Baraza la madiwani wakiwa katika baraza hilo 13/11/2014 ambapo taarifa utekelezaji wa shughuli za za kamati mbalimbali zilitolewa na kuthibitishwa na Baraza hilo zikiwemo taarifa za kamati ya Fedha na uongozi,kamati ya kudhibiti ukimwi,kamati ya mipango miji na mazingira na kamati ya huduma za Uchumi,Afya naElimu .Pamoja na hayo pia ilitolewa taarifa ya utendaji kazi ya wakuu wa Idara na vitengo robo ya kwanza kipindi cha julai -septemba.Pichani ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mheshimiwa Yusuph Mwenda ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo akiendesha kikao hicho.
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni leo 7/9/2014 imeendesha semina kwa wachezaji wa timu ya KMC-FC ambapo wachezaji hao wamefundishwa juu ya sheria mbalimbali zinazowahusu wachezaji .Akiongea katika semina hiyo Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Eng.Mussa Natty amewataka wachezaji hao kuzingatia mafunzo hayo ili kuepuka uvunjwaji wa sheria katika mchezo huo wa mpira wa miguu na kuzingatia nidhamu.
Akitoa mafunzo hayo mkufunzi kutoka Bodi ya ligi kutoka TFF ndugu Lesle
Liunda amezichambua kwa undani sheria hizo na kuwasisitizia wachezaji
hao utii wa sheria ili kuepuka adhabu mbalimbali ambazo zinaweza
kugharimu matokeo ya mchezo na hata kusababisha timu kushindwa kufikia
malengo yake.
Timu ya KMC -FC ni timu ambayo ipo katika daraja la kwanza na tayari
imeshafanya usajili kushiriki katika ligi inayotarajiwa kuanza hivi
karibuni.
Picha ikionyesha Mkufunzi Lesle Liunda akisisitiza jambo wakati wa
mafunzo hayo huku Mkurugenzi wa Manispaa pamoja na Mratibu wa Timu hii
ya Manispaa wakisikiliza kwa makini
0 comments:
Post a Comment