MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA BANDA LA KINONDONI, MAONESHO YA NANENANE KANDA YA MASHARIKI, MKOANI MOROGOROPosted On: August 6th, 2020Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Bi. Mwanana Msumi, akipata maelezo kutoka kwa Maafisa wa Kitengo cha Uchaguzi Manispaa ya Kinondoni alipotembelea Banda hilo kwa lengo la kujionea maonesho hayo.Mtaalamu wa kutengeneza mfumo wa kisasa wa ufugaji wa Samaki Bwana. Jonas Ndau akitoa maelezo kwa Wananchi waliofika kuona mfumo huo unavyofanya kazi.Afisa Kilimo wa zao la mboga mboga kutoka Manispaa ya Kinondoni, Bwana. Emanuel Chacha akitoa maelezo ya Kilimo hicho kwa kutumia udongo kwa Wananchi waliofika katika Banda la Maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro.Muonekano wa zao la Nyanya lililolimwa kwa kutumia mfumo wa eneo la wazi. Mtaalamu wa ufugaji wa Samaki kwa kutumia njia ya Bwawa la maji kutoka Manispaa ya Kinondoni, bwana Masumbuko Nzingula akitoa maelezo kwa Wananchi waliofika katika Banda la Manispaa hiyo katika Viwanja vya Maonyesho ya Nanenane mkoani Morogoro. Mjasiriamali wa Samaki na Dagaa kutoka Manispaa ya Kinondoni, Bi. Mwajuma Mwinyimbe akitoa maelezo kwa Wananchi waliofika katika banda la Manispaa hiyo viwanja vya maonesho ya Wakulima Nanenane yanayoendelea Mkoani Morgoro.Imeandaliwa naKitengo cha Habari na Mahusiano MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA BANDA LA KINONDONI, MAONESHO YA NANENANE KANDA YA MASHARIKI, MKOANI MOROGORO Posted On: August 6th, 2020 K... + Read more »
MATUKIO KATIKA PICHA BANDA LA KINONDONI MAONESHO YA NANENAE ,VIWANJA VYA TUNGI, MKOANI MOROGOROPosted On: August 4th, 2020Mfumo wa kuzungusha maji kwa ajili ya ufugaji wa Samaki kwa njia ya kisasa unaojulikana kwa jina la Recirculating Aquaculture System (RAS).Mzee ambaye ni mkazi wa Morogoro, akipata maelezo kutoka kwa Maafisa wa Kitengo cha uchaguzi Manispaa ya Kinondoni kuhusu masuala ya uchaguzi alipofika kwenye Banda la Manispaa hiyo katika maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro.Wananchi waliofika katika Banda la Manispaa ya Kinondoni katika kikundi cha Vijana wajasiriamali ambao ni wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Manispaa hiyo wakiangalia bidhaa za viatu vya ngozi katika maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro.Afisa mifugo wa Kampuni ya Ronheana kutoka Manispaa ya Kinondoni akitoa maelezo kwa Maafisa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi walipopita kutembelea Banda la Manispaa hiyo katika maonesho ya wakulima nanenane yanayoendelea mkoaani Morogoro.Mkurugenzi mwendeshaji wa Kampuni ya Wasambazaji wa Teknolojia ya Jividudu hai (E.M) kutoka Manispaa ya Kinondoni Bi. Gigwa Swai akitoa maelezo kwa mtaaalmu kutoka Manispaa ya Temeke katika Banda la Manispaa ya hiyo katika maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro.Kikundi Cha wajasiriamali wakinamama kutoka Manispaa ya Temeke waliovaa Tishet za kijivu wakibadilishana ujuzi kutoka Kikundi cha wakina Mama wajasiriamali wa Manispaa ya Kinondoni katika maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro.. Maafisa mifugo Bi. Grace Misonge na Bi Ancila Malamshakutoka Halmashauri ya Chalinze wakipata maelezo kuhusiana na masuala ya Kilimo kwa ujumla.Imeandaliwa naKitengo cha Habari na UhusianoManispaa ya Kinondoni. MATUKIO KATIKA PICHA BANDA LA KINONDONI MAONESHO YA NANENAE ,VIWANJA VYA TUNGI, MKOANI MOROGORO Posted On: August 4th, 2020 Mfumo wa kuzun... + Read more »
