Top ad

Top ad










Baraza la Madiwani Manispaa ya Kinondoni chini ya Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mh. Benjamin Sita limepitisha jumla ya Vibali vya ujenzi 168 vyenye thamani ya tsh 36.8Milioni katika kikao chá robo ya tatu kilichofanyika Leo.
Akiwasilisha taarifa ya Kamati ya Mipangomiji na Mazingira mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh. Songoro Mnyonge amesema vibali hivyo vimekamilisha taratibu zote zinazotakiwa na sheria ya Mipangomiji miji Namba 8 ya Mwaka 2007.
Amesema Kamati inalo jukumu kubwa la kusimamia upangaji na uendelezaji wa mji ndani ya Manispaa.
Amezitaja taratibu za kupata vibali hivyo vya ujenzi kuwa ni kwanza mwombaji anatakiwa: kuandaa michoro ya usanifu Majengo, kuandika barua ya Maombi kwa Mkurugenzi, awasilishe michoro yake akiambatisha na nakala ya Hati Miliki pamoja na kujaza fomu maalum ya maombi ya Kibali cha ujenzi.
Pia kwa maeneo ya ghorofa mwombaji atatakiwa kuandaa na kuwasilisha michoro ya vyuma ya jengo kusudiwa.
Vibali vingine vilivyopitishwa na Baraza hilo la Madiwani ni Maombi ya kubadili matumizi ya Ardhi, maombi ya kugawanya viwanja maombi ya kurekibisha michoro pamoja na mawasilisho ya mchoro wa Mipangomiji.
Huu ni mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani Robo ya tatu kwa mwaka 2016/2017 uliofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni leo tarehe 15/06/2017.

0 comments:

Post a Comment

 
Top