RC MAKONDA: KINONDONI NI MFANO WA KUIGWA KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO.Posted On: June 29th, 2020Halmashauri za Mkoa wa Dar es salaam zimetakiwa kuiga mfano wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kutumia vyanzo vya mapato ya ndani, Serikali kuu pamoja na wadau kama ilivyotekelezwa katika Manispaa ya Kinondoni.Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili kwa jimbo la Kinondoni na Kawe yenye lengo la kukabidhi miradi kwa kamati ya siasa ya Mkoa.Amesema kuwa kila Halmashauri katika Mkoa wa Dar es Salaam inakusanya mapato hivyo zinapaswa kutekeleza miradi ambayo itaaacha alama kama ambavyo Manispaa ya Kinondoni imeweka alama katika miradi mikubwa ya Maendeleo chini ya Serikali ya awamu ya Tano ya Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli pamoja na usimamizi mzuri wa Mkurugenzi mzalendo Ndg. Aron Kagurumjuli."Kinondoni nawapongeza sana, mmefanya kazi inayoonekana nakuacha alama kwa Wananchi, kipindi cha nyuma haya mambo hayakuwepo licha ya kwamba Manispaa zilikuwa zinakusanya mapato lakini katika uongozi wa miaka mitano ya Dk. Magufuli mmeitendea haki ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), " amesema Makonda.Akizungumzia mradi wa Soko la kisasa la Magomeni, Mhe. Makonda amesema soko hilo lililojengwa kwa fedha kutoka Serikali kuu, ni chanzo kikubwa cha mapato katika Manispaa ya Kinondoni litakaloongeza hadhi ya wafanyabishara watakaoendesha shuguli zao bila kubugudhiwa.Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mhe. Chongolo amesema kuwa katika Wilaya hiyo Mkurugenzi pamoja na timu yake wamefanikiwa kukamilisha miradi kwa wakati na kwamba wanapoikabidhi kwa kamati hiyo inatoa fursa kuendelea kutekeleza miradi mingine.Katika Ziara hiyo Mhe. Makonda ametembelea miradi mbalimbali ambayo ni ujenzi wa Hospital ya Wilaya iliyopo Mabwepande, Kiwanda Cha kuchakata taka, Shule ya wasichana Mabwe Tumaini na Zahanati ya Bunju.Miradi mingine ni ujenzi wa matanki ya Maji , ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Shekilango hadi Bamaga, Soko la Kisasa Magomeni, Kituo Cha Afya kigogo, Zahanati ya Mikoroshini ,Uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu Mwenge pamoja na Stedi ya daladala iliyopo Mwenge.Imeandaliwa na,Kitengo Cha Habari na MahusianoManispaa ya Kinondoni. RC MAKONDA: KINONDONI NI MFANO WA KUIGWA KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO. Posted On: June 29th, 2020 Halmashauri za Mkoa wa Dar es sa... + Read more »
KINONDONI YAPONGEZWA KWA KUJENGA UWANJA WA MPIRA WA KISASA, TIMU KUBWA ZATAKIWA KUIGA MFANO.Posted On: June 25th, 2020Manispaa ya Kinondoni imepongezwa kwa ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu wenye uwezo wa kuchukua takriban idadi ya mashabiki 3600 kwa mara moja.Pongezi hizo zimetolewa na Naibu wa Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Josephat Kandege wakati wa ziara yake katika Halmashauri hiyo kushuhudia uwanja huo wa kisasa ukijengwa katika eneo la Mwenge kwa mapato ya ndani utakaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 2.2 hadi kukamilika kwake.Amesema kuwa mradi huo utakapokamilika utawezesha timu ya mpira ya Manispaa hiyo (KMC FC) kupata faida kubwa na hivyo kujiendesha yenyewe kupitia mapato yatakayokusanywa katika uwanja,na kuzitaka timu kubwa ambazo hadi sasa hazina viwanja kuiga mfano huo.