Top ad

Top ad

ZOEZI LA UTOAJI WA ELIMU SAHIHI NA HUDUMA YA UZAZI WA MPANGO KWA JAMII LAENDESHWA MANISPAA YA KINONDONI

Posted On: September 7th, 2018
NI KWA KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA JHPIEGO KUPITIA MRADI WA "TUPANGE PAMOJA" LENYE OFISI ZAKE MIKOCHENI.
Zoezi hilo lililoendeshwa kwa siku tatu kwa kushirikiana na shirika la JHPIEGO limehusisha  utoaji wa Elimu sahihi ya uzazi wa mpango, huduma ya uzazi wa Mpango kwa njia za muda mfupi ,na muda mrefu na za kudumu, sambamba na huduma hizo pia zimejumuisha upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi, maambukizi ya vvu, pamoja na shinikizo la damu, kwa Kata tano Kati ya Kata ishirini(20), za Manispaa hiyo.
Akifafanua malengo ya zoezi hilo Mratibu wa huduma za Afya ya uzazi, na Mtoto wa  Manispaa ya Kinondoni Bi.Edith Manase Mboga amesema lengo ni kuhakikisha elimu sahihi juu ya maswala ya uzazi wa mpango inawafikia wananchi bila kupotoshwa, ikienda sambamba na ongezeko la matumizi sahihi ya njia za uzazi wa mpango
Ameongeza kuwa  kwa kushirikiana na shirika la JHPIEGO chini ya mradi wa "TUPANGE PAMOJA" wamehakikisha Elimu sahihi, huduma ya uzazi wa Mpango,ushauri na upimaji wa magonjwa hayo inatolewa bure kwa wananchi.
Katika zoezi hilo lililohusisha Kata ya Hananasif, Magomeni, Tandale, Kunduchi na Mwananyamala, mratibu huyo amewataka wananchi kuwa na utaratibu wa kutumia njia za uzazi wa mpango, kupima afya zao mara kwa mara ili kuweza kutambua muenendo wa mwili Kiafya na kuchukua hatua stahiki pindi inapohitajika.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.

0 comments:

Post a Comment

 
Top