokeza". Aidha mratibu wa Maafa Manispaa ya Kinondon Bi. Pendo Mwaisaka wakati akiongea,ametoa msisitizo wa utoaji wa taarifa kwa wakati, na taarifa hizo ziambatane na takwimu sahihi la tukio husika na kusisitiza kuwa suala la Maafa ni suala mtambuka linalohitaji nguvu ya pamoja na Serikali, sekta binafsi na wadau wengine. Mada zilizowasilishwa katika semina hiyo ni Mpango wa kukabiliana na dharura mkoa wa Dar es salaam, Jinsi ya kuandaa mipango ya kujiandaa na kupunguza athari za majanga, Uokozi na namna ya kukabiliana na majanga mbalimbali, maafa, majanga na uokozi na nini kifanyike kukabiliana na majanga. Nyingine ni miradi inayotekelezwa na Manispaa ya Kinondoni DMDP iliyolenga kupunguza athari za mafuriko, sheria ya usimamizi ya maafa ya mwaka 2015 pamoja na utoaji wa taarifa za majanga. Semina hii imepata uwakilishi kutoka DarMAERT, oxford policy, Chama cha msalaba mwekundu, na Jeshi la zimamoto, na kuhudhuriwa na maafisa watendaji wa kata, maafisa maendeleo ya jamii Kata pamoja na wadau wengine. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAENDESHA SEMINA ELEKEZI KWA WENYEVITI NA MAKATIBU WA KAMATI ZA USIMAMIZI WA MAAFA ZA KATA. Posted On: May 25th, 2019 NI KUHU... + Read more »
JAMII YA KINONDONI YATAKIWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUTUMIA MAZIWA ILI KUIMARISHA AFYA YA MWILI NA AKILI KUELEKEA UCHUMI WA KATI WA VIWANDA Posted On: May 24th, 2019 Kauli hiyo imetolewa leo na Mhe Diwani wa kata ya Kunduchi Mh. Michael Urio kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya unywaji wa maziwa mashuleni inayoratibiwa na Idara ya mifugo na uvuvi kwa Manispaa ya Kinondoni na kufanyika katika Shule ya Sekondari Kondo. Amesema kuwa, serikali ya awamu ya tano inayo nia madhubuti na mwelekeo wa dhati katika kuijenga Tanzania ya Viwanda na uchumi wa Kati, hivyo inahitaji jamii ya watu wenye afya thabiti na akili ya kupambanua mambo kwa ufasaha ili waweze kuendana na sera hiyo. "Maziwa yana virutubisho vyote mhimu vinavyotakiwa katika ujenzi wa mwili na akili hivyo badala ya kunywa pombe na vinywaji vingine tunyweni maziwa kwa wingi ili kuunga juhudi za serikali pia viwanda vyetu vya ndani" ameongeza mhe Urio. Aidha Quenter Mawinda kwa niaba ya msajili wa bodi ya maziwa amewashauri wanafunzi kutumia maziwa kwa wingi ili kuimarisha afya ya akili na mwili na waweze kuendana na Kasi ya Mhe Rais maana anahitaji vijana wachapakazi walioimara. Mara baada ya uzinduzi huo , Manispaa ya Kinondoni kupitia idara ya mifugo na uvuvi imegawa maziwa katika shule tano za Sekondari ambazo ni Shule ya Sekondari Mbopo, Kondo, Mtakuja Beach, Boko na Bunju A, ambapo zaidi ya paketi 350 kwa kila shule zimegawiwa, lakini siku ya pili kwa idadi ya paketi hizo hizo itagawiwa kwa Shule tano za Msingi za Manispaa ya Kinondoni . Uzinduzi huu unatarajiwa kitaifa kufanyika Mkoani Arusha kuanzia tar 28 mwezi wa tano hadi tarehe 1 mwezi wa sita. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. JAMII YA KINONDONI YATAKIWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUTUMIA MAZIWA ILI KUIMARISHA AFYA YA MWILI NA AKILI KUELEKEA UCHUMI WA KATI WA VIWANDA ... + Read more »