“Niwapongeze sana Kinondoni, kwakujenga uwanja huu, utakapomalizika najua faida yake ipo wazi kabisa, kwanza inapendezesha, lakini pia inaleta changamoto kwa Halmashauri nyingine na timu kubwa kuiga kwenu, kama timu ya Kinondoni inaweza kuwa na uwanja wa kisasa wao wanashindwa nini” amesema Mhe. Kandege.Hata hivyo Mhe. Kandege ameipongeza timu ya KMC FC kwakuendelea kufanya vizuri katika michezo yake na kusema kuwa kwa mwenendo huo hivi sasa inanafasi kubwa ya kushiriki ligi kuu katika msimu ujao.Imeandaliwa nakitengo cha Habari na MahusianoHalmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAPONGEZWA KWA KUJENGA UWANJA WA MPIRA WA KISASA, TIMU KUBWA ZATAKIWA KUIGA MFANO. Posted On: June 25th, 2020 Manispaa ya Kinondon... + Read more »
TAMISEMI YARIDHISHWA NA MATUMIZI MAZURI YA FEDHA ZA MAPATO YA NDANI KATIKA MIRADI YA MAENDELEO KINONDONIPosted On: June 25th, 2020Hayo yamebainishwa na Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Josephat Kandege alipozuru Kinondoni kwa lengo la ukaguzi wa miradi ya maendeleo, kujiridhisha na hatua za utekelezaji wake unaoenda sambamba na thamani ya fedha na ukamilishaji wa viwango kwa wakati.Amesema kuwa Manispaa hiyo ni mfano wakuigwa kwa kuwa imeonesha nidhamu nzuri katika matumizi ya fedha zinazotokana na vyanzo vya mapato ya ndani na kwamba miradi ambayo imetekelezwa kupitia fedha hizo inaendana na thamani halisia. “Kimsingi leo nimemaliza ziara yangu katika Halmashauri hii, na kikubwa nilikuwa nimelenga zaidi kuona fedha zinazokusanywa na Halmashauri na namna ambavyo zinatumika katika miradi ambayo inaonekana na kimsingi naomba niwapongeze sana Kinondoni, mnazitendea haki fedha zenu mnazokusanya” amesema Mhe. Kandege.Kadhalika Mhe. Kandege ameridhishwa na kiwango cha barabara zinazojengwa katika Halmashauri hiyo kupitia mradi wa DMDP na kusema kuwa kukamilika kwake kutaleta mafanikio makubwa kwa wananchi hususani watumiaji wa barabara ya Shekilango na kwamba itaondoa msongamano wa daladala na kuwawezesha wananchi kuondokana na adha ya foleni.Amefafanua kuwa Mafanikio haya yanayoonekana leo Kinondoni ni kutokana na uongozi imara wa Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na usimamizi mzuri wa Mkurugenzi ndg. Aron Kagurumjuli ulioleta tija kwa Wananchi.Katika hatua nyingine Mhe.Kandege ameipongeza Manispaa ya Kinondoni kwa kujenga kituo cha Afya katika Kata ya Kigogo na kusema kuwa walifanya mamuzi ya busara na yakujali wananchi kwakuwa eneo hilo halikuwa na Hospitali na kwamba litawasaidia wakazi hao kupata huduma bora ya afya. “Kinondoni mliona mbali kuweka kituo cha Afya pale Kigogo, mlitumia busara ya hali ya juu mkaona ni bora mnunue eneo kwa ajili ya kuwajengea wananchi kituo cha Afya, hivyo hata kwenye Kata ya Kawe kwa ujumla ukiondoa Kawe kama Kawe eneo lililobaki halikuwa na kituo cha Afya, pamoja na ujenzi wa Hopsitali ya Wilaya nilazima uwe navituo hivi ili hata mgonjwa wa eneo jirani apate huduma.Katika ziara hiyo Mhe. Kandege ametembelea Barabara ya shekilango inayojengwa kwa kiwango cha lami kwa shilingi Bilioni 14. 8, mfereji wa Kilongawima uliyopo Jimbo la Kawe kwa shilingi Bilioni 3.1 pamoja na upanuzi wa Zahanati ya Bunju mradi unajongekwa cha shilingi Milioni 600.Imeandaliwa naKitengo cha Habari na MahusianoHalmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. TAMISEMI YARIDHISHWA NA MATUMIZI MAZURI YA FEDHA ZA MAPATO YA NDANI KATIKA MIRADI YA MAENDELEO KINONDONI Posted On: June 25th, 2020 Hayo yam... + Read more »
