KINONDONI YAUNGANA NA HALMASHURI NYINGINE KOTE NCHINI KUADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRAPosted On: June 5th, 2021Manispaa ya Kinondoni leo imeungana na Halmashauri nyingine kote nchini, kuadhimisha siku ya mazingira duniani iliyoambatana na kauli mbiu isemayo" Tutumie nishati mbadala kuongoa mfumo Ikolojia"Akiongea katika maadhimisho hayo yaliyofanyika Kimkoa katika viwanja vya mnazi mmoja, Mkuu wa Wilaya ya Ilala kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe.Ngw'ilabuzu ludigija amesema mazingira ni uhai, hivyo yatunzwe na fukwe pia ziendelee kutunzwa na kusisistiza wakandarasi wa mazingira kulipwa kwa wakati hali itakayowaongezea ufanisi katika kutekeleza Majukumu yao.Mhe Ngw'ilabuzu amepongeza juhudi mbalimbali zinazofanywa na Halmashauri za mkoa wa Dar es salaam katika utunzaji wa mazingira na kuwataka kuongeza nguvu zaidi katika kuhakikisha mazingira yanalindwa pia.Aidha zawadi mbalimbali zimetolewa kwa shule, wadau na Mitaa iliyofanya vizuri katika utunzaji wa Mazingira.Katika maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na Jiji la Dar es salaam pamoja na Halmashauri zake nne, pia yamehudhuriwa na wadau mbalimbali na kuonesha teknolojia zao zinazotumika katika kuhakikisha mazingira yanatunzwa vizuri "Imeandaliwa naKitengo cha Habari na UhusianoManispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAUNGANA NA HALMASHURI NYINGINE KOTE NCHINI KUADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA Posted On: June 5th, 2021 Manispaa ya Kinondoni leo im... + Read more »
JENGENI UTARATIBU WA KUPIMA AFYA ILI KUJUA HATUA ZA KUCHUKUA KATIKA KUJILINDAPosted On: May 30th, 2021Rai hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mhe Abas Tarimba alipokuwa akifunga mafunzo ya siku tatu yaliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Manispaa kwa kamati ya kudhibiti maambukizi ya Virusi vya UKIMWI yenye lengo la kuwajengea uwezo katika kutekeleza majukumu yao.Amesisitiza kuwa kujua Afya ndio msingi mzima wa mstakabali utakaokutaka kuchukua hatua stahiki pindi inapotakiwa kufanya hivyo hasa ikizingatiwa takwimu kutoka mwezeshaji wa TACAIDS zinaonesha kutokuwepo na mwamko wa Jamii kuchukua hatua za Afya hali inayoashiria hatari katika ongezeko la maambukizi ya VVU.Amesema "bado baadhi ya watu hawana mwamko wa kujua afya zao, hali hii inapelekea watu waliokwishapata maambukizi ya VVU kuishi bila kufuata utaratibu wa kiafya anaotakiwa kuufuata kulingana na maelekezo ya wataalamu na hivyo kusababisha athari kubwa zaidi"Aidha Amebainisha kuwa Katika kipindi hiki cha mlipuko wa corona, tahadhari kubwa inaelekezwa jinsi ya kupambana na Corona huku watu wakijisahau kuhusu uwepo wa UKIMWI kwenye Jamii."UKIMWI upo na tunaishi nao, kila mtu azungumze na nafsi yake ili asifanye yale ambayo yanapelekea kusambaa kwa maambukizi ya UKIMWI" Ameongeza Mhe TarimbaKatika hatua nyingine ameshauri kuwa elimu zaidi itolewe kwa wale ambao wameshabainika kuwa na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ili waweze kuishi wakifuata ushauri wa wataalamu wa afya na kuendelea na shughuli zao za uzalishaji mali.Imeandaliwa naKitengo cha Habari na UhusianoManispaa ya Kinondoni. JENGENI UTARATIBU WA KUPIMA AFYA ILI KUJUA HATUA ZA KUCHUKUA KATIKA KUJILINDA Posted On: May 30th, 2021 Rai hiyo imetolewa na Mbunge wa Ji... + Read more »
MAFUNZO YA SIKU TATU YATOLEWA KWA WAJUMBE WA KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI KINONDONIPosted On: May 29th, 2021Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo shirikishi, Mwenyekiti wa Kamati ya kudhibiti UKIMWI Kinondoni ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa hiyo Mhe.Herri Misinga amesema mafunzo haya ni kwa lengo la kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati hiyo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.Amesema lengo pia ni kuwaandaa wajumbe kuwa mabalozi wazuri na ndio maana Serikali kupitia mpango wakuthibiti maambukizi ya virusi vya Ukimwi imekuwa ikisisitiza utoaji wa elimu kwa wananchi.