KAMATI YA SIASA YA MKOA WA DAR ES SALAAM, YARIDHISHWA NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA KATIKA WILAYA YA KINONDONI. Posted On: May 24th, 2019 Kamati hiyo Chini ya mwenyekiti wake Bi Kate Kamba imeonesha kuridhishwa na maboresho ya miundombinu ya barabara yanayofanyika maeneo ya katikati hususan Tandale, Kijitonyama na Mwananyamala Manispaa ya Kinondoni. Hali hiyo imedhihirika wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo ukiendelea katika ziara ya Kamati ya katika Manispaa ya Kinondoni, chini ya Mwenyekiti wake Bi. Kate Kamba, iliyofanyika kwa lengo la kujiridhisha na utekelezaji wa ilani unaoenda sambamba na ubora wa miradi inayotekelezwa. Bi Kate amesema kuwa wakati umefika sasa kwa Kinondoni kuelekeza nguvu katika kuboresha makazi holela wanayoishi wananchi kwani wanaamini maboresho ya miundombinu yakienda sambamba na maboresho ya makazi ndipo tija itakapopatokana. Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bw Maduhu Kazi ameishukuru Kamati hiyo kwa kutembelea Kinondoni na kuahidi kufanyia kazi ushauri na maelekezo yote yaliyotolewa na Kamati hiyo ya Siasa. Miradi iliyotembelewa katika ziara hiyo ni pamoja na miradi ya barabara, Shule za Msingi na Sekondari, zahanati pamoja na vituo vya Afya. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. KAMATI YA SIASA YA MKOA WA DAR ES SALAAM, YARIDHISHWA NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA KATIKA WILAYA YA KINONDONI. Posted On: May... + Read more »
JAMII YA KINONDONI IMETAKIWA KUSHIRIKI KATIKA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU PAMOJA NA MAZINGIRA YA SHULE ILI WANAFUNZI WAWEZE KUPATIWA ELIMU BORA. Posted On: May 7th, 2019 Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Daniel Chongolo katika hafla ya upokeaji mabati kutoka kampuni ya ando, yatakayowezesha kuezeka darasa moja katika shule ya msingi Wazo hill. Amesema kwa juhudi za pamoja kati ya Serikali kwa kushirikiana na wadau katika kuhakikisha miundombinu ya shule, elimu na mazingira vinaboreshwa, kwa hakika taaluma katika Wilaya yeu itapanda. "Serikali inalengo mahususi la kuhakikisha miundombinu ya elimu inapatikana na inaboreshwa, katika hili ninafurahishwa sana kuona tunao wadau katika Wilaya yetu walio tayari kutuunga mkono, tunawashukuru sana kwa uzalendo mlionao"Amesema Chongolo. Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya (ando), Bw Godlistern Maimu amesema, kampuni yao imejiwekea utaratibu wa kusaidia jamii kwani wanaamini ndoto za wanafunzi zitafikiwa pale watakapopatiwa elimu bora na katika mazingira mazuri. Naye Afisa Elimu wa Manispaa hiyo Ndg Kiduma Mageni alipotakiwa kuongea, aliushukuru uongozi mzima wa kampuni ya ando) kwa kushirikiana na Serikali katika kuboresha mazingira ya elimu, na kuahidi kuyalinda na kuyatumia kwa makusudi yaliyokusudiwa. Katika hatua nyingine Mhe Chongolo ameahidi kutatua changamoto ya vyumba vya madarasa pamoja na ukosefu wa ofisi ya walimu unaoikabili shule ya Msingi Wazo hill kwani kwa sasa ina idadi ya wanafunzi zaidi ya 3000 huku ikiwa na walimu 57 pekee. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. JAMII YA KINONDONI IMETAKIWA KUSHIRIKI KATIKA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU PAMOJA NA MAZINGIRA YA SHULE ILI WANAFUNZI WAWEZE KUPATIWA ELIMU BO... + Read more »