PROFESA KABUDI AIPONGEZA KINONDONI MAONESHO YA WAKULIMA NANENANEPosted On: August 1st, 2020Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Profesa Paramagamba Kabudi ametembelea Banda la Kinondoni katika maonesho ya wakulima ya nanenane Mkoani Morogoro nakuipongeza kwakuwa na vitu ambavyo vinavutia watazamaji.Profesa Kabudi amesema katika Banda hilo amevutiwa na Teknolojia ya kilimo Cha mjini na Vijijini ikiwemo kilimo Cha kisasa cha mbogamboga na mazao ya chakula sambamba na ufugaji wa kisasaAmeongeza kuwa kupitia maonesho hayo wananchi wa Dar es Salaam wanakila sababu ya kujifunza teknolojia hizo kutoka Manispaa ya Kinondoni kwakuwa itawawezesha kuendesha shuguli zao za kilimo Cha mijini.Amesema katika Banda hilo pia amevutiwa na wajasiriamli wakina Mama wanaotengeneza bidhaa za nguo kwa kutumia Teknolojia ya kisasa ambao inaongeza thamani ya bidhaa hiyo na hivyo kumpongeza Mkurugenzi Aron Kagurumjuli kwa kuwawezesha wajasiriamali hao." Mkurugenzi nakupongeza wewe pamoja na timu nzima ya Kinondoni, mmefanya kazi kubwa kwenye maonesho hayo, mmewaletea Wananchi mambo mazuri ambapo wanapokuja kuangalia wanaondoka na ujuzi mzuri katika nyanja zote ikiwemo kilimo, ufugaji, usindikikaji wa vyakula na utengenezaji wa bidhaa za nguo za batiki.Aidha ameipongeza Manispaa hiyo kwa kuwawezesha vijana wajasiriamali katika utengenezaji wa bidhaa za ngozi ikiwemo viatu nakusema kuwa mpango huo ni mzuri kwani unaendana sambamba na kauli mbiu ya Serikali ya Viwanda ya Rais Dk. John Pombe Magufuli.Ameongeza kuwa Rais Magufuli anaguswa na vijana ambao wanatumia ujuzi wao kwa ajili ya kuijenga nchi na kwamba Manispaa imeonambali katika kuwawezesha kwenye ufanisi huo ambao unatija kwa Taifa.Imeandaliwa naKitengo Cha Habari na UhusianoManispaa ya Kinondoni. PROFESA KABUDI AIPONGEZA KINONDONI MAONESHO YA WAKULIMA NANENANE Posted On: August 1st, 2020 Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Kima... + Read more »
KINONDONI YAZINDUA MFUMO WA KUTUMIA SIMU MPANGUSO KUPATA USHAURI WA LISHE (BETTER YOUR HEALTH) KWA WATUMIAJI WA DAWA ZA KUFUBAZA MAKALI YA VIRUSI VYA UKIMWIPosted On: July 29th, 2020Akizindua mfumo huo wa kutumia simu mapanguso( smartphone) better your health kupata ushauri wa lishe na taarifa za hali ya afya na kwa watumiaji wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI (vvu) kwa kushirikiana na wadau kutoka Fabstech, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dr. Samweli lizer kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo amesema ni mfumo mzuri utakaosaidia kutoa taarifa za msingi katika kuhakikisha mtumiaji anazipata ili kuboresha afya yake.Amesema ni fursa pekee itakayosaidia kundi hili maalumu kula mlo kamili kwa kufuata utaratibu hali itakayosaidia kupungua kwa maambukizi katika jamii.Akiutambulisha mfumo huo Dr.Linda Mlunde kutoka kampuni ya teknolojia inayojishughulisha na utengenezaji wa mifumo ( Fabstech ltd).amesema ni mfumo rafiki wa kutumia simu kwa watumiaji wa dawa za kufubaza makali ya VVU ili kupata ushauri wa lishe na taarifa za afya zitakazowasaidia kuimarisha afya zao.Ameongeza kuwa mtumiaji wa mfumo huu atatakiwa kuwa na simu mpanguso ( smartphone) ili aweze kujisajili na ili mtumishi aweze kutumia mfumo atafuata maelezo na kuingiza taarifa zake kwenye mfumo ambazo ni uzito, urefu, muda na kiasi cha chakula alichokula kwa siku baada ya kuingiza taarifa hizo kwenye mfumo mtumiaji atapata mrejesho kuhusu afya yake ya mwili na ushauri wa lishe kutokana na Hali yake ya afya aliyonayo.Akieleza jinsi ya kujiunga na mfumo huo wa Better yourHealth Ndg Karimu Iddi kutoka kampuni ya Fabstech ameeleza namna ya kupata mfumo huo katika simu yako kwa kufuata hatua ambazo ni kufungua Playstore-na kupakua app ya chrome, pili Update App ya Chrome, tatu kufungua App ya Chrome na kuandika maneno, betteryouth.co.tz, nne kubonyeza kitufe Cha Go, tano kufuata maelekezo ili kuruhusu mfumo wa better your helath katika simu yako, kujisajili na kuanza kutumia mfumo wa better YH.Naye Bi.Gisela Mallya ambaye ni mtumiaji wa mfumo wa better your health amesema ni mfumo rafiki na mzuri kwani unasaidia kupata ushauri wa lishe na taarifa