“ Nimeambiwa mafunzo haya ni ya siku tatu, ninaamini kuwa wawezeshaji ambao wamekuja leo hii, watatoa elimu nzuri ambayo kwetu sisi itatusaidia kwenda kuwaelimisha wananchi ambao tumewawakilisha hapa, nimpongeze Mkurugenzi kwakutuandalia mafunzo haya” amesema Mhe. Misinga.Awali akimkaribisha Naibu Meya, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Bi Sipora Liana amesema kuwa anatambua umuhimu wa Kamati hiyo na kwamba anaamini elimu ya siku tatu itakayotolewa kupitia mafunzo hayo itakuwa chachu ya mafanikio katika kuhakikisha maambukizi ya virusi vya Ukimwi yanaendelea kupungua katika Manispaa hiyo hasa ikizingatiwa kwamba kunajumla ya vituo vya kupimia maambukizi ya VVU 240, ambapo kati ya hivyo vya Serikali ni 27 na vya binafsi ni 213.Kwaupande wake mratibu wa kudhibiti UKIMWI Manispaa ya Kinondoni Bi.Robby Gwesso amesema mafunzo hayo, yamehusisha warataibu kutoka TACAIDS, Manispaa ya Kinondoni, wataalamu kutoka Taasisi binafsi, Madiwani, wawakilishi kutoka makundi ya Vijana, Wazee, Asasi za kiraia, Viongozi wa dini,Watu wenye ulemavu, Watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya ukimwi pamoja na watendaji wa Manispaa ya Kinondoni. Mada zilizofundishwa ni pamoja na UKIMWI mahala pa Kazi, Sera ya taiga ya kudhibiti UKIMWI Tafsiri ya sheria ya kudhibiti UKIMWI, Sera na miongozo inayosimamia ithibiti wa VVU na UKIMWI Katika Jamii, Muundo wa kamati ya kudhibiti UKIMWI ngazi ya wilaya, kata na mtaa/ vijiji, Wajibu na majukumu ya kamati shirikishi za kudhibiti UKIMWI ngazi ya wilaya, kata na mitaa/vijiji.Nyingine ni Ukweli Kuhusu UKIMWI, kifua kikuu na Homa ya ini, Mawasiliano Kuhusu UKIMWI, utoaji wa taarifa za VVU na UKIMWI, Mpango shirikishi, ufuatiliaji na tathmini pamoja na Uongozi na ubia Katika mwitikio wa VVU na UKIMWIImeandaliwa naKitengo cha Habari na MahusianoManispaa ya Kinondoni. MAFUNZO YA SIKU TATU YATOLEWA KWA WAJUMBE WA KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI KINONDONI Posted On: May 29th, 2021 Akizungumza wakati wa ufunguzi... + Read more »
KINONDONI YAHAMASISHA USAFI WA FUKWE KUELEKEA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MAZINGIRAPosted On: May 29th, 2021 Kuelekea kilele hicho chenye kauli mbiu isemayo "Tutumie nishati mbadala kuongoa mfumo ikolojia" kinachotarajiwa kufanyika Juni 5 mwaka huu, Manispaa ya Kinondoni imeadhimsha kwa kufanya usafi Katika fukwe ya Jangwani Beach iliyopo Kata ya Kunduchi.Zoezi hilo la usafi lililoratibiwa na Diwani wa Viti maalum Mhe Jackline Kweka limefanyika wakati ambapo Kinondoni imeweka mpango mkakati wa kuhakikisha fukwe zinalindwa kwa maslahi mapana ya wananchi kwa kuhakikisha ufukuaji wa taka zilizojifukia katika eneo la fukwe unafanyika ikiwa ni pamoja na kuzisafirisha kwenda dampo.Amesema Kinondoni imejikita katika kuhakikisha suala la usafi wa Mazingira ni jukumu la kila mwananchi na kwamba kauli mbiu ya mwaka huu ikawe sehemu ya chachu katika kuhakikisha inatekelezeka.Nae Mkuu wa Idara ya Usafishaji na Mazingira Ndg Shedrack Maximilian amewasihi wananchi wanaoishi maeneo ya fukwe kujijengea utaratibu wa kusafisha maeneo hayo na kuahidi ushirikiano kutoka Manispaa wa utoaji wa vifaa na magari ya kuzolea taka pale ambapo eneo husika litahitaji.Maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja ambapo viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali wanatarajiwa kuhudhuria.Imeandaliwa naKitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAHAMASISHA USAFI WA FUKWE KUELEKEA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MAZINGIRA Posted On: May 29th, 2021 Kuelekea kilele hicho chenye ... + Read more »