KINONDONI YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2015-2020, KWA VITENDOPosted On: June 19th, 2020Pongezi hizo zimetolewa na Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni kwenye kikao cha majumuisho baada ya ziara ya siku mbili ya ukaguzi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.Akizitoa pongezi hizo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya kinondoni Ndg Arold Maruma amesema Kinondoni imeonesha uzalendo katika kuhakikisha ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 hadi 2020, inatekelezwa kwa vitendo kwa kutumia makusanyo yao ya Ndani, Fedha kutoka Serikli kuu pamoja na Fedha kutoka kwa wadau wa maendeleo. "Kinondoni kwakweli mmeitendea haki ilani ya uchaguzi ya CCM kwa mwaka 2015-2020, miradi mliotekeleza hapa ni mfano wa kuigwa na mmeacha taswira inayoonekana kwa Wananchi." Ameongeza Mwenyekiti.Aidha amebainisha kuwa thamani halisi ya fedha imeonekana Katika miradi hiyo kwani mbali na kutumia fedha za ndani, Serikali kuu na wadau, lakini pia kiasi kilichotumika katika ukamilishaji wake vinaenda sambamba na ubora .Awali akikabidhi ripoti ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa Mwenyekiti wa CCM, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amesema Kinondoni imeweza kufanikiwa kukamilisha miradi hiyo kutokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya ofisi yake, Ofisi ya Mkurugenzi na Mstahiki Meya.Ameongeza kuwa viongozi hawa wa Manispaa na timu zao wamekuwa na lengo moja la kuiletea Halmashauri hii maendeleo kwa kuwapatia na kusimamia vyema miradi ambayo inakwenda kumaliza changamoto mbalimbali za Wananchi.Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndugu Aron Kagurumjuli amesema kuwa Halmashauri imekuwa na utaratibu wa kutenga asilimia 60 ya mapato yake ya ndani na kuipeleka kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo na asilimia 40 inayobaki kutumika katika matumizi mengine ya kuendesha Halmashauri.Miradi iliyotembelewa na kamati hiyo ni pamoja na ujenzi wa Jengo la Utawala la Halmashauri, Ujenzi wa soko la kisasa la magomeni, Ujenzi wa kituo Cha afya Cha kigogo, Ujenzi wa barabara ya akachube, Ujenzi wa zahanati ya Magomeni, zahanati ya Makumbusho , Ujenzi wa uwanja wa mpira wa kisasa uliopo mwenge na Ujenzi wa stendi ya kisasa ya daladala.Mingine ni ujenzi wa Kiwanda Cha kuchakata taka na kutengeneza mbolea mboji kilichopo mabwepande, Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya iliyopo Mabwepande, Shule ya sekondari ya wasichana ya kidato Cha tano na sita Mabwe Tumaini girls, Upanuzi wa kituo cha afya Bunju na Ujenzi wa shule ya Msingi Mkoani.Imeandaliwa naKitengo Cha habari na UhusianoManispaa ya kinondoni. KINONDONI YAPONGEZWA KWA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2015-2020, KWA VITENDO Posted On: June 19th, 2020 Pongezi hizo zimetolewa n... + Read more »
