Top ad

Top ad

 

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA BANDA LA KINONDONI, MAONESHO YA NANENANE KANDA YA MASHARIKI, MKOANI MOROGORO

Posted On: August 6th, 2020

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Bi. Mwanana Msumi, akipata maelezo kutoka kwa Maafisa wa Kitengo cha Uchaguzi Manispaa ya Kinondoni alipotembelea Banda hilo kwa lengo la kujionea maonesho hayo.

Mtaalamu wa kutengeneza mfumo wa kisasa wa ufugaji wa Samaki Bwana. Jonas Ndau akitoa maelezo kwa Wananchi waliofika kuona mfumo huo unavyofanya kazi.

Afisa Kilimo wa zao la mboga mboga kutoka  Manispaa ya Kinondoni, Bwana. Emanuel Chacha akitoa maelezo ya Kilimo hicho kwa kutumia udongo kwa Wananchi waliofika katika Banda la Maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro.

Muonekano wa zao la Nyanya lililolimwa kwa kutumia mfumo wa eneo la wazi.

 

Mtaalamu wa ufugaji wa Samaki kwa kutumia njia ya Bwawa la maji kutoka Manispaa ya Kinondoni, bwana Masumbuko Nzingula akitoa maelezo kwa Wananchi waliofika katika Banda la Manispaa hiyo katika Viwanja vya Maonyesho ya Nanenane mkoani Morogoro.

 

Mjasiriamali wa Samaki na Dagaa kutoka Manispaa ya Kinondoni, Bi. Mwajuma Mwinyimbe akitoa maelezo kwa Wananchi waliofika katika banda la Manispaa hiyo viwanja vya maonesho ya Wakulima Nanenane yanayoendelea Mkoani Morgoro.


Imeandaliwa na

Kitengo cha Habari na Mahusiano

0 comments:

Post a Comment

 
Top