PONGEZI ZATOLEWA KATIKA UJENZI WA JENGO JIPYA LA MAMA NA MTOTO MWANANYAMALA Posted On: September 14th, 2019 Pongezi hizo zimetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Daniel Chongolo alipozuru katika hospitali ya Mwananyamala kujiridhisha na hatua za ujenzi wa jengo jipya la mama na mtoto linalojengwa na chuo cha MUST Mbeya lililohusisha uwekaji wa CT-scan na X ray limekamilika kwa kiwango kilichokusudiwa. Amesema kuzuru kwake hapo ni katika kuhakikisha shughuli zinazotekelezwa na Serikali katika nyanja mbalimbali na kugusa wananchi zinakamilika kwa kusudi mahususi hasa ikizingatiwa yeye ndiye mwakilishi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwatumikia wananchi Wilayani kwake. "Hakika ninawapongeza sana kwa ujenzi wa jengo hili lenye kiwango mahususi uliohusisha mtazamo wa mbali ulio chanya katika uwekaji wa vifaa muhimu, haya ndiyo mambo Serikali yetu inayataka, kuwa na ubunifu kama huu wa uwekaji wa CT Scan na X-ray katika ujenzi kwani uhitaji wake ni wa muhimu sana, huo ni uthubutu wa hali ya juu" Ameongeza Mh Chongolo. Naye Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya hiyo Dr. Daniel Nkungu katika mazungumzo yake amemshukuru Mkuu huyo wa Wilaya kwa uzalendo alionao katika ufuatiliaji wa miradi ya Serikali kwani kwa kuzuru kwake katika jengo hilo kunaamsha hamasa si tu ya utendaji kazi, bali umakini katika kuhakikisha miradi ya serikali inakamilika kwa tija iliyokusudiwa. Imeandaliwa na kitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. PONGEZI ZATOLEWA KATIKA UJENZI WA JENGO JIPYA LA MAMA NA MTOTO MWANANYAMALA Posted On: September 14th, 2019 Pongezi hizo zimetolewa leo... + Read more »
KINONDONI KUENDELEZA KIWANJA NA.1024 MWENGE KIHUDUMA NA KIBIASHARA KWA KUJENGA KITUO CHA MABASI Posted On: September 11th, 2019 Hayo yameelezwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Daniel Chongolo alipokutana na wafanyabiashara wa eneo hilo la Mwenge na kuzungumza nao katika kikao kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa Manispaa. Amesema kwa kufanya hivyo ni kwenda sambamba na utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi inayosisitiza suala zima la uboreshaji wa miundombinu katika nyanja mbalimbali ikiwemo huduma za jamii kwa wamachinga na wafanyabiashara katika shughuli zao za kujipatia kipato na kukuza uchumi wao. "Sisi tunamuongozo unaoitwa ilani ya Chama cha Mapinduzi, kwenye ilani hiyo inasema wazi kabisa kwa kipindi cha miaka mitano tunaweka mazingira rafiki kabisa kwa wafanyabiashara yakihusisha maeneo ya biashara, mtaji na uhakika wa eneo hivyo hatuna budi kuhakikisha hilo ambalo lipo ndani ya uwezo wetu linafanikiwa" Amefafanua Chongolo. Aidha amefafanua kuwa uendelezaji huo utahusisha ujenzi wa maduka ya kati ya kibiashara(min- supermarket), sehemu za mamalishe, maduka ya rejareja, maduka ya spea za magari, saluni, vituo vya tax na bajaji, migahawa, vyoo vya jumuiya pamoja na huduma nyingine. Kadhalika amewataka wakazi na wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao katika eneo la kiwanja1024 kuwa sehemu ya uendelezaji huo kwa kutoa ushirikiano pale inapopasa ili kwa pamoja turahisishe maendeleo yenye tija kwa biashara zetu na Taifa kwa ujumla. Alipokuwa akiongea mfanyabiashara mmoja kwa niaba ya wengine ameonesha kuupokea mradi huo na kuahidi kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha unafanikiwa kwa kiwango chenye tija na kilichokusudiwa, na kuiomba serikali iwafikirie pia mara baada ya kukamilika kwake wawe wakwanza kupatiwa maeneo kwa ajili ya kufanyia biashara. Imeandaliwa na Kitengo cha habari na uhusiano Manispaa ya Kinondoni KINONDONI KUENDELEZA KIWANJA NA.1024 MWENGE KIHUDUMA NA KIBIASHARA KWA KUJENGA KITUO CHA MABASI Posted On: September 11th, 2019 Hayo ya... + Read more »
