ELIMU YATOLEWA KUHUSIANA NA MABORESHO YA BARABARA -CHINI YA DMDP, KATIKA MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA SHEKILANGO -BAMAGA Posted On: August 24th, 2019 Elimu hiyo imetolewa leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya ofisi ya Afisa mtendaji Sinza ukiwahusisha wananchi wa Sinza A, B, C, D na E ambao ndio walengwa mahususi wa mradi. Katika mkutano huo wa hadhara ilielezwa kuwa Lengo kuu ni kuutambulisha mradi na kutoa elimu na ushauri utakaoweka Mazingira rafiki yatakayowezesha utekelezwaji wake, kwa kuzingatia weledi, ufanisi na ubora uliokusudiwa. Akiambatana na timu ya wasimamizi wa mradi huo, Bi. Pendo Fred, ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Kinondoni amesema, ni vema kuundwa kamati za watu watano kila mtaa kwa lengo la kutoa taarifa stahiki kuhusiana na mradi mzima ikihusisha faida zitakazopatikana wakati na baada ya mradi kukamilika, kwani hiyo ndiyo njia sahihi itakayomwezesha mwananchi yeyote kutoa ushirikiano pale inapobidi, na pia kujua nini wajibu wake na namna ya kutoa taarifa ikiwa kutakuwa na shida yoyote inayoweza kuzalishwa na mradi wakati wa utekelezaji. Kwa upande wake Diwani wa kata ya Sinza Mhe Godfrey Chikandamwali amewashukuru na kuwaahidi wasimamizi wa mradi huo kuendelea kuwaunga mkono kwa kuwa miradi yote ni kwa faida ya wananchi na kusema jukumu walilofuata katika mkutano huo ni jema. Mradi huo utahusisha barabara ya Shekilango mpaka Bamaga awamu ya saba kwa urefu wa km 3.7 kwa usimamizi wa kampuni ya China Road and Bridge Corporation ambao tayari ulishaanza kutekelezwa tangu July 2019, na utakamilika Octoba 2019. Imeandaliwa na Kitngo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. ELIMU YATOLEWA KUHUSIANA NA MABORESHO YA BARABARA -CHINI YA DMDP, KATIKA MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA SHEKILANGO -BAMAGA Posted On: Aug... + Read more »
SERIKALI YAPONGEZA MAONESHO YA NANE NANE KANDA YA MASHARIKI Posted On: August 8th, 2019 NI KUTOKANA NA JUHUDI WANAZOZIFANYA KATIKA KUINUA NA KUKUZA UCHUMI WA NCHI KUPITIA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI. Pongezi hizo zimetolewa leo na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, alipokuwa mgeni rasimi katika kilele cha maadhimisho ya nane nane kanda ya Mashariki yaliyofanyika katika viwanja vya Mwl J K Nyerere Mkoani Morogoro. Amesema ili Uchumi wa nchi ukue, tunategemea viwanda, na malighafi ambazo nyingi tunazipata mashambani, hivyo kwa kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Tanga, Pwani Dar es salaam na Morogoro kwa kauli mbiu isemayo "Kilimo, mifugo na uvuvi kwa ukuaji wa Uchumi wa nchi ", imetekelezeka. "Tunapozungumzia suala la kukuza uchumi wa Nchi kama kauli mbiu yetu inavyoelekeza kwa mwaka huu tunahitaji kuboresha sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi, na hili nimeliona nilipotembelea mabanda mbalimbali hapa, nawapongeza kwa jitihada mnazofanya" amesema Mhe Makamu wa Rais. Pamoja na kuwapongeza viongozi wanaounda ukanda huo, Makamu wa Rais amesisitiza pia juhudi hizo zisiishie kwenye mabanda ya nanenane pekee bali zifikie wananchi wote ambao wanatakiwa kuona mifano halisi kwa viongozi wao wanaowapa mafunzo. Aidha katika maonesho hayo ya 26,Manispaa ya Kinondoni imeshika nafasi ya pili huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na Manispaa ya Ilala. Imeandaliwa na Kitengo cha Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. SERIKALI YAPONGEZA MAONESHO YA NANE NANE KANDA YA MASHARIKI Posted On: August 8th, 2019 NI KUTOKANA NA JUHUDI WANAZOZIFANYA KATIKA KUIN... + Read more »
