KINONDONI YATEKELEZA KAULI MBIU YA SIKU YA WAZEE DUNIANI TAREHE 01/10/2018, KWA VITENDO Posted On: October 1st, 2018 Manispaa ya kinondoni katika kuadhimisha siku ya wazee duniani yenye kauli mbiu isemyao"Wazee ni hazina ya Taifa, tuenzi juhudi za kutetea haki na ustawi wao", imegawa vitambulisho takribani 900 vya matibabu kwa wazee, pamoja na kutoa huduma za vipimo vya afya kwa magonjwa yasiyoambukiza kwa wazee wasiopungua 600, zoezi lililofanyika katika viwanja vya Mwinjuma CCM. Akigawa vitambulisho hivyo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Katibu Tawala ya Wilaya hiyo Bi.Stella Msofe amesema, Serikali inajivunia kuwa na wazee kwani ndiko hazina kubwa ya busara na mafunzo katika kutekeleza majukumu ya Serikali inapatikana. "Wazee ni hazina kubwa na sisi kama Serikali tunajivunia kuwa nanyi, hivyo jukumu letu kubwa ni kuhakikisha mnatimiziwa haki yenu ya msingi ambayo ni huduma za afya zilizo bora bila usumbufu" Amesema Katibu tawala. Akitoa taarifa ya huduma kwa wazee katika Manispaa ya Kinondoni kwenye maadhimisho hayo, Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo, Dr.Festo Dugange amesema Manispaa ya Kinondoni imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza Sera ya wazee ya Wizara ya Afya kwa kuboresha huduma za afya kwa wazee,ikiwemo utoaji wa vitambulisho vya matibabu. Ameongeza kuwa kwa kutambua umuhimu wa siku ya wazee, na kutekeleza kauli mbiu ya mwaka huu, huduma mbalimbali zimetolewa katika maadhimisho hayo ambazo ni kujiandikisha na kutoa vitambulisho vya wazee, kupima uzito na urefu, kusoma BMI, vipimo vya maabara, kupima malaria na kupima macho. Huduma nyingine ni kupima tezi dume kwa kutumia damu, ushauri wa VVU, ushauri kuhusu maambukizi ya TB/Ukoma, na ushauri kuhusu lishe. Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Mwinjuma CCM, pia yalienda sambamba na burudani pamoja na michezo ya kufukuza kuku kwa wazee wanawake na wanaume, kuvuta kamba pamoja na burudani ya miziki ya zamani. Imeandaliwa na Kitengo cha habari na Uhusiano. Manispaa ya kinondoni. KINONDONI YATEKELEZA KAULI MBIU YA SIKU YA WAZEE DUNIANI TAREHE 01/10/2018, KWA VITENDO Posted On: October 1st, 2018 Manispaa ya kinond... + Read more »
KINONDONI YAADHIMISHA SIKU YA KICHAA CHA MBWA DUNIANI KWA KUTOA CHANJO KWA MBWA NA PAKA 1150 KATI YA 1588, WALIOTAMBULIWA. Posted On: September 28th, 2018 Manispaa ya Kinondoni leo imeadhimisha siku ya kichaa cha Mbwa duniani, yenye kauli mbiu isemayo "Sambaza ujumbe, okoa maisha" kwa kutoa chanjo kwa mbwa na paka 1150, zoezi lililofanyika katika Mtaa wa Madale, Kata ya Wazo iliyopo Manispaa hiyo. Akizungumnzia maadhimisho hayo ambayo huadhimishwa duniani tarehe 29/08 ya kila mwaka, kwa niaba ya Afisa Mifugo wa Manispaa ya Kinondoni, Dr. Ntanga amesema, Kinondoni imemudu kudhibiti kwa kiasi kikubwa ugonjwa wa kichaa cha mbwa, kwani chanjo iliyokwishatolewa tangu mwezi wa saba mwaka huu, hadi sasa ni asilimia 70. "Viko viwango vya Afya kutoka shirika la Afya duniani vinavyosadikiwa kwamba, chanjo ya ugonjwa ikifanyika kwa asilimia 70, inakuwa imemudu kwa kiasi kikubwa zuio la ugonjwa husika. Kwa sisi Kinondoni tangu mwezi wa saba mwaka huu, hadi sasa tumefanikiwa kutoa chanjo kwa mbwa na Paka 1150 kati ya 1588 waliotambuliwa" Amebainisha Dr.Ntanga. Aidha Dr Ntanga pia ametahadharisha athari zinazopatikana kwa kung'atwa na mbwa mwenye kichaa kuwa ni kupelekea kifo endapo matibabu yatacheleweshwa, na kuwataka wananchi wakazi wa Kinondoni kuhakikisha wanazingatia sheria ndogo za ufugaji mijini kwa kuhakikisha wanawapeleka mbwa wao na paka kwenye chanjo. Maadhimisho hayo yameenda sambamba na uoneshaji wa sinema kwa wanafunzi inayotoa elimu na uelewa wa namna thabiti ya kujikinga na athari za kichaa cha mbwa. Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAADHIMISHA SIKU YA KICHAA CHA MBWA DUNIANI KWA KUTOA CHANJO KWA MBWA NA PAKA 1150 KATI YA 1588, WALIOTAMBULIWA. Posted On: Sep... + Read more »
KINONDONI YASOGEZA HUDUMA KWA WANANCHI, KWA KUFUNGUA VITUO VYA KUKUSANYA MAPATO KATIKA KATA TANO. Posted On: September 19th, 2018 Hayo yamebainishwa na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mh Benjamini Sitta, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika mahojiano yaliyofanyika mara baada ya kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa. Amesema lengo la ufunguzi wa vituo hivyo ni kutekeleza mpango mkakati wa kuongeza mapato, unaoenda sambamba na ukusanyaji wake, ikihusisha ulipaji wa tozo mbalimbali katika Halmashauri, lakini pia ni katika kuwajali wananchi kwa kuwasogezea huduma hiyo kwa ukaribu zaidi kutakakorahisisha ulipaji wa tozo na kodi mbalimbali ambapo hapo awali iliwalazimu kufuata huduma hiyo katika ofisi za Halmashauri. "leo tulikuwa na kikao cha kawaida cha baraza la madiwani, na katika kikao hicho, yamejadiliwa mambo mengi yakiwemo mpango mkakati wa kukabiliana na changamoto ya ukusanyaji mapato, ila kama Halmashauri tumekuja na mkakati thabiti wa kukabiliana na swala hilo kwa kufungua vituo vya kimapato katika Kata tano za Halmashauri yetu." Amefafanua Meya Sitta. Aidha amezitaja Kata na vituo hivyo kuwa ni Bunju, Tegeta-Kibo Complex, Mwenge, Msasani na Mikocheni,na kuanisha huduma zitakazopatikana kuwa ni ukataji na ulipaji wa leseni za vileo, Ada za kupima afya, ada za TFDA, na ada za SUMATRA kwa vyombo vya usafiri kama vile pikipiki, na Bajaji. Aidha katika kikao hicho cha Baraza kilichojumuisha wakuu wa idara na vitengo, Wah. Madiwani, Tarura,TAKUKURU, na Jeshi la Polisi, kimejadili ajenda kuu tatu ambazo ni taarifa za utekelezaji wa Kamati mbalimbali za kudumu robo ya nne, taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, pamoja na kuthibitisha taarifa za kamati mbalimbali za kudumu. Katika hatua nyingine Meya Sitta amewataka wananchi wa Manispaa ya kinondoni kuvitumia vituo vilivyofunguliwa katika Kata na maeneo wanakoishi kwa ajili ya kulipia tozo mbalimbali kwani ndio njia rahisi ya kuepukana na mlolongo wa foleni wakati wa kupatiwa huduma hizo. Aidha kikao hicho kimeenda sambamba na kuapishwa kwa Mbunge wa jimbo la Kinondoni Mhe. Abdallah Mtulia, aliyeshinda uchaguzi mara baada ya kufanyika uchaguzi wa marudio katika jimbo hilo. Imeandaliwa na Kitengo cha Uhusiano na Habari. Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YASOGEZA HUDUMA KWA WANANCHI, KWA KUFUNGUA VITUO VYA KUKUSANYA MAPATO KATIKA KATA TANO. Posted On: September 19th, 2018 Hayo ... + Read more »
