WITO WATOLEWA KWA WAZAZI NA WALIMU WA SHULE ZA SERIKALI MANISPAA YA KINONDONI. NI KATIKA MWENDELEZO WA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA MITIHANI YA PAMOJA KWA WANAFUNZI WA DARASA LA SABA. Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kupitia idara ya elimu Msingi imeendelea na mpango wa kuandaa mitihani ya pamoja kwa wanafunzi Wa darasa la saba, ambapo leo imetangaza matokeo ya mtihani wa jaribio la pamoja uliofanyika tarehe 02-03/05/2019. Akitangaza matokeo hayo kwa niaba ya Afisa Elimu Msingi Bi Fatuma Mwiru, amewasihi Walimu na Wazazi wa shule za serikali kutilia mkazo fursa hii kwani ni maandilizi sahihi na kipimo tosha kuelekea mtihani wa Taifa. Ametoa nasaha hiyo baada ya kubaini kuwa idadi ya wanafunzi waliofanya vizuri na kupata zawadi imetawaliwa na watoto kutoka shule binafsi. "Napenda kuwasihi Wazazi na Walimu Wa shule za serikali wawe msitali wa mbele kuhakikisha watoto wanafanya vizuri katika mitihani hii maana ni dira tosha kuelekea mtihani wa Taifa" ameongeza Bi Fatuma. Aidha Bi Fatuma amesema kuwa ofisi ya Mkurugenzi kupitia idara ya Elimu Msingi ipo bega kwa bega kuhakikisha matokeo chanya yatapatikana katika mtihani wa Taifa na ndio maana Zawadi zinatolewa kwa wanaofanya vizuri ili kuleta hamasa kwa wanafunzi kusoma kwa bidii. Akitangaza matokeo hayo, amesema jumla ya wanafunzi 270 walifanya jaribio hilo la pamoja ambapo waliopata daraja A ni wanafunzi 112, daraja B ni wanafunzi 150 na daraja C ni wanafunzi 08. Katika hatua nyingine Bi Fatuma amekiri kuwa ushindani ni wa hali ya juu sana maana mtoto aliyeongoza mtihani uliopita amekosekana kumi bora lakini aliyeongoza leo mtihani uliopita hakuwepo kumi bora. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. WITO WATOLEWA KWA WAZAZI NA WALIMU WA SHULE ZA SERIKALI MANISPAA YA KINONDONI. NI KATIKA MWENDELEZO WA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA MITIHANI ... + Read more »
KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU KINONDONI, YATAKIWA KUBUNI MBINU MBADALA ZA KUONGEZA VYANZO VYA MAPATO KATIKA HALMASHAURI YAO Ushauri huo umetolewa leo na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mh.Benjamini Sitta katika kikao cha majumuisho ya ziara hiyo baada ya kutembelea miradi ya elimu kilichofanyika katika ukumbi w mikutano wa Manispaa. Amesema kamati ya huduma za uchumi, afya na elimu ndio injini ya Halmashuri kwani inagusa sekta muhimu za uchumi na afya ambazo moja kati yake isipoenda sawia basi hakuwezi kuwa na mafanikio. Amesema" Hii kamati ya Huduma za Uchumi ni ya muhimu sana, lakini mmejikita sana kwenye miradi ya elimu, mnasahau sekta muhimu ya uchumi na afya, mimi nadhani wakati umefika sasa muje na mikakati mipya ya kukuza uchumi kwa kuibua vyanzo vipya vya mapato" Mh Sitta. Akipokea ushauri huo kutoka kwa mstahiki Meya, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Thadeus Massawe ameahidi kuufanyia kazi, yeye pamoja na timu yake nzima, na kumshukuru Mstahiki Meya kwa ushauri huo wenye tija kwa Halmashauri yetu. Kamati hiyo katika ziara yake, imetembelea na kukagua miradi mitatu ya shule ambayo ni ; shule ya Msingi na awali Liberman iliyopo Kawe, Shule ya awali Del Paul iliyopo Wazo na Shule ya awali Mbweni Heights iliyopo Mbweni. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU KINONDONI, YATAKIWA KUBUNI MBINU MBADALA ZA KUONGEZA VYANZO VYA MAPATO KATIKA HALMASHAURI YAO Us... + Read more »
MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, MH.PAUL MAKONDA AFANYA ZIARA KATIKA WILAYA YA KINONDONI KUKAGUA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO. Posted On: April 15th, 2019 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda leo amefanya ziara katika wilaya ya Kinondoni kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa fedha kutoka serikali kuu ,Mapato ya ndani ya Manispaa na fedha za wadau wa nje na ndani ili kujiridhisha kwa kulinganisha taarifa anazopewa na hali halisi katika maeneo ya mradi husika ambapo pamoja na kupongeza hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa Miradi hiyo ametoa Maagizo na maelekezo mbalimbali yanayotakiwa kufanyiwa kazi ili kuboresha na kuifanya iendane na thamani halisi. Katika mradi wa ujenzi wa soko la magomeni Mhe. Mkuu wa mkoa alionesha kutoridhishwa na ubadilishaji wa dizaini ya ujenzi wa Soko hilo, hivyo amewataka Wahandisi na Wataalam wengine wanaosimamia Miradi mbalimbali ya ujenzi kutokubali Wahandisi washauri wa miradi kubadilisha dizaini ya miradi hiyo, kwani inaweza kupoteza ubora na kutoa huduma kwa wachache tofauti na lengo la serikali la kuangalia mahitaji ya sasa na baadae. Akiwa katika kituo cha Afya Kigogo, Mhe.Mkuu wa Mkoa pamoja na kuupongeza uongozi wa wa Manispaa ya Kinondoni kwa maamuzi ya busara ya kununua majengo, kuyakarabati na kujenga majengo mengine kwa matumizi ya Kituo kikubwa cha Afya kitakachohudumia zaidi ya wakazi laki moja, ameagiza kasi ya utekelezaji wake iongezwe na endapo kutakuwa na jambo linalokwamisha kuhusiana na ufuatiliaji katika Mamlaka za juu ashirikishwe Mkuu wa Wilaya kwani heshima ya Serikali kutaka kupata matokeo ya Mradi kwa wakati na sio ugumu wa kupata matokeo ya miradi inayotekelezwa. Mhe Mkuu wa mkoa alieleza kutoridhishwa na baadhi ya Barabara zinazojengwa chini ya kiwango hususani Barabara ya Mburahati ambapo pamoja na Mkandarasi kuwa nyuma ya muda wa Utekelezaji, viwango vya ubora wake sio wa kuridhisha katika upana na ubora wa mifereji ya maji ya mvua, hivyo amewataka wasimamizi wa mradi huo kuhakikisha wanafanyia kazi ili kuiwezesha kuwa katika viwango vinavyokubalika. Akizungumzia gharama za ujenzi wa miradi ya barabra hizo, Mhe. Mkuu wa Mkoa amezitaka Mamlaka husika kuliangalia suala la tofauti ya gharama za ujenzi kwa Miradi ya Barabara ya DMDP inayojengwa kwa thamani ya bilioni 2 kwa kilometa moja na zile za TANROAD na TARURA zikijengwa kwa thamani ya bilioni 1.3 kwa kilometa moja, kwani tofauti ni kubwa na fedha zinazotumika katika ujenzi ni mkopo sio msaada, hivyo akashauri kuliangalia jambo hili. Katika hatua nyingine Mhe. Mkuu wa Mkoa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo kushughulikia malalamiko ya vibarua wanaodai kupunjwa malipo yao na kampuni za ujenzi ambazo huwalipa shilingi 7500 kwa siku badala ya shilingi 12,500 kwa siku zinazotakiwa kulipwa kisheria. Katika hatua nyingine Mhe. Mkuu wa Mkoa ameshauri Fedha zilizotakiwa kutumika katika ujenzi wa kipande cha mita 200 katika Barabara ya Simu 2000 na nyingine zikajenge Barabara ya Shekilango Ubungo maziwa kupita Makaburi ya Urafiki ili kuondoa kero kwa watumiaji wa Barabara hiyo. Akiwa katika Mradi wa ujenzi wa soko la Sinza II Kata ya kijitonyama ambapo linajengwa kwa gharama ya milioni 128 zinazotokana na mapato ya ndani ya Manispaa, Mhe. Mkuu wa Mkoa amefurahishwa na Ubora wake na kutaka likamilishwe haraka na kuwaweka wafanyabiashara sambamba na kuboresha maeneo ya maegesho na njia ya kuingilia Magari Sokoni hapo. Aidha katika ziara hiyo Mhe Mkuu wa Mkoa alionesha kusikitishwa kwake na baadhi ya maeneo kuwa na mazingira machafu hivyo ameuagiza uongozi wa Manispaa kuhakikisha Maafisa Watendaji wa Kata katika maeneneo hayo kuanza kujitathmini uwezo wao katika kusimamia usafi kwani kama Watendaji Wakuu wa Maeneo husika wana wajibu wa kuwasimamia Maafisa Afya wa Kata kutekeleza kikamilifu Majukumu yao. Mwisho Mhe. Mkuu wa Mkoa amewataka wakandarasi wa Kampuni ya