KINONDONI YAPOKEA MSAADA WA SAMANI ZA SHULE KUTOKA KWA INTERNATIONAL SCHOOL OF TANGANYIKA Posted On: September 6th, 2019 Akipokea msaada huo kutoka kwa Mkurugenzi wa IST Dr. Mark Hardeman, Mstahiki Meya Manispaa ya Kinondoni Mhe.Benjamini Sita amesema samani hizi zimekuja wakati ambao Serikali yetu ya awamu ya tano inasisitiza ubora wa miundombinu ya elimu, inayoenda sambamba na ushirikiano wa kielimu baina ya shule na shule kwa lengo la kukuza ujuzi katika kufundisha. Amesema suala la elimu nchini Tanzania limechukua sura ya kipekee hali inayopelekea viongozi kuwa wabunifu katika kuhakikisha wanaendana na sera ya elimu bora na kubainisha kuwa Kinondoni tayari wamejipanga vizuri katika kuhakikisha wanatekeleza upatikanaji wa elimu bora na sio bora elimu. "Katika kuhakikisha tunaendana na kasi ya Mhe. Rais tunatakiwa kuwa wabunifu kila iitwapo leo, leo hii tumepata samani kwa ajili ya shule zetu mbili za Mbweni Teta na Kigogo pamoja na vitabu zaidi ya boksi 44 na tumefanikiwa kupata vifaa hivi kwa kuwa na ushirikiano mzuri na wenzetu wa International School of Tanganyika, hata hivyo tunarajia kupokea vifaa vingi zaidi." Ameongeza Meya. Aidha Msitahiki Meya amesema kuwa upo mfumo mpya ambao anatarajia kuutambulisha hivi karibuni ambao utakuwa chachu ya mafanikio ya elimu kwa Manispaa yake ambacho kitaweza kuinufaisha Nchi kwa ujumla. Naye Dr. Mark Hardeman kutoka International School of Tanganyika amesema kuwa ushirikiano uliopo baina ya Taasisi yake na Manispaa ya Kinondoni ni wa kipekee sana na ameahidi kudumisha na kunufaisha sekta mbalimbali zilizopo na zitakazobuniwa wakati wowote. Kadhalika Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Kinondoni Mwl. Leonard Msigwa kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ameishukuru Taasisi hiyo ya shule kwa kuonesha ushirikiano wenye manufaa zaidi tena kwa mda muafaka . Imeandaliwa na Kitengo Cha Uhusiano na Habari Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAPOKEA MSAADA WA SAMANI ZA SHULE KUTOKA KWA INTERNATIONAL SCHOOL OF TANGANYIKA Posted On: September 6th, 2019 Akipokea msaad... + Read more »
ELIMU YATOLEWA KUHUSIANA NA MABORESHO YA BARABARA -CHINI YA DMDP, KATIKA MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA SHEKILANGO -BAMAGA Posted On: August 24th, 2019 Elimu hiyo imetolewa leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya ofisi ya Afisa mtendaji Sinza ukiwahusisha wananchi wa Sinza A, B, C, D na E ambao ndio walengwa mahususi wa mradi. Katika mkutano huo wa hadhara ilielezwa kuwa Lengo kuu ni kuutambulisha mradi na kutoa elimu na ushauri utakaoweka Mazingira rafiki yatakayowezesha utekelezwaji wake, kwa kuzingatia weledi, ufanisi na ubora uliokusudiwa. Akiambatana na timu ya wasimamizi wa mradi huo, Bi. Pendo Fred, ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Kinondoni amesema, ni vema kuundwa kamati za watu watano kila mtaa kwa lengo la kutoa taarifa stahiki kuhusiana na mradi mzima ikihusisha faida zitakazopatikana wakati na baada ya mradi kukamilika, kwani hiyo ndiyo njia sahihi itakayomwezesha mwananchi yeyote kutoa ushirikiano pale inapobidi, na pia kujua nini wajibu wake na namna ya kutoa taarifa ikiwa kutakuwa na shida yoyote inayoweza kuzalishwa na mradi wakati wa utekelezaji. Kwa upande wake Diwani wa kata ya Sinza Mhe Godfrey Chikandamwali amewashukuru na kuwaahidi wasimamizi wa mradi huo kuendelea kuwaunga mkono kwa kuwa miradi yote ni kwa faida ya wananchi na kusema jukumu walilofuata katika mkutano huo ni jema. Mradi huo utahusisha barabara ya Shekilango mpaka Bamaga awamu ya saba kwa urefu wa km 3.7 kwa usimamizi wa kampuni ya China Road and Bridge Corporation ambao tayari ulishaanza kutekelezwa tangu July 2019, na utakamilika Octoba 2019. Imeandaliwa na Kitngo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. ELIMU YATOLEWA KUHUSIANA NA MABORESHO YA BARABARA -CHINI YA DMDP, KATIKA MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA SHEKILANGO -BAMAGA Posted On: Aug... + Read more »