WITO WATOLEWA KWA WANANCHI WAISHIO NA WATU WENYE ULEMAVU WILAYA YA KINONDONI Posted On: September 12th, 2018 KUHAKIKISHA WANASHIRIKIANA NA NIDA WILAYANI HAPO, KUWASAJILI KATIKA DAFTARI LA TAIFA NA KUWATAMBUA KWA LENGO LA KUPATIWA VITAMBULISHO VYA TAIFA. Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Daniel Chongolo, alipokuwa mgeni rasmi kwenye zoezi la usajili na utambuzi wa watu wenye ulemavu kwenye daftari la Taifa, lililofanywa na NIDA, kwa kushirikiana na SHIVYAWATA, pamoja na Ofisi ya Ustawi wa Jamii Manispaa ya Kinondoni, kwa lengo la kupatiwa vitambulisho vya Taifa. Amesema zoezi hili ni zuri, kwani kwa kufanya hivi ni kutekeleza haki ya msingi kikatiba na pia ni kutoa fursa ya watu wenye ulemavu kusajiliwa na kupatiwa vitambulisho vya Taifa, na kuwataka wananchi wanaoishi nao majumbani, kuhakikisha wanawaleta kwa ajili ya zoezi hilo la siku tatu la utambuzi na uandikishaji linaloendelea katika shule ya Ndugumbi Manispaa ya Kinondoni. "Wito wangu kwa wanakinondoni, wito wangu kwa wale wanaoishi na watu wenye ulemavu, naomba sana ndani ya siku tatu hizi, muwashawishi, wawalete, wawape fursa watu wenye ulemavu kutumia haki yao ya msingi waliyopewa ya kujisajili kwenye daftari la Taifa, kwa ajili ya kupata vitambulisho vya Taifa".Amesisitiza Chongolo. Awali akitoa taarifa ya zoezi hilo, Afisa Msajili wa NIDA Wilaya ya Kinondoni Ndg. Dickson Mmbaga amesema, kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi Kinondoni kupitia zoezi hili tumetambua, tumesajili, tumeweka mazingira wezeshi na kupata takwimu zitakazosaidia kuboresha maendeleo ya watu wenye ulemavu, ikiwa ni pamoja na kupatiwa vitambulisho vya Taifa vitakavyowasaidia katika shughuli zao mbalimbali. Aidha amezitaja faida za kupatiwa vitambulisho vya Taifa kuwa ni kurahisisha upatikanaji wa huduma zote za msingi, kumtambulisha mtu mwenye ulemavu anapohitaji huduma, kumuwezesha kujidhamini kama anahitajika kufanya hivyo, kurahisisha zoezi la kuhesabu watu, pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama wa watu wenye ulemavu. Naye Mwenyekiti wa SHIVYAWATA Wilaya ya Kinondoni, Bi.Subira Semsimbazi alipokuwa akitoa salaam za shukrani kwa Mkuu huyo wa Wilaya, ameainisha changamoto zinazowakabili kuwa ni ukosefu wa ofisi, ukosefu wa wakalimani, kutopatiwa huduma za bima afya, na pia kutopatiwa mikopo ya wanawake na vijana ili waweze kujishughulisha na shughuli za ujasiriamali. Zoezi hili la utambuzi na usajili wa watu wenye ulemavu kwenye daftari la Taifa, kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa linafanyika kwa siku tatu katika shule ya msingi Ndugumbi iliyoko Manispaa ya Kinondoni. Imeandaliwa na Kitengo cha Uhusiano na Habari. Manispaa ya Kinondoni. WITO WATOLEWA KWA WANANCHI WAISHIO NA WATU WENYE ULEMAVU WILAYA YA KINONDONI Posted On: September 12th, 2018 KUHAKIKISHA WANASHIRIKIANA... + Read more »
ZOEZI LA UTOAJI WA ELIMU SAHIHI NA HUDUMA YA UZAZI WA MPANGO KWA JAMII LAENDESHWA MANISPAA YA KINONDONI Posted On: September 7th, 2018 NI KWA KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA JHPIEGO KUPITIA MRADI WA "TUPANGE PAMOJA" LENYE OFISI ZAKE MIKOCHENI. Zoezi hilo lililoendeshwa kwa siku tatu kwa kushirikiana na shirika la JHPIEGO limehusisha utoaji wa Elimu sahihi ya uzazi wa mpango, huduma ya uzazi wa Mpango kwa njia za muda mfupi ,na muda mrefu na za kudumu, sambamba na