KUELEKEA KILELE CHA MAAZIMISHO YA SHEREHE ZA MAONESHO YA NANENANE YENYE KAULI MBIU ISEMAYO "KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KWA MAENDELEO YA UKUAJI WA UCHUMI WA NCHI , TEMBELEA BANDA LA KINONDONI UPATE ELIMU KUHUSINA NA UFUGAJI WA NGOMBE NA MBUZI WA MAZIWA NA NYAMA, KUKU WA KIENYEJI NA CHOTARA, UFUGAJI WA SUNGURA NA USHAURI WA UCHIMBAJI WA MABWAWA BORA YA SAMAKI NA KILIMO BORA CHA MBOGAMBOGA NJOO UJIFUNZE KUTOKA KWA WATAALAMU WALIOBOBEA. Banda la manispaa ya Kinondoni ambalo yake kuna mfereji uliotengenezwa kama bwawa dogo kwaajili ya kuonesha ufugaji wa samaki wa kisasa na kuna samaki aina ya kambale wa kutosha watu wanaotembelea kujionea bidhaa mbalimbali katika banda la Kinondoni Shamba la mboga mboga Banda la kuku wa kisasa Shamba la mahindi na mbele yake kuna shamba la zao la mikunde Shamba la migomba Ng"ombe wa maziwa KUELEKEA KILELE CHA MAAZIMISHO YA SHEREHE ZA MAONESHO YA NANENANE YENYE KAULI MBIU ISEMAYO "KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KWA MAENDELEO YA UK... + Read more »
MWENGE WA UHURU MWAKA 2019, WILAYA YA KINONDONI UMEZINDUA, UMEWEKA JIWE LA MSINGI NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO 8 YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI THEMANINI Posted On: July 20th, 2019 Miradi iliyozinduliwa na mwenge wa Uhuru ni pamoja na mradi wa uwezeshaji wananchi kiuchumi wenye gharama ya zaidi ya Milioni 50. Mradi wa ujenzi wa Barabara ya Kilongawima kiwango Cha lami yenye urefu wa km 2 wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 2, Mradi wa Ujenzi wa kituo Cha Afya kigogo wenye thamani ya Zaidi ya Milioni 700. Miradi mingine ni mradi wa Ujenzi wa shule mpya ya Mivumoni uliogharimu Zaidi ya Milioni 200, Mradi wa Ujenzi wa Tanki la maji na miundombinu yake wenye gharama ya Zaidi ya Bilioni 75, Kiwanda cha ushonaji nguo wenye gharama ya kiasi Cha sh Milioni 500 na Ujenzi wa soko la Kijitonyama wenye gharama ya Zaidi ya shillingi Milioni 100. Aidha Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Mzee Mkongea Ally ameipongeza Kinondoni kwa kubuni na kusimamia vizuri miradi hiyo ya maendeleo ambayo itakuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi wa Kinondoni. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. MWENGE WA UHURU MWAKA 2019, WILAYA YA KINONDONI UMEZINDUA, UMEWEKA JIWE LA MSINGI NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO 8 YENYE THAMANI YA ZAIDI Y... + Read more »
TAMISEMI KWA KUSHIRIKIANA NA WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA YAUNGA MKONO JITIHADA ZA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU KINONDONI Posted On: July 10th, 2019 NI KUPITIA MPANGO WA LIPA KUTOKANA NA MATOKEO (EP4R), KWA KUTOA MILIONI 75, KUKAMILISHA UJENZI WA MIUNDOMBINU SHULE YA MSINGI KISAUKE. Akifafanua mpango huo wenye dhamira ya dhati ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Halmashauri kuboresha miundombinu ya elimu katika kikao cha wazazi kilichofanyika shuleni hapo, Kaimu Afisa Elimu msingi Bi Chitegetse Dominik amesema TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na