SERIKALI YAPONGEZA MAONESHO YA NANE NANE KANDA YA MASHARIKI Posted On: August 8th, 2019 NI KUTOKANA NA JUHUDI WANAZOZIFANYA KATIKA KUINUA NA KUKUZA UCHUMI WA NCHI KUPITIA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI. Pongezi hizo zimetolewa leo na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, alipokuwa mgeni rasimi katika kilele cha maadhimisho ya nane nane kanda ya Mashariki yaliyofanyika katika viwanja vya Mwl J K Nyerere Mkoani Morogoro. Amesema ili Uchumi wa nchi ukue, tunategemea viwanda, na malighafi ambazo nyingi tunazipata mashambani, hivyo kwa kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Tanga, Pwani Dar es salaam na Morogoro kwa kauli mbiu isemayo "Kilimo, mifugo na uvuvi kwa ukuaji wa Uchumi wa nchi ", imetekelezeka. "Tunapozungumzia suala la kukuza uchumi wa Nchi kama kauli mbiu yetu inavyoelekeza kwa mwaka huu tunahitaji kuboresha sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi, na hili nimeliona nilipotembelea mabanda mbalimbali hapa, nawapongeza kwa jitihada mnazofanya" amesema Mhe Makamu wa Rais. Pamoja na kuwapongeza viongozi wanaounda ukanda huo, Makamu wa Rais amesisitiza pia juhudi hizo zisiishie kwenye mabanda ya nanenane pekee bali zifikie wananchi wote ambao wanatakiwa kuona mifano halisi kwa viongozi wao wanaowapa mafunzo. Aidha katika maonesho hayo ya 26,Manispaa ya Kinondoni imeshika nafasi ya pili huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na Manispaa ya Ilala. Imeandaliwa na Kitengo cha Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. SERIKALI YAPONGEZA MAONESHO YA NANE NANE KANDA YA MASHARIKI Posted On: August 8th, 2019 NI KUTOKANA NA JUHUDI WANAZOZIFANYA KATIKA KUIN... + Read more »
KUELEKEA KILELE CHA MAAZIMISHO YA SHEREHE ZA MAONESHO YA NANENANE YENYE KAULI MBIU ISEMAYO "KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KWA MAENDELEO YA UKUAJI WA UCHUMI WA NCHI , TEMBELEA BANDA LA KINONDONI UPATE ELIMU KUHUSINA NA UFUGAJI WA NGOMBE NA MBUZI WA MAZIWA NA NYAMA, KUKU WA KIENYEJI NA CHOTARA, UFUGAJI WA SUNGURA NA USHAURI WA UCHIMBAJI WA MABWAWA BORA YA SAMAKI NA KILIMO BORA CHA MBOGAMBOGA NJOO UJIFUNZE KUTOKA KWA WATAALAMU WALIOBOBEA. Banda la manispaa ya Kinondoni ambalo yake kuna mfereji uliotengenezwa kama bwawa dogo kwaajili ya kuonesha ufugaji wa samaki wa kisasa na kuna samaki aina ya kambale wa kutosha watu wanaotembelea kujionea bidhaa mbalimbali katika banda la Kinondoni Shamba la mboga mboga Banda la kuku wa kisasa Shamba la mahindi na mbele yake kuna shamba la zao la mikunde Shamba la migomba Ng"ombe wa maziwa KUELEKEA KILELE CHA MAAZIMISHO YA SHEREHE ZA MAONESHO YA NANENANE YENYE KAULI MBIU ISEMAYO "KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KWA MAENDELEO YA UK... + Read more »
MWENGE WA UHURU MWAKA 2019, WILAYA YA KINONDONI UMEZINDUA, UMEWEKA JIWE LA MSINGI NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO 8 YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI THEMANINI Posted On: July 20th, 2019 Miradi iliyozinduliwa na mwenge wa Uhuru ni pamoja na mradi wa uwezeshaji wananchi kiuchumi wenye gharama ya zaidi ya Milioni 50. Mradi wa ujenzi wa Barabara ya Kilongawima kiwango Cha lami yenye urefu wa km 2 wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 2, Mradi wa Ujenzi wa kituo Cha Afya kigogo wenye thamani ya Zaidi ya Milioni 700. Miradi mingine ni mradi wa Ujenzi wa shule mpya ya Mivumoni uliogharimu Zaidi ya Milioni 200, Mradi wa Ujenzi wa Tanki la maji na miundombinu yake wenye gharama ya Zaidi ya Bilioni 75, Kiwanda cha ushonaji nguo wenye gharama ya kiasi Cha sh Milioni 500 na Ujenzi wa soko la Kijitonyama wenye gharama ya Zaidi ya shillingi Milioni 100. Aidha Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Mzee Mkongea Ally ameipongeza Kinondoni kwa kubuni na kusimamia vizuri miradi hiyo ya maendeleo ambayo itakuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi wa Kinondoni. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. MWENGE WA UHURU MWAKA 2019, WILAYA YA KINONDONI UMEZINDUA, UMEWEKA JIWE LA MSINGI NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO 8 YENYE THAMANI YA ZAIDI Y... + Read more »