huduma hizo pia zimejumuisha upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi, maambukizi ya vvu, pamoja na shinikizo la damu, kwa Kata tano Kati ya Kata ishirini(20), za Manispaa hiyo. Akifafanua malengo ya zoezi hilo Mratibu wa huduma za Afya ya uzazi, na Mtoto wa Manispaa ya Kinondoni Bi.Edith Manase Mboga amesema lengo ni kuhakikisha elimu sahihi juu ya maswala ya uzazi wa mpango inawafikia wananchi bila kupotoshwa, ikienda sambamba na ongezeko la matumizi sahihi ya njia za uzazi wa mpango Ameongeza kuwa kwa kushirikiana na shirika la JHPIEGO chini ya mradi wa "TUPANGE PAMOJA" wamehakikisha Elimu sahihi, huduma ya uzazi wa Mpango,ushauri na upimaji wa magonjwa hayo inatolewa bure kwa wananchi. Katika zoezi hilo lililohusisha Kata ya Hananasif, Magomeni, Tandale, Kunduchi na Mwananyamala, mratibu huyo amewataka wananchi kuwa na utaratibu wa kutumia njia za uzazi wa mpango, kupima afya zao mara kwa mara ili kuweza kutambua muenendo wa mwili Kiafya na kuchukua hatua stahiki pindi inapohitajika. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. ZOEZI LA UTOAJI WA ELIMU SAHIHI NA HUDUMA YA UZAZI WA MPANGO KWA JAMII LAENDESHWA MANISPAA YA KINONDONI Posted On: September 7th, 2018 ... + Read more »
KINONDONI YAKABIDHIWA KISIMA CHA MAJI CHENYE THAMANI YA TSH MILIONI KUMI NA NNE ZA KITANZANIA Posted On: August 31st, 2018 Kisima hicho kilichojengwa kwa ufadhili wa Asasi ya Kiraia ya TIME TO HELP, chenye ukubwa wa mita 104, kimekabidhiwa leo kwa Shule ya Sekondari Boko na Shule ya msingi Boko National Housing zilizopo Kata ya Bunju, Mtaa wa Dovya Manispaa ya Kinondoni. Akipokea kisima hicho kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Katibu tawala wa Wilaya hiyo, Bi.Stella Msofe amesema, ujenzi wa kisima hicho ni kielelezo tosha cha Asasi ya Kiraia ya Time to help kinachoonesha dhamira ya dhati ya kuunga mkono jitihada za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini Rais Dr.John Pombe Joseph Magufuli, ya kuboresha miundombinu ya elimu na maji Mashuleni. "Tunaishukuru sana TIME TO HELP, mlichokifanya mmerudisha nuru kwenye nyuso zilizofubaa, mmedhihirisha uzalendo mlionao kwa Taifa hili, lakini pia mmerudisha uhai kwa wanafunzi hawa kwa kutujengea kisima cha ukubwa wa mita 104, kitakachoziwezesha shule hizi mbili kupata maji."Amesema Katibu Tawala. Aidha Bi.Msofe amewataka waalimu na wanafunzi wa shule hizo mbili kuhakikisha wanakitunza, wanakilinda, na kukithamini kisima hicho kwa matumizi yaliyokusudiwa. Akisoma taarifa ya shule kwa mgeni rasmi, Mkuu wa Shule ya Sekondari Boko Bi Rosalia Chelesi amesema, Shule inajumla ya wanafunzi 1,015, kati yake wavulana ni 510, na wasichana ni 240, na kwa upande wa Shule ya Msingi Boko National Housing idadi ya wanafunzi ni 498, ambapo wavulana ni 258, na wasichana ni 240. Bi.Chelesi pia ameainisha changamoto zilizopo shuleni hapo kuwa ni ubovu wa madarasa, upungufu wa madawati, ukosefu wa uzio, upungufu wa matundu ya vyoo, uharibifu wa barabara hasa kipindi cha mvua, upungufu wa nyumba za waalimu, pamoja na ukosefu wa umeme kwa shule ya Msingi Boko National Housing. Imeandaliwa na Kitengo cha Uhusiano na habari. Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAKABIDHIWA KISIMA CHA MAJI CHENYE THAMANI YA TSH MILIONI KUMI NA NNE ZA KITANZANIA Posted On: August 31st, 2018 Kisima hicho... + Read more »
