WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA MANISPAA YA KINONDONI WATAKIWA KUSIMAMIA SHERIA KATIKA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHIPosted On: June 12th, 2020WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA MANISPAA YA KINONDONI WATAKIWA KUSIMAMIA SHERIA KATIKA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI. Wajumbe wa Mabaraza ya Kata Manispaa ya Kinondoni wametakiwa kusimamia sheria ikiwa ni pamoja na kutoa haki kwa Wananchi kuhusiana na masuala ya migogoro ya Ardhi yanapoletwa kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi. Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo jana alipokutana na wajumbe wa Mabaraza hayo kikao kilichokuwa na lengo la kujadili changamoto mbalimbali zinazo wakabili ambapo pamoja na mambo mengine amewakumbusha kutambua wajibu na majukumu yao.Alisema katika kutambua wajibu wao ni vema wakajiepusha kujihusisha na vitendo vya rushwa kwakuwa vinaweza kuharibu uaminifu waliopewa na Halmashauri pamoja na kusababisha migogoro kwa Wananchi.Katika kikao hicho pia Mhe. Chongolo na wajumbe wa Mabaraza hayo wamejadili hatua zitakazo wawezesha kupunguza kama sio kumaliza kabisa migogoro katika Wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto za wananchi na hivyo kuleta tija na ufanisi wa utendaji wa kazi zao.Aidha amewataka wajumbe hao kuweka utaratibu wa kutembelea maeneo ambayo yanashukiwa kuwa na migogoro na kwamba kwakufanya hivyo itakua ni njia sawia katika kukabiliana na changamoto ambazo wananchi wanakutana nazo. “Mabaraza haya yapokisheria, mnanguvu ya kuwachukulia hatua wale ambao wanakiuka sheria zilizoweka, kukaidi maelekezo mnayotoa, msiwe wanyonge fanyeni kazi kwakusimamia haki na sheria kama ambavyo siku zote Rais wetu Dk. John Pombe Joseph Magufuli anatuelekeza” alisema Mhe. Chongolo. Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo ameipongeza Idara ya sheria ya Manispaa hiyo kwakufanyakazi bega kwa bega na Mabaraza hayo na hivyo kuleta mafanikio makubwa ya utatuzi wa migogoro ya Ardhi. Wajumbe wa Mabaraza ya Kata wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Mhe. Daniel Chongolo. Imeandaliwa na Kitengo Cha habari na MahusianoManispaa ya Kinondoni. WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA MANISPAA YA KINONDONI WATAKIWA KUSIMAMIA SHERIA KATIKA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI Posted On: June 12th, 2020 WAJU... + Read more »
KINONDONI YATEKELEZA MIRADI YA TAKRIBANI BIL. 242.8 KWA KIPINDI CHA MIAKAMITANO YA RAIS DK.MAGUFULIPosted On: June 10th, 2020KINONDONI YAWEKA HISTORIAYATEKELEZA MIRADI YA TAKRIBAN BILIONI 242.8 KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO, ALAT YATOA TUZO. Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeweka historia katika suala la utekelezaji wa miradi ya maendeleo na ile ya kimkakati kwa kipindi cha miaka mitano iliyogharimu takribani shilingi bilioni 242.8 fedha zilizotokana na vyanzo vya mapato ya ndani, Serikali kuu na wadau wengine wa maendeleo.Taarifa hii imetolewa wakati wa uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji wa shughuli za Serikali kwa kipindi cha miaka mitano katika kikao cha mwisho cha Baraza la Madiwani kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa. Akitoa taarifa hiyo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Ndg.Aron Kagurumjuli amesema Kinondoni imefanikiwa kugusa sekta zote muhimu zinazomuhusu kila mwananchi zikiwemo za uchumi, kisiasa, kijamii pamoja na miradi ya Maendeleo na kuitaja kuwa ni ujenzi