stahiki zinazomuwezesha kujua uwiano Kati ya urefu na uzito wake na suala zima la lishe hali uliyonayo ikiwa ni pamoja na aina yachakula unachotakiwa kula, kiasi cha chakula na wakati gani unaoenda sambamba na nini kifanyike pindi unapohitajika kufanya hivyo.Uzinduzi wa mfumo huo uliodhaminiwa na PEPFAR, MCC, na WFP, na kusimamiwa na Tanzania data lab, mehudhuriwa na wajumbe kutoka Tanzania Data lab (dLab), CHMT, watoa huduma wa afya kutoka vituo vya afya, watoa huduma kutoka ngazi ya jamii, Wateja ambao ndio watumiaji wa mfumo na timu iliyotengeneza mfumo wa better your health kutoka kampuni ya Fabstech limited.Imeandaliwa naKitengo Cha Habari na UhusianoManispaa ya Kinondoni KINONDONI YAZINDUA MFUMO WA KUTUMIA SIMU MPANGUSO KUPATA USHAURI WA LISHE (BETTER YOUR HEALTH) KWA WATUMIAJI WA DAWA ZA KUFUBAZA MAKALI YA... + Read more »
KINONDONI YAPOKEA VIFAA VYA KUWAKINGA WANAFUNZI DHIDI YA MAAMBUKIZI YA VIRUS VYA CORONAPosted On: July 9th, 2020Vifaa hivyo vimepokelewa toka shirika la kulinda watoto la save the children kwa lengo la kuhakikisha wanafunzi wanakuwa salama kwa wakati huu ambao wamerudi shuleni kuendelea na masomo yao.Akiongea wakati wa kupokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispa, Mganga Mkuu wa manispa Dkt Samwel Laiza amelishukuru shirika la save the children kwa kuwezesha kupatikana kwa vifaa hivyo kwani vifaa vilivyopo sasa havitoshelezi mahitaji halisi ya wanafunzi."Tunawashukuru Ndugu zetu hawa sababu wameona Kuna umuhimu wa kuwakinga watoto wetu kwani corona Bado ipo japo imepungua Sana, lakini Kama jamii Bado inatakiwa kuchukua tahadhari zinazoshauriwa na wataalamu wetu"Amesema Dkt LaizaAmeongeza pia kinondoni Ina mkakati wa kufanya zoezi la unawaji mikono kuwa endelevu hata baada ya kuisha kwa mlipuko wa ugonjwa wa corona kwani tafiti zinaonesha kwa kunawa mikono kunapunguza asilimia 60 ya magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya mfumo wa chakula.Akiongea wakati wa kukabidhi vifaa hivyo meneja wa uchechemuzi na kampeni wa shirika la save the children Bi Nuria Mshare amesema kuwa wao kama shirika Wana wajibu wa kuhakikisha watoto wanakuwa salama , hivyo wameguswa kuhakikisha watoto wa Shule wanakuwa salama wakiwa shuleni kwa kuwapatia vifaa vitakavyowawezesha kutakasa mikono Yao wakati wote watakaokuwa wanaendelea na masomo.Amesema shirika liko begakwabega na serikali kuhakikisha mapambano dhidi ya virusi vya corona kwa wanafunzi yanafanikwa na wanafunzi wanaendelea na masomo Yao bila ya kuwa na usumbufu wowote.Naye mwalimu mkuu wa Shule ya secondari ya Kigogo Mwl Ester Idabu amesema awali walikuwa na changamoto ya vifaa vya kunawia ambapo walikua wanatumia ndoo za kawaida hali iliyowalazimu kujaza maji kila baada ya muda fulani lakini kwasasa baada ya kupata matanki hayo makubwa yatapunguza isumbufu huo.Afisa elimu Msingi anaeshughulika na masuala ya afyaeza wanafunzi Bi Martha Kusaga amesema vifaa hivyo vitagawiwa kwa shule kumi ambazo ni kisauke ( Msingi na sekondari), Sekondari za Kigogo, mikocheni, Kawe na Bunju pamoja na shule za Msingi za Changanyikeni, Salasala, Mbezi Ndumbwi pamoja na makongo juu.Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na Matanki ya maji 20, Sabuni za kunawia mikono 500, Taulo za kike 1000 na Nguo za ndani 500.Imeandaliwa naKitengo Cha habari na UhusianoManispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAPOKEA VIFAA VYA KUWAKINGA WANAFUNZI DHIDI YA MAAMBUKIZI YA VIRUS VYA CORONA Posted On: July 9th, 2020 Vifaa hivyo vimepokelewa t... + Read more »