"TENGENEZENI MPANGO WA UWASILISHAJI MADA ZA AFYA ZINAZOISHI, KWENYE KILA MKUTANO WA WANANCHI UNAOFANYIKA Posted On: August 29th, 2018 Ni agizo lake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Daniel Chongolo, alipokuwa akitoa maelekezo, katika kikao kazi cha Kamati ya Afya ya Msingi ya Wilaya, kilichofanyika leo kwa lengo la kupokea taarifa za utekelezaji wa shughuli za Afya, ikiwemo utekelezaji wa kampeni ya ugawaji dawa kinga na tiba kwa magonjwa ya kichocho na Minyoo ya tumbo kwa wanafunzi wa shule za awali na msingi. Amesema mada zinazoishi kuhusiana na masuala ya magonjwa ya jumla yanayoweza kuzuilika, ni kitu ambacho mwananchi anatakiwa kukumbushwa mara kwa mara kupitia watendaji ngazi ya Kata na Mitaa kwani asilimia kubwa yanatokana na uchafu na mazalia ya mbu. "Nitoe Rai idara ya Afya, tusisubiri dharura kwenye kushughulikia magonjwa ya mlipuko, katika vikao vyenu, ngazi za Kata,Mikutano ya wananchi, tengenezeni mpango wa uwasilishaji mada zinazoishi, mada inayoishi katika magonjwa ya jumla kama kipindupindu, kichocho, kwani haya msingi wake ni uchafu" Amebainisha Mh.Chongolo. Awali akimkaribisha Mkuu wa Wilaya, Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo Dr. Festo Dugange amesema, Manispaa ya Kinondoni inavyo vituo 187, vya kutolea huduma za Afya vikihusisha hospitali, zahanati, kliniki, na martenity home ambavyo, kati yake 27 ni vya Serikali, na 160, ni vya binafsi, taasisi za Serikali, na Mashirika ya kidini tunavyoshirikiana navyo katika kuboresha utoaji huduma za Afya, ikiwa ni pamoja na kushughulikia changamoto zinazojitokeza, na kuweka mikakati ya maboresho katika sekta hiyo. Akitoa taarifa ya kampeni ya ugawaji wa dawa kinga na tiba kwa magonjwa ya kichocho na minyoo ya tumbo kwa wanafunzi wa shule za awali na Msingi, mratibu wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dr. Neema Mlole amesema, Kinondoni imelenga kufikia wanafunzi 121,086 , wenye umri kuanzia miaka 5 hadi 14, walioandikishwa katika shule za awali na Msingi, 157, zilizopo ndani ya Kata 20 za Manispaa ya Kinondoni. Ameongeza kuwa, katika kampeni hii, kwa kushirikiana na Wizara ya Afya maendeleo ya jamii, jinsia ,wazee na watoto kupitia kitengo cha Mpango wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele imeshachukua hatua stahiki kuelekea kwenye utekelezaji ikiwemo kutoa elimu kwa wazazi na walezi, kutoa elimu kwa wagawa kinga tiba hizo watakaoshiriki zoezi, kusambaza dawa na vifaa maalumu, pamoj na mpango wa kuandaa chakula kwa wanafunzi kabla ya kuwapa kinga tiba hizo. Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya, kwenye kikao hicho kilichohusisha Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya, wawakilishi wa mashirika ya dini, pamoja na wajumbe wa kamati, ameitaka idara ya Afya kuhakikisha inashughulikia maduka ya dawa muhimu, pamoja na hospitali bubu zinazoendeshwa bila vibali wala utaratibu, ili kujiepusha na madhara ya kiafya yanayoweza kutokea kwa watumiaji. Imeandaliwa na Kitengo cha Uhusiano na Habari. Manispaa ya Kinondoni. "TENGENEZENI MPANGO WA UWASILISHAJI MADA ZA AFYA ZINAZOISHI, KWENYE KILA MKUTANO WA WANANCHI UNAOFANYIKA Posted On: August 29th,... + Read more »