Top ad

Top ad

MWILI WA ALIYEKUWA DIWANI WA KATA YA MAGOMENI MH.JULIAN RUSHAIGO BUJUGO UMEAGWA LEO

Posted On: October 23rd, 2018
Mwili wa aliyekuwa diwani wa Kata ya Magomeni kwa kipindi cha miaka kumi na nne(14), Mh.Juliani Rushaigo Bujugo umeagwa leo katika viwanja vya Manispaa ya Kinondoni.
Akiongoza shughuli hiyo iliyohudhuriwa pia na viongozi wa vyama na Serkali,  Mstahiki Meya wa Manispaa ya kinondoni  Mh.Benjamini Sitta amesema,  Kinondoni imepoteza mpiganaji, mpenda haki, mtetezi wa wanyonge,  lakini pia mzalendo.
"Bujugo alikuwa mzalendo, alikuwa ni mtu aliyependa kuona mambo yanakwenda, wanyonge wanapata haki, hata siku ambayo usiku wake mauti inamkuta, Mh Bujugo alikuja ofisini kwangu mchana kwa swala la walemavu wa magomeni kuhusiana na ada ya usajili wa kikundi wanayotozwa" Amezungumnza Meya Sitta.
Shughuli hii ya kuuaga mwili wa marehemu Julian Rushaigo Bujugo imehudhuriwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Ndg Aron Kagurumjuli, wakuu wa idara na vitengo, wananchi wa kata ya Magomeni, pamoja na viongozi wa vyama na serikali, akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bi.Kate Kamba, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Ndg. Harold Maruma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Paul Makonda, pamoja na Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kinondoni.
Bwana ametoa, bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi Amen.

Imeandaliwa na,
Kitengo cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.

0 comments:

Post a Comment

 
Top