na ukarabati wa Vyumba vya Madasara, Vyoo kwa shule za msingi na Sekondari, ununuzi wa madawati kwa shule hizo, ujenzi, ukarabati na upanuzi wa Zahanati , Vituo vya Afya na Hospitali, ujenzi wa miradi ya Masoko na uwekezaji.Ametaja maeneo mengine kuwa ni miradi ya barabara kwa kiwango cha lami km. 189 kutoka km. 134, kupitia mradi wa DMDP, TARURA, uendelezaji wa miradi ya kilimo na mifugo, ujenzi wa kiwanda cha kuchakata taka na kuzalisha mbolea mboji, hali ya ukusanyaji wa mapato ya ndani na utoaji wa asilimia 10 ya mikopo ya Wanawake, Vijana na Walemavu.Aidha amefafanua kuwa Halmashauri katika kipindi cha miaka mitano hadi kufikia Juni mwaka huu imetumia kiasi cha shilingi Bil. 3.3 kwa ajili ya kugharamia Elimu ya Msingi bila malipo, Bil. 2.2 Elimu ya Sekondari na hivyo kumpongeza Rais Magufuli kwa kuleta mpango huo.Mbali na fedha hizo, lakini pia Manispaa imefanikiwa kujenga shule nne za Msingi, ujenzi wa vyumba vya madarasa kutoka 983 Oktoba 2015 hadi kufikia 1147, ukarabati wa vyumba 111, matundu ya choo kutoka 686 hadi 1167, ununuzi wa Madawati kutoka 12,962 hadi kufikia 28,705, Maktaba kutoka 13 hadi 22, majengo ya utawala sita pamoja na ofisi za walimu kutoka 49 hadi 62.Kwa upande wa shule za Sekondari Manispaa imefanikiwa “kujenga vyumba vya madarasa 48, katika shule mpya za Mzimuni, Kijitonyama, Magomeni, Mbezi juu, Mivumoni, Shule mpya mbili za Alevel, ukarabati wa vyumba 21, Matundu ya choo kutoka 389 hadi 473, Viti na Meza kutoka 19,353 hadi 25,067, Hosteli moja, Nyumba nne, Walimu maabara kutoka 63 hadi 120, majengo ya utawala saba” ameeleza Kagurumjuli.“ Kwa upande wa Afya tumefanikiwa kujenga Zahanati Nne, vituo vya Afya vitatu ambapo kimoja ni kituo cha Afya Kigogo chenye Ghorofa tano, Hospitali mbili za Ghorofa, upanuzi na ukarabati wa Zahanati sita, Magari ya kubebea wagonjwa matatu, Nyumba za watumishi mbili, Wodi ya Baba, Mama na Mtoto (RCH) 14” ameeleza Kagurumjuli.Kwa upande wa Masoko, amesema “tumekuwa na miradi ya kimkakati na uwekezaji ambayo ni Soko la kisasa la Magomeni, Tandale, vituo vya ukusanyaji wa mapato sita, uwanja wa mpira Mwenge pamoja na Stendi ya daladala ya Mwenge” ameongeza Kagurumjuli.Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tawala na Serikali za Mitaa (ALAT), Bwana Elirehemu Kaaya akitoa salamu ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kufanya kazi nzuri na kusema kuwa ndio Halmashauri pekee Tanzania iliyoweka historia ya utekelezaji wa miradi yake kwa wakati.Amesema kuwa Halmashauri hiyo pia imeweka historia ya kuwa na Mkurugenzi mchapa kazi, mwadilifu, msikivu, na mwenyekusimamia maendeleo iliyopelekea kutunukiwa cheti cha shukrani ikiwa ni katika kutambua mchango wake katika utekelezaji wa miradi kwa wakati .Naye Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Benjamini Sita amesema kuwa Halmashauri hiyo kupitia Mkurugenzi Kagurumjuli imeweka historia Tanzania nzima kwani imefanya mambo makubwa katika kipindi cha uongozi wao na hivyo kumtunuku tuzo ya kutambua mchango wake.Amefafanua kuwa pamoja na mambo mengine wanaondoka wakiwa wameacha alama kubwa ambayo imeacha alama na kusema kuwa iwapo watakuwa na nafasi nyingine ya kurudi watafanya mambo makubwa mengine kwa ajili ya kuwaletea maendeleo Wananchi wa Kinondoni.“Mkurugenzi hongera sana, umefanya mambo makubwa, kwenye uongozi huu tumeshirikiana kama timu, hukujali itikadi za vyama, umewavumilia madiwani wangu, mwisho wa siku umefanya jambo ambalo historia yake tunaiandika leo hii” amesema Mhe. Sita.Mstahiki Meya Benjamini Sitta akimkabidhi Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Aron Kagurumjuli tuzo ya heshima na kutambua mchango wake katika shughuli za utekelezaji wa Serikali katika kipindi cha miaka mitano.Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo akimkabidhi Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Benjamini Sitta tuzo ya heshima ya usimamizi wa utekelezaji wa shughuli za Serikali kwa kipindi cha uongozi wake.Imeandaliwa naKitengo cha Habari na UhusinoManispaa ya Kinondoni KINONDONI YATEKELEZA MIRADI YA TAKRIBANI BIL. 242.8 KWA KIPINDI CHA MIAKAMITANO YA RAIS DK.MAGUFULI Posted On: June 10th, 2020 KINONDONI YAW... + Read more »
KINONDONI YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI MIAKA MITANO MFULULIZOPosted On: June 3rd, 2020Manispaa ya Kinondoni imepongezwa kwa kupata hati safi kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo katika hoja za ukaguzi wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2014/2015 hadi 2018/2019. Pongezi hizo zimetolewa leo na Bi. Mary Assey kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Dar es salaam wakati uchangiaji mada wa taarifa ya hoja za ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2018/ 2019 iliyowasilishwa na mkaguzi wa hesabu za nje Manispaa ya Kinondoni.Amesema Kinondoni imeonesha uzalendo katika usimamiaji mzuri wa rasilimali za Serikali, hasa matumizi mazuri ya Fedha yanayoenda sambamba na thamani halisi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuzitaka Halmashauri nyingine kuiga mfano ya uendeshaji pamoja na usimamizi ili ziweze kuwa na mafanikio makubwa zaidi.“ Ni wapongeze Kinondoni kwakupata hati safi kwa miaka mitano mfufulizo, hii inaonesha ni kwa kiasi gani Mkurugenzi na timu yako mpomakini kwenye utendaji wenu, hasa usimamizi wa matumizi ya fedha kisera ,utekelezaji wa ilani sambamba na usimamizi mzuri wa miradi, tunazo Halmashauri tano katika mkoa wetu wa Dar es Salaam, lakini Kinondoni mnafanya vizuri, hongereni kwa hilo” amesema Bi. Mary.Akitoa taarifa hiyo ya ukaguzi wa hesabu kwa mwaka 2018/ 2019, Mkaguzi Mkuu wa hesabu za nje Manispaa ya Kinondoni Ndg. Eliuther Msombola amesema kuwa ukaguzi huo umefanyika kwa mujibu wa ibara ya 143(2), ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano w Tanzania ya mwaka 1977 (iliyorekebishwa mwaka 2005).Aidha amefafanua kuwa lengo la ukaguzi huo ni kupata uthibitisho wa kuridhia kama taarifa za fedha kwa ujumla wake hazina makosa makubwa yanayotokana na udanganyifu au makosa ya kawaida.Awali akizungumza kwa niaba ya Madiwani,Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Benjamini Sitta amesema kuwa mafanikio ya hati hizo safi zimetokana na usimamizi mahiri wa Mkurugenzi Ndugu. Aron Kagurumjuli pamoja na menejimenti kwani amekuwa mzalendo na kiongozi anayefuata sera na miongozo ya serikali.Imeandaliwa naKitengo cha habari na UhusianoManispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI MIAKA MITANO MFULULIZO Posted On: June 3rd, 2020 Manispaa ya Kinondoni imepongezwa kwa kupata hati... + Read more »