teknolojia imefikia uamuzi huo baada ya kuridhishwa na juhudi za Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni katika azma yake ya ujenzi na uboreshaji wa vyumba 100,vya madarasa kwa kushirikiana na wadau pamoja na wananchi katika Wilaya yake. Amesema miundo mbinu ya shule ya msingi kiasuke haikuwa rafiki kwa mfumo mzima wa elimu, kwani changamoto kubwa ilikuwa ni upungufu wa vyumba vya madarasa, vyoo vya waalimu na wanafunzi, pamoja na ofisi ya waalimu. "Kutokana na adha hiyo imemlazimu mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Daniel Chongolo kuleta mradi wa kujenga vyumba sita vya madarasa, ofisi ndogo ya mwalimu mkuu ikiwa na choo chake pamoja na vyoo viwili vya walimu ili aweze kupunguza msongamano wa wanafunzi kwenye darasa Moja na kupunguza usumbufu wa wanafunzi kuvuka barabara mara kwa mara kwenda kusomea kwenye madarasa yaliyoazimwa toka shule ya sekondari ya jirani".Amefafanua Chitegetse. Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bi. Pellagia Mdimi akitoa taarifa ya shule yake amesema inayo jumla ya wanafunzi 1886, ambapo wanaume ni 915 na wanawake ni 971 na kuainisha changamoto zilizopo kuwa ni msongamano wa wanafunzi kwenye madarasa, upungufu wa vyoo pamoja na ofisi ya waalimu. Kwa nyakati tofauti wazazi wa wanafunzi wanaosoma shule ya Msingi kisauke wamepongeza juhudi za Serikali pamoja na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni kuona changamoto zilizopo mashuleni na kufikia hatua ya kuzifanyia kazi, ikiwa ni pamoja na kupunguza changamoto zilizokuwa zinawakabili watoto wao. Miradi hiyo inatarajiwa kufikia mwezi wa tisa iwe imekamilika ili wanafunzi pamoja na waalimu waweze kunufaika kwa kuwapatia elimu iliyobora na sio bora elimu. Imeandaliwana Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni TAMISEMI KWA KUSHIRIKIANA NA WIZARA YA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA YAUNGA MKONO JITIHADA ZA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU KINONDONI ... + Read more »
RAI YATOLEWA KWA WANANCHI KINONDONI KUSHIRIKI KWA PAMOJA KUANGAMIZA MAZALIA YA MBU, ILI KUWEZA KUJIKINGA NA UGONJWA WA DENGUE Posted On: July 4th, 2019 Rai hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika ziara yake Manispaa ya Kinondoni kwa lengo la kushiriki zoezi la unyunyuziaji wa viuadudu (biolarvicides) kwa mazalia ya mbu ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono zoezi la uhamasishaji wa udhibiti wa ugonjwa huo katika Wilaya hiyo. Amesema swala la uwajibikaji udhibiti wa mazalia haya ya mbu ni ya kila mwananchi, kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia si tu kuondokana na ugonjwa wa Dengue, bali pia magonjwa mengine kama vile Malaria, zika, matende, Atikungunya na homa ya manjano. Amesema "Kwanza niipongeze Manispaa ya Kinondoni kwa kuonesha jitihada za kuhakikisha wanadhibiti ugonjwa huu wa Dengue kwa kununua mashine na viuadudu hivi ambavyo leo tunapulizia dawa, katika kupambana na mazalia ya mbu lakini pia niwapongeze kwa kupunguza idadi ya wagonjwa wapya wa homa ya Dengue kutoka 45 kwa siku mwezi April mpaka kufikia wagonjwa 17 kwa siku mwezi June" Waziri Ummy. Naye Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe Daniel Chongolo amesema Kinondoni imeshafikia asilimia 70 ya maeneo yake kwa kupulizia dawa ya kuua mazalia ya mbu kwa kutumia