Watendaji wa Kata, Mitaa pamoja na Maafisa Afya wametakiwa kuhakikisha wanasimamia na kuviondoa vibanda vyote vya kuonesha video kwenye mitaa yao pamoja na kutoruhusu uuzaji na unywaji wa pombe masaa ya kazi.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi alipokuwa katika ziara yake ya kutembelea Kata ya Mikocheni na kujionea Jiographia ya kata, Miradi ya maendeleo, utekelezaji wa Ilani pamoja na changamoto zinazowakabili.
Hapi amesema kuwepo kwa vibanda vya kuonesha video kwenye Mitaa kunachangia mmomonyoko mkubwa wa maadili kwa vijana wetu na kupelekea hata kufeli masomo yao kutokana na utoro mashuleni na pia kutumia muda mwingi kuhadithiana wanachokiangalia na sio kusoma.
Amesema ni vema watendaji wa Kata wakaacha kufanya kazi kwa mazoea na kuhahakikisha wanawatumikia wananchi.
Amewataka Watendaji wa Kata kuhakikisha wanatenga siku ya kusikiliza kero za wananchi, kuwa wabunifu katika utendaji wao, kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kuhakikisha kila mgeni anayehamia kutoka kata au mtaa awe na utambulisho maalumu
.
Naye Mtendaji wa Kata ya Mikocheni Ndg Sylvester Ntonja akisoma taarifa yake kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, ameainisha changamoto zinazoikabili Kata ya Mikocheni kuwa ni Maswala ya Ulinzi na usalama, upungufu wa madawati kwa shule za Msingi, ukosefu wa maabara kwa shule za Sekondari, kutokuwepo na Zahanati ya Kata, umbali wa dampo kwa ajili ya kutupa taka, na wakandarasi wengi kutokuwa na uwezo wa kuondoa takataka kwa wakati.

Mkuu wa Wilaya amefanikiwa kutembelea Shule ya Msingi na Sekondari ya Mikocheni, Soko la Mikocheni, Barabara ya Chwako, na kuongea na wananchi wa Mikocheni A katika mkutano wa hadhara.
Hii ni kata ya NNE kutembelea kati ya Kata ISHIRINI za Manispaa ya Kinondoni katika ziara yake ya kujionea changamoto na utekelezaji wa Miradi pamoja na Ilani, ikiwa alianza kata ya Tandale, Kigogo na Mabwepande.
0 comments:
Post a Comment