KINONDONI KUTEMBELEWA NA RC MAKONDA UKAGUZI MIRADI YA MAENDELEOPosted On: June 18th, 2020Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda anatarajiwa kufanya ziara ya siku mbili katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni yenye majimbo mawili, kuanzia Juni 20 hadi 21 mwaka huu itakayohusisha ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayoenda sambamba na utekelezaji wa Ilani ya UchaguziAkizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amesema kuwa miradi hiyo ni ile iliyotekelezwa kwa kipindi cha Miaka mitano ya Uongozi wa Rais Mhe. Dkt John Pombe Joseph Magufuli, ambayo imetekelezwa kwa fedha ambazo ni vyanzo mbalimbli ikiwemo mapato ya ndani, Serikali Kuu na Wadau.Amesema kwa kufanya hivyo ni kuonesha uzalendo hasa ikizingatiwa miradi hiyo imetekeleza kwa kiwango kilichokusudiwa na kukamilika kwa ubora na wakati uliopangwa.“Miradi hii ambayo Manispaa imetekeleza nikutokana na dhamana ambayo CCM imetupatia na hivi sasa tunakwenda kukiabidhi ,nasio hii tu ambayo tumeitaja , Manispaa ya Kinondoni inamiradi mingi mikubwa ambayo imefanyika ila hii tumeichagua kama alama ya uwasilishwaji wa majukumu yetu” amesema Mhe.Chongolo.Ameitaja miradi ambayo itatembelewa kwa Jimbo la Kawe kuwa ni umaliziaji wa Hospitali ya Wilaya iliyopo Mabwepande, jengo la Mama na Mtoto RCH, nyumba ya watumishi wa Hospitali hiyo, Shule ya Sekondari ya wasichana Tumaini, Kiwanda cha kuchakata taka kilichopo Mabwepande, Kituo cha Afya Bunju, ujenzi wa mantaki matano ya maji yenye ujazo wa mita milioni saba pamoja na Zahanati ya Mikoroshini. Kwa upande wa Jimbo la Kinondoni Miradi itakayotembelewa ni ujenzi wa Kiwanja cha kisasa cha mpira kilichopo Mwenge, Kituo cha daladala Mwenge, Soko la Sinza Africasana, ujenzi wa Barabara ya Moroco mwenge yenye urefu wa kilomita 4.2, Hospitali ya Mwananyamala jengo la Mama na Mtoto, Kituo cha Afya cha Kisasa Kigogo kilichojengwa kwa ghorofa tano, shule ya Sekondari Mzimuni kwa ngazi ya Ghorofa mbili pamoja na Soko la Kisasa Magomeni.Katika hatua nyingine , Mkuu huyo wa Wilaya Kinondoni amesema kuwa Manispaa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeweza kuboresha miundombinu ya sekta muhimu za Afya pembezoni mwa mji iliyopeleke wananchi kupata huduma za afya kwa urahisi, na ile ya elimu kwa wenye uhitaji maalumu hali iliyofanikisha makundi haya maalumu kupata huduma stahiki.Imeandaliwa naKitengo cha Habari na UhusianoManispaa ya Kinondoni. KINONDONI KUTEMBELEWA NA RC MAKONDA UKAGUZI MIRADI YA MAENDELEO Posted On: June 18th, 2020 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda ... + Read more »
ZOEZI LA UGAWAJI WA HATI ZA VIWANJA KWA WANANCHI WA NYAKASANGWE KUANZA RASMIPosted On: June 17th, 2020Zoezi hilo la ugawaji wa hati za viwanja kwa wakaazi wa maeneo ya Nakasangwe ni kufuatia ukamilishaji wa upimaji viwanja 9741vya wananchi hao walioendeleza maeneo kiholela hali iliyopelekea tatizo sugu la uvamizi.Zoezi hilo limetangazwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo alipokuwa akiongea na wananchi wa Nakasangwe, katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo viwanja vya shule ya msingi Nakasangwe.Amesema kwa kuwamilikisha Wananchi maeneo yao kisheria kutapunguza na kumaliza kabisa migogoro ya ardhi iliyokuwa ikiwakabili siku za nyuma."Ninafahamu Katika kata hizi za pembezoni hususani Mabwepande kumekuwa na watu wachache wanaojishughulisha na uvamizi wa maeneo na kuwauzia Wananchi hali inayopelekea migogoro, Nipende tuu kuwakumbusha kuwa magereza zetu nchini zinahitaji nguvu Kazi, serikali haitokubali kuwaacha watu Hawa waendelee kusababisha migogoro kwenye maeneo yetu."Naye mkuu wa Idara ya Ardhi na Mipango Miji Manispaa ya Kinondoni Ndg. Maduhu Kazi amesema ugawaji huo wa hati