CHONGOLO AAGIZA KUCHUKULIWA HATUA WATAKAOCHIMBA MCHANGA KWENYE MITO. Posted On: April 8th, 2020 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo ameliagiza Jeshi la Polisi Wilayani hapo kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kuingia kwenye mito na kuchimba mchanga katika bonde la mto Salasala, bonde la mto Mbezi na bonde la mto Tegemeta. Mhe. Chongolo ametoa agizo hilo leo wakati alipofanya ziara na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na kushuhudia vitendo hivyo vikiendelea ikiwa ni takribani miezi miwili imepita tangu kuendesha zoezi la upandaji miti ya mianzi na magugu pamoja na kusitishwa kwa vibali vya uchimbaji wa mchanga vilivyotolewa na Bodi ya Maji Bonde la Ruvu. Amesema kuwa licha ya kutoa maelekezo pamoja na kusitishwa kwa vibali hivyo lakini bado wananchi wanaendelea kuchimba mchanga jambo ambalo amesema linahatarisha nyumba za makazi ya watu na hivyo kulisisitizia jeshi hilo kuwachukulia hatua wananchi hao ambao wanajihusisha na shuguli hizo. “Tulishazuia hii mito isichimbwe mchanga, tumepita mto Salasala, Mbezi kule kwenye daraja la Malechela, pamoja na huku juu mpakani mwa eneo la jeshi la Lugalo, bado vitendo hivi vinaendelea nasisitiza naninaagiza jeshi la polisi kwenye Wilaya ya Mabwepande na Kawe ambayo ndio inahusika, niliagiza na leo narudia kwa mara ya pili hatutakuwa na msamaha kwenye jambo hili. Amefafanua kuwa “mtu yeyote ambaye ataonekana analea vitendo vya uharibifu huu wa mazingira, tukimkuta na kumkamata tutamchukulia hatua kali za kisheria kwasababu jukumu letu sisi viongozi ni kusimamia na kuilinda sheria. Mhe. Chongolo amesisitiza kuwa“ Hatuko hapa kuwaonea watu, wala kuwaacha wananchi waharibikiwe na nyumba zao kwasababu ya maslahi na uroho wa watu wachache, kufanya hivi ni kuhujumu maslahi ya nchi hatuwezi kuendelea kuwaacha watu wanamna hii kwa hiyo nilazima tuchukue hatua kwa kila tutakaye mbaini anafanya shughuli hii. Aidha Mhe. Chongolo amesema kuwa baada ya ziara hiyo ataunda timu ya kufuatilia mwenendo wa watu hao kwa kuwa alishatoa maagizo ya kuwashugulikia wote wanaohusika na kufanya shuguli za kuchimba mchanga kwenye mito hiyo. Mapema mwaka huu, Mhe. Chongolo alisitisha vibali vya uchimbaji mchanga vilivyotolewa na Bodi ya Maji Bonde la Ruvu kutokana na kuleta madhara ya uharibifu wa mito na kusababisha athari kwenye makazi ya watu katika Halmashauri hiyo. Vibali vilivyositishwa ni vile vilivyotolewa kufanya shughuli hizo katika Bonde la mto Salasala, Mto mbezi, Ndumbwi, Nyakasangwe, na kusema kuwa mito hiyo inapita katikati ya makazi ya watu na kwamba baada ya kufanyika marekebisho utawekwa utaratibu upya wa kufanya shughuli hizo. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na uhusiano Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. CHONGOLO AAGIZA KUCHUKULIWA HATUA WATAKAOCHIMBA MCHANGA KWENYE MITO. Posted On: April 8th, 2020 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel... + Read more »
DC CHONGOLO APOKEA VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORONA KUTOKA KAMPUNI YA SPORT PESA Posted On: March 30th, 2020 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imepokea vifaa vya kunawia mikono (zaidi ya ndoo 100) pamoja na Vitakasa mikono kutoka mtandao wa kubashiri wa SportPesa kwa lengo la kuwasaidia wananchi kujikinga na maambukizi ya homa ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya COVID 19 (Corona). Vifaa hivyo vya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona vimepokelewa na Mkuu wa Wilaa hiyo Mhe. Daniel Chongolo ,akiwa ameambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Dk. Patricia Henjewele, Mganga Mkuu Samweli Laizre pamoja na Katibu Tawala Bi Stella Msofe. Akizungumza wakati wakupokea vifaa hivyo, Mhe. Chongolo amesema kuwa Kinondoni imepokea vifaa hivvyo na kwamba wataendelea kuhamasisha wadau wengine waweze kuchangia ili kuendelea kudhibiti ugonjwa huo usisambae kwenye maeneo mengine. Amefafanua kuwa Virusi vya Corona vimekuwa janga