vikundi vya jamii vinavyopita mtaani na kubainisha hatua ambazo tayari zimeshakuliwa kuendelea kudhibiti mazalia haya ya mbu ambayo ni uagizaji wa mashine maalum za upuliziaji hewani (Fog machine) ambazo zitawezesha kupuliza dawa eneo kubwa zaidi kwa muda mchache. Aidha Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dkt Festo Dugange katika nafasi yake amewataka wananchi mara waonapo dalili za homa ya dengue kuwahi kituo cha afya ili waweze kupata matibabu stahiki na kuachana na tiba za mtaani kama majani ya mpapai na mafuta ya nazi. Zoezi hilo la upuliziaji viuadudu vya kuua mazalia ya mbu limehudhuriwa pia na Mbunge wa Kinondoni Mh Maulid Mtulia, Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Benjamin Sitta, Mkurugenzi wa Manispaa Ndg Aron Kagurumjuli na wakazi wa Eneo la Mwananyamala. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. RAI YATOLEWA KWA WANANCHI KINONDONI KUSHIRIKI KWA PAMOJA KUANGAMIZA MAZALIA YA MBU, ILI KUWEZA KUJIKINGA NA UGONJWA WA DENGUE Posted On: ... + Read more »
KINONDONI YAUNDA BARAZA LA WAZEE LA WILAYA Posted On: June 21st, 2019 Baraza hilo lenye wajumbe saba akiwemo Mwenyekiti na msaidizi, Katibu na Msaidizi wake, mtunza fedha na wawakilishi wawili, limeundwa kwa uchaguzi uliofanyika kwa wazee wawakilishi kutoka kata 20, za Manispaa hiyo kupiga kura katika kikao kilichofanyika katika moja ya kumbi za Kanisa katoliki Manzese. Akiongoza zoezi hilo, kwa niaba ya Maganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Bi Nusura Kessy amesema, wazee ni hazina ya Taifa, hivyo yapaswa kupaza sauti juu ya maswala yanayowahusu na kuwasemea haki zao za Msingi pale inapobidi ili waweze kutatuliwa. "Wazee ni hazina ya Taifa, nilazima walindwe, waheshimiwe watunzwe, na mashauri yao yasikilizwe, hivyo kwa baraza hili la wazee wa Wilaya mtakaloliunda kwa kufanya uchaguzi huru na wa haki unaozingatia vigezo leo, mtakuwa mmejitendea haki lakini pia baraza hilo likawe kisemeo katika yale yanayowapasa kusema " Bi. Nusura Kessy. Awali akitaja majukumu ya baraza hilo la wazee la Wilaya, Bi. Judith Kimaro ambaye pia ni mkuu wa Kitengo cha ustawi wa jamii amesema Baraza linalo majukumu yake ya msingi ambayo ni kupitia majumuisho ya kero za wazee zilizoletwa na wawakilishi, kufanya mkutano wa baraza la wazee la Wilaya kila baada ya miezi mitatu, kuwasilisha kero za wazee kwenye baraza la madiwani, kuchagua wawakilishi wawili kwenye baraza la madiwani, kushawishi Halmashauri kutenga bajeti kwa ajili ya miradi ya uzalishaji ya wazee pamoja na kuratibu mabaraza ya wazee ya Kata. Naye mratibu wa wazee Manispaa ya Kinondoni Bi Neema Mwalubilo alipokuwa akitoa taarifa ya hali ya wazee Manispaa ya Kinondoni amesema ni ya kiridhisha kwani wameweza kuunganishwa kwenye huduma za afya kwa kutengenezewa vitambulisho takribani 11,340 vya msamaha . Aidha ameainisha mikakati iliyopo ya kuinua hali ya wazee katika Manispaa hiyo kuwa ni kuhakikisha wote wanapata kadi za matibabu, kuwaongezea na kuwajengea uwezo wa kujikwamua kiuchumi pamoja na kuwaunganisha na wadau mbalimbali kwa ajili ya misaada. Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Uhusiano. Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAUNDA BARAZA LA WAZEE LA WILAYA Posted On: June 21st, 2019 Baraza hilo lenye wajumbe saba akiwemo Mwenyekiti na msaidizi, K... + Read more »