ni kufuatia utekelezaji wa maagizo ya Serikali yanayozitaka Manispaa kupima meneo yote yalioendelezwa kiholela.Amesema viwanja vilivyopimwa ni 9741 ambapo kulikuwa na makundi ya wenye migogoro na wasio na migogoro na kuwataka wanachi kufahamu kuwa ugawaji wa hati unaoanza kesho utahusisha maeneo ambayo hayakuwa na changamoto za migogoro.Katika hatua nyingine, Mhe.Chongolo ameagiza wataalamu wa Manispaa kuanza kupima mtaa wa Mbopo uliopo Kata ya Mabwepande ndani ya siku 14, na kuwataarifu wanachi wanaosababisha migogoro kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.Zoezi la upimaji wa viwanja ni endelevu na litafanyika kwa awamu likihusisha maeneo yote yaliyoendelezwa kiholela.Imeandaliwa naKitengo Cha habari na uhusianoManispaa ya Kinondoni. ZOEZI LA UGAWAJI WA HATI ZA VIWANJA KWA WANANCHI WA NYAKASANGWE KUANZA RASMI Posted On: June 17th, 2020 Zoezi hilo la ugawaji wa hati za viw... + Read more »
MKURUGENZI KINONDONI AWATAKA BVR KITS OPERATORS, KUZINGATIA KANUNI NA TARATIBU ZA UBORESHAJI DAFTARI AWAMU YA PILIPosted On: May 1st, 2020Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeanza zoezi la uboreshaji awamu ya pili wa daftari la kudumu la mpiga kura ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ambaye ndio Afisa mwandikishaji bwana Aron Kagurumjuli amesema wamejipanga vilivyo katika uboreshaji huo.Kagurumjuli ametoa kauli hiyo wakati wamafunzo ya kuwajengea uwezo mbalimbali kuhusu namna ya kuwahudumia wananchi wanaokuja kuboresha taarifa zao sambamba na namna ya kutumia mashine wakati wa kuchukua picha kwa ajili ya kutoa vitambulisho. Kagurumjuli amesema kuwa Halmashauri yake imejipanga vizuri katika mchakato huo na kwamba inategema matokeo mazuri ya mwitikio wa wananchi kama ilivyokuwa kwa awamu ya kwanza kutokana na kuwepo kwa ushirikiano madhubuti baina ya AROKATA pamoja na watendaji wengine wa Hamashauri hiyo.Ameongeza kuwa mchakato huo ni mahususi kwa ajili ya kuwapatia wananchi vitambulisho vyao na kuwataka wale ambao walipitwa na mchakato huo kwa awamu ya kwanza kujitokeza sasa ili waweze kupata vitambulisho vyao. “ Nawapongeza wote mliopata nafasi hii, kiapo mlichokula hapa ni cha uaminifu na uadilifu, mnakwenda kuwahudumia wananchi, niwasihi hatuhitaji muende kinyume na maelekezo ambayo mnapewa na watalaamu wetu kwenye mafunzo haya, wahudumieni wananchi vizuri” amesema Kagurumjuli.Aidha Kagurumjuli amewataka watumishi hao kuzingatia maelekezo wanayopewa na watalaamu kuhusu namna ya kumuhudumia mwananchi hasa katika kipindi hiki cha ugonjwa wa mlipuko wa homa ya mapafu unaosababishwa na Virusi vya COVID 19 (Corona) ikiwemo kunawa mikono na maji tiririka pamoja na kupaka vitakasa mikono (Sanitizer).Amesema kuwa katika kila kituo kutakuwa na watu ambao watakuwa ni mahususi kwa ajili ya kuwanawisha mikopo pamoja na kuwapaka vitakasa mikono ili kuwakinga na maambukizi ya ugonjwa huo.Kagurumjuli amefafanua kuwa zoezi hilo la uandikishaji litaanza rasmi Mei mbili na kumalizika Mei Nne mwaka huu na kwamba wote ambao hawakupata nafasi ya kujiandikisha awamu ya kwanza wanaruhusiwa kwenda kwenye vituo vyao kwa ajili ya kujiandikisha. Imeandaliwa na kitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni MKURUGENZI KINONDONI AWATAKA BVR KITS OPERATORS, KUZINGATIA KANUNI NA TARATIBU ZA UBORESHAJI DAFTARI AWAMU YA PILI Posted On: May 1st, 2020 ... + Read more »