WITO WATOLEWA KWA WAZAZI NA WALIMU WA SHULE ZA SERIKALI MANISPAA YA KINONDONI. NI KATIKA MWENDELEZO WA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA MITIHANI YA PAMOJA KWA WANAFUNZI WA DARASA LA SABA. Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kupitia idara ya elimu Msingi imeendelea na mpango wa kuandaa mitihani ya pamoja kwa wanafunzi Wa darasa la saba, ambapo leo imetangaza matokeo ya mtihani wa jaribio la pamoja uliofanyika tarehe 02-03/05/2019. Akitangaza matokeo hayo kwa niaba ya Afisa Elimu Msingi Bi Fatuma Mwiru, amewasihi Walimu na Wazazi wa shule za serikali kutilia mkazo fursa hii kwani ni maandilizi sahihi na kipimo tosha kuelekea mtihani wa Taifa. Ametoa nasaha hiyo baada ya kubaini kuwa idadi ya wanafunzi waliofanya vizuri na kupata zawadi imetawaliwa na watoto kutoka shule binafsi. "Napenda kuwasihi Wazazi na Walimu Wa shule za serikali wawe msitali wa mbele kuhakikisha watoto wanafanya vizuri katika mitihani hii maana ni dira tosha kuelekea mtihani wa Taifa" ameongeza Bi Fatuma. Aidha Bi Fatuma amesema kuwa ofisi ya Mkurugenzi kupitia idara ya Elimu Msingi ipo bega kwa bega kuhakikisha matokeo chanya yatapatikana katika mtihani wa Taifa na ndio maana Zawadi zinatolewa kwa wanaofanya vizuri ili kuleta hamasa kwa wanafunzi kusoma kwa bidii. Akitangaza matokeo hayo, amesema jumla ya wanafunzi 270 walifanya jaribio hilo la pamoja ambapo waliopata daraja A ni wanafunzi 112, daraja B ni wanafunzi 150 na daraja C ni wanafunzi 08. Katika hatua nyingine Bi Fatuma amekiri kuwa ushindani ni wa hali ya juu sana maana mtoto aliyeongoza mtihani uliopita amekosekana kumi bora lakini aliyeongoza leo mtihani uliopita hakuwepo kumi bora. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. WITO WATOLEWA KWA WAZAZI NA WALIMU WA SHULE ZA SERIKALI MANISPAA YA KINONDONI. NI KATIKA MWENDELEZO WA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA MITIHANI ... + Read more »
KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU KINONDONI, YATAKIWA KUBUNI MBINU MBADALA ZA KUONGEZA VYANZO VYA MAPATO KATIKA HALMASHAURI YAO Ushauri huo umetolewa leo na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mh.Benjamini Sitta katika kikao cha majumuisho ya ziara hiyo baada ya kutembelea miradi ya elimu kilichofanyika katika ukumbi w mikutano wa Manispaa. Amesema kamati ya huduma za uchumi, afya na elimu ndio injini ya Halmashuri kwani inagusa sekta muhimu za uchumi na afya ambazo moja kati yake isipoenda sawia basi hakuwezi kuwa na mafanikio. Amesema" Hii kamati ya Huduma za Uchumi ni ya muhimu sana, lakini mmejikita sana kwenye miradi ya elimu, mnasahau sekta muhimu ya uchumi na afya, mimi nadhani wakati umefika sasa muje na mikakati mipya ya kukuza uchumi kwa kuibua vyanzo vipya vya mapato" Mh Sitta. Akipokea ushauri huo kutoka kwa mstahiki Meya, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Thadeus Massawe ameahidi kuufanyia kazi, yeye pamoja na timu yake nzima, na kumshukuru Mstahiki Meya kwa ushauri huo wenye tija kwa Halmashauri yetu. Kamati hiyo katika ziara yake, imetembelea na kukagua miradi mitatu ya shule ambayo ni ; shule ya Msingi na awali Liberman iliyopo Kawe, Shule ya awali Del Paul iliyopo Wazo na Shule ya awali Mbweni Heights iliyopo Mbweni. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU KINONDONI, YATAKIWA KUBUNI MBINU MBADALA ZA KUONGEZA VYANZO VYA MAPATO KATIKA HALMASHAURI YAO Us... + Read more »