KILIMO TARI-MIKOCHENI WASHIRIKIANA KATIKA KUFANYA UTAFITI WA KILIMO
CHA MBOGA MBOGA
"Kila kitu huenda kwa hatua, Hapa walipofikia Malolo na Manispaa ya Kindoni ni mwendelezo mzuri wa kufikia malengo waliyojiwekea katika kufanya kilimo bora cha Mijini nasi pia kushirikiana nao kwa kila hatua." Dr Bira.
Aidha Afisa kilimo wa Manispaa ya Kinondoni Ndugu Salehe Hija amesema kuwa utafiti huu ni mwendelezo wa mikakati iliyowekwa na kituo cha Malolo ya kuhakikisha kinawanufaisha Wananchi na Wakazi wa Kinondoni kwa ujumla.
Aina 22 ya mboga mboga za mchicha zimefanyiwa utafiti. Wakulima kutoka Manispaa ya Kinondoni na Ubungo wamehudhuria katika zoezi hilo ambapo awali wamesikiliza semina fupi iliyowasilishwa na Dr Minja katika kuweka bayana nini hasa lengo la utafiti huo, zoezi hilo pia limehusisha uoanjaji wa aina mbalimbali za mchicha ili kubaini upi una ladha nzuri.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari
na Uhsiano Manispaa ya Kinondoni.
0 comments:
Post a Comment