Top ad

Top ad

Wakuu wa shule za Msingi na Sekondari Manispaa ya Kinondoni wametakiwa kuhakikisha wanaondoa vibanda vya biashara vilivyopo ndani ya maeneo ya shule.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ali Hapi alipotembelea shule ya Msingi Mikocheni leo na kukuta vibanda vya biashara shuleni hapo.
Amesema kuwepo kwa vibanda hivyo kunasababisha mazingira ya shule kutokuwa rafiki kwa mwanafunzi kujisomea na pia kuwaondolea umakini katika masomo yao
.
Ziarani hapo Mkuu wa Wilaya amefanikiwa kukagua maktaba ya kujifunzia, kisima cha maji yanayotumiwa na wanafunzi, ujenzi wa choo kipya, uchakavu wa choo cha zamani, pamoja na uhaba wa madawati.
Amewataka waalimu kuwa waadilifu kwenye kazi yao kwani ndio nguzo na msingi wa Maisha kwa vijana wa Taifa la leo ambalo ndilo nguvu kazi ya Taifa.

0 comments:

Post a Comment

 
Top