Scoll na Del-monte waliosimamishwa kupewa miradi ya ujenzi katika Mkoa wa Dar es salaam kwa kosa la kujenga Barabra chini ya kiwango, kuzijenga upya kwa gharama zao kama walivyoagizwa haraka iwezekanavyo ili waweze kupewa miradi mingine ambapo amempongeza Mkandarasi wa kampuni ya Delmonte anayerudia ujenzi katika barabara ya Mabatini kwa gharama zake na kwa kiwango cha kuridhisha. IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO NA UHUSIANO MANISPAA YA KINONDONI. MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, MH.PAUL MAKONDA AFANYA ZIARA KATIKA WILAYA YA KINONDONI KUKAGUA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO. Posted... + Read more »
TATHMINI YA MATOKEO YA MTIHANI WA KWANZA WA UTAMILIFU (MOCK) DARASA LA SABA KINONDONI YATOLEWA Posted On: April 12th, 2019 Akitoa tathmini hiyo leo, Afisa elimu msingi Manispaa ya Kinondoni Bw.Kiduma Mageni amesema, jumla ya shule 138, zenye wanafunzi 12, 622, walifanya mtihani huo ambao ni sawa na asilimia 99.33% na kati yake waliofaulu ni 9,302, sawa na asilimia 74.20% Amesema lengo la mtihani huu ni kutekeleza mkakati maalum wa kuhakikisha inaendelea kufanya vizuri kitaaluma hasa ikizingatiwa Kinondoni ilishika nafasi ya tatu Kimkoa kwa ufaulu wa asilimia 95.70%, matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE) 2018. "Kinondoni iliandaa mkakati maalumu wa kuendelea kufanya vizuri zaidi kitaaluma kwa kuhakikisha inaendesha mitihani miwili ya utamilifu kiwilaya kwa wanafunzi wa darasa la saba 2019 na mtihani huo ulifanyika tarehe 27-28/03/2019" Amefafanua Mageni. Aidha amezitaja shule tatu za serikali zilizofanya vizuri kuwa ni Msisiri, Victoria na Lugalo na shule za binafsi ni Royal Elite, Mother's of Mercy na Libermann. Amewataka walimu kutumia Matokeo haya kama chachu ya kurekebisha changamoto ndogondogo zilizoonekana ili kuweza kufanya vizuri mitihani ijayo ya ngazi ya Mkoa na Taifa. Katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Oysterbay na kuenda sambamba na ugawaji zawadi kwa shule zilizofanya,vizuri kutoka CRDB Bank, pia imehudhuriwa na waalimu wakuu, waratibu wa Elimu Kata pamoja na waalimu wa darasa la saba. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. TATHMINI YA MATOKEO YA MTIHANI WA KWANZA WA UTAMILIFU (MOCK) DARASA LA SABA KINONDONI YATOLEWA Posted On: April 12th, 2019 Akitoa tathm... + Read more »
KINONDONI YASAINI MAKUBALIANO YA MASHIRIKIANO NA MJI WA LOUD ULIOPO JIMBO LA HUNAN KUTOKA JAMHURI YA WATU WA CHINA. Posted On: March 29th, 2019 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni leo imetiliana saini makubaliano ya mashirikiano na mji wa Loud uliopo Jimbo la Hunan Kutoka Jamhuri ya watu wa China wenye lengo la kukuza soko la kibiashara na kuimarisha mahusiano ya kirafiki ya pande zote mbili. Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Dkt Patricia Henjewele amesema kuwa ni heshima kubwa kwa Manispaa ya Kinondoni kupokea ujumbe huo kutoka Jimbo la Hunan ukiongozwa na Peng Zheng ambae ni mkuu wa sehemu wa ofisi ya mashirikiano ya idara ya Biashara ya Jimbo la Hunan. Aliuhakikishia ujumbe huo kuwa Kinondoni inamazingira mazuri ya uwekezaji yenye vivutio mbalimbali Katika maeneo ya Afya, mazingira, Uchumi, Kilimo, Mifugo, uvuvi, makazi , Habari na Mawasiliano yatakayowezesha upanuzi wa mji na maendeleo ya mji. Ninaamini mahusiano haya yatakuwa na matokeo makubwa Katika maeneo Muhimu ya uwekaji kama vile shughuli za kibiashara, masoko, makazi, michezo , utalii, utamaduni, Elimu , Afya , Utalii, utumishi, upangaji na uboreshaji wa miji pamoja na shemu za kiburudani. Ameongeza Dkt Henjewele. Kwa upande wake Mstahiki meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Kawe Sitta alitoa shukrani za dhati kwa timu nzima iliyoshiriki kufanikisha mashirikiano hayo ikiwa ni pamoja na wizara ya fedha na mipango, idara ya uwekezaji Tanzania pamoja na Wizara ya Mambo ya nje kwa kutenga muda wao kuungana na Manispaa kufanikisha majadiliano yalipopelekea kufikia makubaliano ya mahusiano haya. Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo akishuhudia utilianaji saini makubaliano hayo ametoa shukrani zake za dhati kwa Ndugu Peng Zheng na kuuhakikishia ujumbe toka China kuwa wilaya ya Kinondoni inamazingira tulivu na hali ya hewa safi hivyo wageni waje kuwekeza wilaya ya Kinondoni yenye fursa nyingi za uwekezaji. Amesema yeye kama kiongozi mkuu wa serikali atawapa ushirikiano wa kutosha ili kufikia malengo ya makubaliano haya ya ushirikiano wa kirafiki. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari Mwasiliano na uhusiano Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YASAINI MAKUBALIANO YA MASHIRIKIANO NA MJI WA LOUD ULIOPO JIMBO LA HUNAN KUTOKA JAMHURI YA WATU WA CHINA. Posted On: March 29th... + Read more »
KINONDONI YAKABIDHIWA APATIMENTI 17 ZA MAJENGO YA UWEKEZAJI KUTOKA KWA MWEKEZAJI WA OSTERBAY VILLA. Posted On: March 18th, 2019 Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh Daniel Chongolo amepokea Apatimenti hizo ikiwa ni baada ya kufikiwa kwa makubaliano ya kimkataba Kati ya Manispaa ya Kinondoni na mwekezaji Osterbay Villa kwa mazungumzo Kati ya pande mbili kutokana na kuondoa kesi iliyodumu kwa zaidi ya miaka 8 mahakamani. Aidha kwa mijibu wa makubaliano ya mradi huu wa uwekezaji asilimia 60 ya mapato yatakuwa Chini ya Manispaa ya Kinondoni na asilimia 40 yatakuwa Chini ya Manispaa ya Ubungo. Amezitaja Apatimenti hizo Kuwa ni zile zilizopo Katika majengo ya 277 MAWENZI RD na 322 RUVU RD. Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni mhe Benjamin Kawe sitta amewapongeza wakuu wa wilaya ya Kinondoni na ubungo kwa kufanikisha makubaliano hayo yaliyowezesha kupatikana mapato yatakayotumika kugharamia huduma mbalimbali za kijamii Katika Manispaa zote mbili. Imeandaliwa na kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAKABIDHIWA APATIMENTI 17 ZA MAJENGO YA UWEKEZAJI KUTOKA KWA MWEKEZAJI WA OSTERBAY VILLA. Posted On: March 18th, 2019 ... + Read more »
TAARIFA KWA UMMA Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni leo Alhamis, March 14, 2019 katika Mkutano wake wa kawaida wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni, pamoja na mambo mengine imethibitisha matumizi ya jumla ya Tshs. 3,675,202,443.90 zilizotumika kutekeleza Miradi ya Maendeleo robo ya pili kwa kipindi cha kuanzia mwezi Octoba hadi Disemba, 2018. Kwa mujibu wa Mchanganuo wa Taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo robo ya pili, kati ya fedha hizo Tshs. 2,678,384,151.30 ni fedha za Mapato ya ndani ya Manispaa, Tshs. 510,438,100.00 ni fedha za Mfuko wa pamoja wa Afya, Tshs.176,006,913.6 ni fedha za Elimu bila malipo Msingi, Tshs. 176,053,020.00 ni fedha za Elimu bila Malipo Sekondari, Tshs. 41,050,000.00 ni fedha za Mfuko wa kuchochea Maendeleo ya Jimbo na Tshs. 93,270,259.00 ni fedha za Michango ya Jamii. Aidha Baraza la Madiwani katika Mkutano huo wa kawaida limethibitisha taarifa za utekelezaji wa kazi za Kamati za kudumu za Halmashari yaani Kamati ya Huduma za Uchumi Afya na Elimu, Kamati ya Mipangomiji na Mazingira, Kamati ya Maadili, Kamati ya Kuthibiti Ukimwi na Kamati ya Fedha na Uongozi zilizofanyika katika robo ya pili kuanzia Mwezi Oktoba hadi Disemba 2018. Imetolewa na kitengo cha Habari na Uhusiano, Manispaa ya Kinondoni. TAARIFA KWA UMMA Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni leo Alhamis, March 14, 2019 katika Mku... + Read more »