kubwa Duniani na kwamba Wilaya hiyo imejipanga kuhakikisha kuwa kila mmoja anatumia vitakasa hivyo ili kujikinga na maambukizi ya Virusi hivyo pasipo kuambukiza wengine. “Kama mkuu wa Wilaya ninashukuru kwa msaada huu, kwetu utasaidia kwa sababu ofisi zote za Serikali za mitaa na Kata zitapata seti za vifaa hivi, tutakuwa huru kwa kuendelea kutoa huduma kwa wananchi kama kawaida, ndio mana mmeona hapa kila anaeingia ana nawamikono yake kabla ya kuingia kupatiwa huduma” amesema Mhe. Chongolo. Mhe. Chongolo ameongeza” kwetu sisi hatupambani kama Kinondoni, tunapambana kama mkoa ,nandio jukumu tulilopewa , hivyo hivyo nitumie fursa hii kuwaalika wadau wengine wenye mapenzi mema kutupatia vifaa vingine. Mhe. Chongolo ameeleza kuwa Wilaya hiyo imejipanga vizuri katika kupambana na virusi vya Corona ikiwemo kuendelea kutoa matangazo ya kuhamasisha na kuelimisha wananchi namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo. Kwaupande wake Mkurugenzi wa uendeshaji kampuni ya SportPesa nchini, Abbas Tarimba, amesema kuwa ndoo hizo zakunawia mikono zitasaidia wananchi ikiwa ni hatua ya kujikinga na virusi hivyo vya homa ya mapafu inayosababishwa na Covid 19. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. DC CHONGOLO APOKEA VIFAA VYA KUJIKINGA NA CORONA KUTOKA KAMPUNI YA SPORT PESA Posted On: March 30th, 2020 Halmashauri ya Manispaa ya Ki... + Read more »
DC CHONGOLO AAGIZA WATA ALAMU WA AFYA KUTOA ELIMU YA KUJIKINGA NA CORONA KWA WANANCHI Posted On: March 19th, 2020 NI KATIKA VITUO VYA DALADALA, NYUMBA ZAIBADA Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo, amewaagiza wata alaamu wa Afya Wilayani hapo kuanza mara moja kutoa elimu ya kujikinga na virusi vya Corona kwenye nyumba za Ibada ikiwemo Makanisani na Misikitini. Aidha Mhe. Chongolo ameagiza pia elimu hiyo kutolewa kwenye vituo vya daladala ili kuwasaidia wananchi kutambua namna ya kutumia na kujikinga na Virusi hivyo. Mhe. Chongolo ametoa agizo hilo leo katika kikao cha zarura kilichofanyika katika ukumbi wa Afya ambapo kimehusisha Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Idara ya Afya, watendaji pamoja na viongozi wa Dini . Amesema kuwa lengo la kikao hicho cha zarura ilikuwa ni kujadili namna na hatua zitakazo chukuliwa katika kudhibiti virusi hivyo ili visiweze kusambaa pamoja na kutoa elimu ya kutosha kwa watumishi sambamba wananchi katika Wilaya hiyo. Amesema kutokana na kuingia kwa Virusi hivyo vya Corona katika jiji la Dar es Salaam, wataalamu hao wa Afya wa Wilaya hiyo wanapaswa kutoa elimu madhubuti kwenye maeneo ambayo ni lazima wananchi kuyatumia kama vile Vituo vya daladala ikiwemo vya mwendokasi, nyumba zaibada kuhusu namna ya kujikinga na virusi hivyo. Amefafanua kuwa katika elimu hiyo pia itajikita katika kuelimisha wananchi namna ya kutumia vifaa vya kujikinga na maambukizi hayo kama vile vifaa vya kusafishia mikono, Gloves na Barakoa (Mask ) za kufunika pua na mdomo. “ Hili jambo tunapaswa kulichukulia kwa tahadhari kubwa, muwaelimishe wananchi kuhusu namna ya kujikinga na Virusi hivyo, pamoja na kutumia hivyo vifaa ,mnapopita kwenye hayo maeneo hakikisheni kwamba mnawaelimisha vizuri ili wajue ni wakati gani wanapaswa kuvitumia, pia kusafisha miko mara kwa mara” amesema Mhe. Chongolo. “ Lakini pia tuwasaidie wananchi kutoka kwenye presha waliyo kuwa nayo hivi sasa, tunafahamu kuwa watanzania wengi wamepata taharuki juu ya Vizuri hivi, tusipojitahidi tutajikuta tatizo la presha lina adhiri wananchi kuliko Vizuri vya Corona. Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo amewaeleza viongozi wadini kwamba mikusanyiko isiyokuwa ya lazima haipaswi kuwepo ila kwa ambao wanataka kufunga ndoa wafungishwe lakini kwa kufuata utaratibu ambao utaepusha mikusanyiko ya watu. Awali Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo, John Kijumbe amesema kuwa hadi sasa wameshachukua tahadhari na kama vile kutoa elimu katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwa watumishi na wahudumu wa Afya pamoja na kugawa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo. Hata hivyo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imejidhatiti kikamilifu katika kujikinga na virusi hivyo kwakuweka visafisha mikono kwenye mageti yote ya kuingia ikiwa ni katika kuhakikisha kuwa kila mwananchi anayefika kupata huduma mbalimbali wanakuwa salama. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. DC CHONGOLO AAGIZA WATA ALAMU WA AFYA KUTOA ELIMU YA KUJIKINGA NA CORONA KWA WANANCHI Posted On: March 19th, 2020 NI KATIKA VITUO VYA D... + Read more »
DC CHONGOLO AWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA UGONJWA WA CORONA Posted On: March 17th, 2020 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo amewataka wakazi wa Wilaya hiyo kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa Homa ya Vizuri vya Corona ikiwa ni pamoja na kupokea wageni wasio wajuwa bila kuwa na uhakika wa afya zao. Mhe. Chongolo ametoa kauli hiyo leo wakati alipokuwa kwenye mkutano na wananchi uliokuwa na lengo la kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali hivyo kuwataka kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake sambamba na kuepuka kukaribisha wageni kienyeji. Ameongeza kuwa “ kuanzia leo nyinyi wenyewe muwe walinzi wa wenzenu, chukueni tahadhari, msije kupokea wageni wa aina yoyote ile kwa sababu wapo watu ambao wanaweza kutumia njia mbalimbali za kuleta vizuri hivyo katika maeneo yetu” amesisitiza Mhe. Chongolo. Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo amezindua Bandari Bubu iliyopo Mbweni nakuzitaka Malaka za Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuepusha changamoto kwa wananchi, wafanyabiashara wanaotumia bandari hiyo. Mhe.Chongolo amesema kila mamlaka husika zinapaswa kuwepo katika eneo pamoja na Taasisi nyingine ili kuwezesha wananchi na wafanyabiashara wanaotumia bandari hiyo kufanya shuguli zao kwa urahisi kulingana na mazingira rafiki yaliyopo. Amefafanua kuwa Nchi ilikuwa inakosa mapato mengi kupitia upitishaji wa magendo katika maeneo ya fukwe za Mbeni, Ununio, Kunduchi pamoja na maeneo mengine ya pembezoni mwa fukwe za bahari na hivyo kueleza kuwa tayari bandari hiyo imeruhusiwa kutumika na watu kufanyabishara zao. ”hapo awali tulikuwa hatupati fedha kwenye hii Bandari, ila hivi sasa tumeanza kupata fedha , naomba tushirikiane vizuri na nikiondoka hapa kwenye mkutano , mamlaka zote ambazo zinapaswa kuwepo hapa ziwepo ikiwemo TRA, tunataka mapato wao wasiwe kikwazo cha kutukosesha mapato. Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo amemtaka OCD wa Kawe kuhakikisha kuwa usalama kwa wafanyabiashara unakuwepo sambamba na kuwachukulia hatua wote ambao watakiuka na kushindwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa. Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Uhusiano Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. DC CHONGOLO AWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA UGONJWA WA CORONA Posted On: March 17th, 2020 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe... + Read more »