Top ad

Top ad

KINONDONI YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI MIAKA MITANO MFULULIZO

Posted On: June 3rd, 2020

Manispaa ya Kinondoni imepongezwa kwa kupata hati safi kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo katika  hoja za ukaguzi wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2014/2015 hadi 2018/2019.

 Pongezi hizo zimetolewa leo na Bi. Mary Assey kwa niaba ya  Katibu Tawala Mkoa wa Dar es salaam wakati uchangiaji mada wa taarifa ya hoja za ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2018/ 2019 iliyowasilishwa na mkaguzi wa hesabu za nje  Manispaa ya Kinondoni.

Amesema  Kinondoni imeonesha uzalendo katika usimamiaji mzuri wa rasilimali za Serikali, hasa matumizi mazuri ya Fedha yanayoenda sambamba na thamani halisi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuzitaka  Halmashauri nyingine kuiga mfano ya uendeshaji pamoja na usimamizi ili ziweze kuwa na mafanikio makubwa zaidi.

“ Ni wapongeze Kinondoni kwakupata hati safi kwa miaka mitano mfufulizo, hii inaonesha ni kwa kiasi gani Mkurugenzi na timu yako mpomakini kwenye utendaji wenu, hasa usimamizi wa matumizi ya fedha kisera ,utekelezaji wa ilani sambamba na usimamizi mzuri wa miradi, tunazo Halmashauri tano katika mkoa wetu wa Dar es Salaam, lakini Kinondoni mnafanya vizuri, hongereni kwa hilo” amesema Bi. Mary.

Akitoa taarifa hiyo ya ukaguzi wa hesabu kwa mwaka 2018/ 2019, Mkaguzi Mkuu wa hesabu za nje Manispaa ya Kinondoni Ndg.  Eliuther Msombola amesema kuwa ukaguzi huo umefanyika kwa mujibu wa ibara ya 143(2), ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano w Tanzania ya mwaka 1977 (iliyorekebishwa mwaka 2005).

Aidha amefafanua kuwa lengo la ukaguzi huo ni kupata uthibitisho wa kuridhia kama taarifa za fedha kwa ujumla wake hazina makosa makubwa yanayotokana na udanganyifu au makosa ya kawaida.

Awali akizungumza kwa niaba ya Madiwani,Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Benjamini Sitta amesema kuwa mafanikio ya hati hizo safi zimetokana na usimamizi mahiri wa Mkurugenzi Ndugu. Aron Kagurumjuli pamoja na menejimenti kwani amekuwa mzalendo na kiongozi anayefuata sera na miongozo ya serikali.

Imeandaliwa na

Kitengo cha habari na Uhusiano

Manispaa ya Kinondoni.

0 comments:

Post a Comment

 
Top