Top ad

Top ad

 

MATUKIO KATIKA PICHA BANDA LA KINONDONI MAONESHO YA NANENAE ,VIWANJA VYA TUNGI, MKOANI MOROGORO

Posted On: August 4th, 2020


Mfumo wa kuzungusha maji kwa ajili ya ufugaji wa Samaki kwa njia ya kisasa unaojulikana kwa jina la Recirculating Aquaculture System (RAS).

Mzee ambaye ni mkazi wa Morogoro, akipata maelezo  kutoka kwa Maafisa wa Kitengo cha uchaguzi Manispaa ya Kinondoni kuhusu masuala ya uchaguzi alipofika kwenye Banda la Manispaa hiyo  katika maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro.

Wananchi waliofika katika Banda la Manispaa ya Kinondoni katika kikundi cha Vijana  wajasiriamali ambao ni wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Manispaa hiyo wakiangalia  bidhaa za viatu vya ngozi katika maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea  mkoani Morogoro.

Afisa mifugo wa Kampuni ya Ronheana kutoka Manispaa ya Kinondoni akitoa maelezo kwa Maafisa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi walipopita kutembelea Banda la Manispaa hiyo katika maonesho ya wakulima nanenane yanayoendelea mkoaani Morogoro.

Mkurugenzi mwendeshaji wa Kampuni ya Wasambazaji wa Teknolojia ya Jividudu hai (E.M) kutoka Manispaa ya Kinondoni Bi. Gigwa Swai akitoa maelezo kwa mtaaalmu kutoka Manispaa ya Temeke katika Banda la Manispaa ya hiyo katika maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro.

Kikundi Cha wajasiriamali wakinamama kutoka Manispaa ya Temeke waliovaa Tishet za kijivu wakibadilishana ujuzi kutoka Kikundi cha wakina Mama wajasiriamali wa Manispaa ya Kinondoni katika maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro.

. Maafisa mifugo  Bi. Grace Misonge na Bi Ancila Malamshakutoka Halmashauri ya Chalinze wakipata maelezo kuhusiana na masuala ya Kilimo kwa ujumla.


Imeandaliwa na

Kitengo cha Habari na Uhusiano

Manispaa ya Kinondoni.

0 comments:

Post a Comment

 
Top