RC MAKONDA: KINONDONI NI MFANO WA KUIGWA KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO.Posted On: June 29th, 2020Halmashauri za Mkoa wa Dar es salaam zimetakiwa kuiga mfano wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kutumia vyanzo vya mapato ya ndani, Serikali kuu pamoja na wadau kama ilivyotekelezwa katika Manispaa ya Kinondoni.Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili kwa jimbo la Kinondoni na Kawe yenye lengo la kukabidhi miradi kwa kamati ya siasa ya Mkoa.Amesema kuwa kila Halmashauri katika Mkoa wa Dar es Salaam inakusanya mapato hivyo zinapaswa kutekeleza miradi ambayo itaaacha alama kama ambavyo Manispaa ya Kinondoni imeweka alama katika miradi mikubwa ya Maendeleo chini ya Serikali ya awamu ya Tano ya Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli pamoja na usimamizi mzuri wa Mkurugenzi mzalendo Ndg. Aron Kagurumjuli."Kinondoni nawapongeza sana, mmefanya kazi inayoonekana nakuacha alama kwa Wananchi, kipindi cha nyuma haya mambo hayakuwepo licha ya kwamba Manispaa zilikuwa zinakusanya mapato lakini katika uongozi wa miaka mitano ya Dk. Magufuli mmeitendea haki ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), " amesema Makonda.Akizungumzia mradi wa Soko la kisasa la Magomeni, Mhe. Makonda amesema soko hilo lililojengwa kwa fedha kutoka Serikali kuu, ni chanzo kikubwa cha mapato katika Manispaa ya Kinondoni litakaloongeza hadhi ya wafanyabishara watakaoendesha shuguli zao bila kubugudhiwa.Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mhe. Chongolo amesema kuwa katika Wilaya hiyo Mkurugenzi pamoja na timu yake wamefanikiwa kukamilisha miradi kwa wakati na kwamba wanapoikabidhi kwa kamati hiyo inatoa fursa kuendelea kutekeleza miradi mingine.Katika Ziara hiyo Mhe. Makonda ametembelea miradi mbalimbali ambayo ni ujenzi wa Hospital ya Wilaya iliyopo Mabwepande, Kiwanda Cha kuchakata taka, Shule ya wasichana Mabwe Tumaini na Zahanati ya Bunju.Miradi mingine ni ujenzi wa matanki ya Maji , ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Shekilango hadi Bamaga, Soko la Kisasa Magomeni, Kituo Cha Afya kigogo, Zahanati ya Mikoroshini ,Uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu Mwenge pamoja na Stedi ya daladala iliyopo Mwenge.Imeandaliwa na,Kitengo Cha Habari na MahusianoManispaa ya Kinondoni. RC MAKONDA: KINONDONI NI MFANO WA KUIGWA KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO. Posted On: June 29th, 2020 Halmashauri za Mkoa wa Dar es sa... + Read more »
KINONDONI YAPONGEZWA KWA KUJENGA UWANJA WA MPIRA WA KISASA, TIMU KUBWA ZATAKIWA KUIGA MFANO.Posted On: June 25th, 2020Manispaa ya Kinondoni imepongezwa kwa ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu wenye uwezo wa kuchukua takriban idadi ya mashabiki 3600 kwa mara moja.Pongezi hizo zimetolewa na Naibu wa Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Josephat Kandege wakati wa ziara yake katika Halmashauri hiyo kushuhudia uwanja huo wa kisasa ukijengwa katika eneo la Mwenge kwa mapato ya ndani utakaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 2.2 hadi kukamilika kwake.Amesema kuwa mradi huo utakapokamilika utawezesha timu ya mpira ya Manispaa hiyo (KMC FC) kupata faida kubwa na hivyo kujiendesha yenyewe kupitia mapato yatakayokusanywa katika uwanja,na kuzitaka timu kubwa ambazo hadi sasa hazina viwanja kuiga mfano huo.“Niwapongeze sana Kinondoni, kwakujenga uwanja huu, utakapomalizika najua faida yake ipo wazi kabisa, kwanza inapendezesha, lakini pia inaleta changamoto kwa Halmashauri nyingine na timu kubwa kuiga kwenu, kama timu ya Kinondoni inaweza kuwa na uwanja wa kisasa wao wanashindwa nini” amesema Mhe. Kandege.Hata hivyo Mhe. Kandege ameipongeza timu ya KMC FC kwakuendelea kufanya vizuri katika michezo yake na kusema kuwa kwa mwenendo huo hivi sasa inanafasi kubwa ya kushiriki ligi kuu katika msimu ujao.Imeandaliwa nakitengo cha Habari na MahusianoHalmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAPONGEZWA KWA KUJENGA UWANJA WA MPIRA WA KISASA, TIMU KUBWA ZATAKIWA KUIGA MFANO. Posted On: June 25th, 2020 Manispaa ya Kinondon... + Read more »