KOREA YA KUSINI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA MAHUSIANO KATI YAKE NA MKOA WA DAR ES SALAAM
Posted On: May 30th, 2019
NI ULE WA MIAKA MITATU UNAOHUSU KUWAJENGEA UWEZO WATAALAM WA KILIMO KATIKA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA ZA KILIMO CHA MJINI CHA KISASA .
Korea ya Kusini jimbo la Gyeongsanam imeoneshwa kuridhishwa na utekelezaji wa makubaliano yalioingiwa kati yake na Mkoa wa Dar és salaam, yahusuyo utoaji wa huduma ya mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam wa kilimo, kuhusiana na teknolojia za Kilimo chá kisasa cha mjini ili kukabiliana na changamoto zilizopo kama ufinyu wa ardhi na magonjwa ya mimea.
Hayo yamedhihirika leo wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya ujumbe kutoka korea ya kusini, waliozuru kwa lengo la kufanya majadiliano ya namna ya kuingia upya mkataba mwingine, wenye lengo la kuboresha zaidi sekta hiyo ya kilimo hasa upande wa matumizi ya teknolojia ya vifaa vya kisasa kwa matumizi madogo ya ardhi yenye tija, baada ya ule wa awali kuisha.
Akipokea ujumbe huo kutoka Korea ya Kusini, ulipozuru kituo cha kilimo Malolo Kinondoni, Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Mhe. Benjamin Sitta amesema Dar es salaam hususani Kinondoni leo imefungua ukurasa mpya wa maendeleo katika sekta ya kilimo cha mjini kwani mkataba huo uliodumu kwa miaka mitatu umeibua ari mpya ya maendeleo na kuleta mapinduzi katika sekta hii kwa kuiniua pato lá mkulima pindi atumiapo utaalam huo ulio rahisi na wamatumizi madogo ya eneo.
"Hakika mapinduzi ya kilimo cha mjini yameneemeshwa vilivyo kupitia uhusiano wetu na Korea kusini maana tumejifunza mambo mengi sana kupitia wao na tunaamini hatutaishia hapa tutaenda mbele zaidi"ameeleza Msitahiki Meya.
Naye Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji wa Mkoa Dar es salaam Dkt. Elizabeth Mshote amesema kuwa Manispaa za jiji la Dar es salaam zimenufaika vilivyo kupitia uhusiano huo na Korea kusini na kuanishia kuwa awamu ijayo itakuwa nzuri zaidi kwani ushiriki utajikita zaidi katika miundombinu ya kilimo tofauti na ule wa awali uliokuwa na lengo la kujengea uwezo wataalam hao wa kilimo.
Kwa upande wao Mr. Lee, Do Wan ambaye ni Mkurugenzi wa Division ya Ushirikiano na nchi za nje kutoka Jimbo la Gyeongsangnam na Dkt Lim Chae Shin kutoka Kituo cha mafunzo ya technologia ya kisasa ya kilimo ATEC kilichopo Mjini Jinju Korea kusini, amesema kuwa anaamini Tanzania inaweza kabisa kufikia Korea kusini maana mwitikio uliooneshwa ndani ya miaka mitatu ni wa kipekee sana na unadhirisha hamu ya mapinduzi ya kilimo ndani ya mioyo yao.
Hafla hiyo imeshirikisha wataalamu wa sekta ya kilimo kutoka Halmashauri zote tano za mkoa wa Dar es salaam, pamoja na KOICA.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
0 comments:
Post a Comment