TIMU MKAKATI YA KUJIANDAA KUKABILIANA NA MAAFA KINONDONI YATAKIWA KUJIKITA KATIKA KUZUIA MAAFAPosted On: May 27th, 2021Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Bi Sipora Liana alipokutana na timu mkakati ya kukabiliana na maafa yenye wataalamu 27 kwa lengo la kujadili mstakabali wa maafa katika kikao kilichofanyika ukumbi wa DMDP Kinondoni.Amesema lengo ni kukumbushana Majukumu yanayowapasa kama wataalamu kufanyika ikiwemo kuweka mikakati ya kutoa elimu zaidi ya namna ya kuzuia ama kuepuka maafa hali itakayopelekea kupungua kwa madhara makubwa pindi yakitokea."Sitaki kusikia mafuriko Kinondoni, wananchi wanapokaa mabondeni waelimishwe na uzuri huwa wanajua chanzo kinachopelekea mafuriko kwenye maeneo yao, hivyo shirikianeni nao katika kuzuia mafuriko yasitokee badala ya kusubiri janga la mafuriko litokee ndio timu ianze kuhangaika" Ameongeza Bi Sipora.Naye Mratibu wa maafa Manispaa ya Kinondoni Bi Pendo Mwaisaka alipokuwa akizungumza amebainisha maeneo ya awali yatakayopitiwa na Timu hiyo ya wataalam kutoa elimu kuwa ni maeneo ya huduma za Jamii kama Vituo vya kulelea watoto wadogo mchana na shule za Msingi na sekondari kufuatia kuripotiwa kwa changamoto za mara kwa mara za milipuko ya Moto.Timu hiyo ya kukabiliana na maafa imehusisha wataalamu kutoka Idara na vitengo vya maendeleo ya jamii, Elimu Msingi na sekondari, Masoko,Takwimu Ugavi, Sheria,Ujenzi, Biashara, Tehama, Utumishi, Afya , Mazingira pamoja na Mipango Miji.Wengine ni wataalam na wadau kutokaTanesco, jeshi la zimamoto na uokoaji, Jeshi la polisi , wakala wa mabasi yaendayo haraka (DART) Na TARURAImeandaliwa naKitengo cha Habari na UhusianoManispaa ya Kinondoni. TIMU MKAKATI YA KUJIANDAA KUKABILIANA NA MAAFA KINONDONI YATAKIWA KUJIKITA KATIKA KUZUIA MAAFA Posted On: May 27th, 2021 Rai hiyo imetolew... + Read more »
KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI AFYA NA ELIMU KINONDONI YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO.Posted On: April 22nd, 2021Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Mhe Michael Urio ambae pia ni Diwani wa Kata ya Kunduchi imekagua Ujenzi wa Soko la kisasa la Tegeta Nyuki, Ujenzi wa madarasa sita shule ya sekondari mitimirefu, Ujenzi wa kiwanja cha mpira wa miguu Mwenge na Ujenzi wa kituo cha mabasi Mwenge.Miradi mingine ni Ujenzi wa madarasa nane Katika shule ya sekondari Kijitonyama pamoja na kuangalia eneo la Ujenzi wa chumba cha kuhifadhia maiti katika kituo cha Afya Kigogo.Kamati imeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikiwa ni Pamoja na hatua zilizofikiwa na kiwango cha ubora wake.Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI AFYA NA ELIMU KINONDONI YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO. Posted On: April 22nd, 2021 Kamati hiyo chini ya Mwenyeki... + Read more »
MSTAHIKI MEYA MANISPAA YA KINONDONI MHE. SONGORO MNYONGE AKIFAFANUA JAMBO WAKATI WA BARAZA LA MADIWANIPosted On: March 17th, 2021Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe Songoro Mnyonge akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya Manispaa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani robo ya pili ya mwaka wa fedha 2020/2021 ambapo aliwataka Waheshimiwa Madiwani kushirikiana na wadau mbalimbali katika maeneo yao kutatua kero za wananchi.Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na UhusianoManispaa ya Kinondoni.MatangazoTANGAZO KUHUSU VIBANDA VYA MWENGEFebruary 22, 2021TAARIFA KUHUSIANA NA WASTAAFU WANAOLIPWA NA HAZINAFebruary 18, 2021TANGAZO KUHUSU WAMILIKI WA KUMBI ZA BURUDANI, SHEREHE NA BAAJanuary 22, 2021HAWA HAPA WADAIWA SUGU WA LESENI ZA BIASHARA MANISPAA YA KINONDONIDecember 04, 2020Tazama zoteHabari mpyaMSTAHIKI MEYA MANISPAA YA KINONDONI MHE. SONGORO MNYONGE AKIFAFANUA JAMBO WAKATI WA BARAZA LA MADIWANIMarch 17, 2021 UWASILISHWAJI WA TAARIFA ZA KAMATI ZA KUDUMU-BARAZA LA MADIWANI.March 17, 2021 MKURUGENZI WA MAISPAA BI SIPORA LIANA AKITOA UFAFANUZI WA JAMBO WAKATI WA BARAZA LA MADIWANI.March 17, 2021 HABARI KATIKA PICHA-MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI.March 17, 2021Tazama zote MSTAHIKI MEYA MANISPAA YA KINONDONI MHE. SONGORO MNYONGE AKIFAFANUA JAMBO WAKATI WA BARAZA LA MADIWANI Posted On: March 17th, 2021 Mstahik... + Read more »