KINONDONI YAINGIA MKATABA NA KAMPUNI MBILI UJENZI WA BARABARA, BILIONI 34.2 KUTUMIKA. Posted On: March 10th, 2020 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni leo imesaini mkataba na Kampuni mbili za China kwa ajili ya ujenzi wa mradi mkubwa wa barabara zenye urefu wa kilomita 12 ambapo jumla ya kiasi cha Tsh. Bil. 34.2 zitatumika kwenye mradi huo. Kampuni ambazo Manispaa ya Kinondoni imeingia mkataba wa ujenzi huo mara baada ya kutangazwa tenda ni Stecol Corporation pamoja na China Ralway Seventh Group Limited. Mkataba huo umesainiwa na Mstahiki Meya Mhe. Benjamini Sitta, na kushuhudiwa na Kaimu Mkurugenzi Dk. Patricia Henjewele pamoja na Kaimu Mhandisi wa Manispaa Mkelewe Tungaraza. Akizungumza mara baada ya hafla ya utiwaji wa saini wa mkataba wa mradi huo, Meya Sitta amefafanua kuwa ujenzi huo utahusisha barabara ya Magomeni mapipa hadi urafiki ambayo inaurefu wa zaidi ya kilomita saba (7), Makumbusho, Mwanamboka, na barabara ya Muhimbili ambazo zinaurefu wa zaidi ya kilomita tano (5). Aidha Meya Sitta ameeleza kuwa ujenzi wa barabara ya Magomeni Mapipa na Urafiki inajengwa na Kampuni ya Stecol Corporation kwa gharama ya Tsh. Bil. 18.7 huku barabara ya Makumbusho, Mwanamboka na Muhimbili ikijengwa na Kampuni ya China Ralway Seventh Group Limited kwa gaharama ya Tsh. Bil.15.5. Mhe. Sitta amemshukuru Mkurugenzi Aron Kagurumjuli kwa kuhakikisha barabara hizo zinajengwa na kwamba maendeleo ambayo yanafanyika katika Manispaa hiyo yanatokana na juhudi kubwa ya utendaji kazi wake. “ Nampongeza Mkurugenzi wetu, anafanya kazi kubwa leo hii tunakwenda kuleta maendeleo makubwa ya barabara katika Manispaa yetu, hivyo mradi huu utakuwa sehemu ya kutatua changamoto zilizopo katika Halmashauri yetu” amesema Meya Sitta. “ Leo ni siku ya kihistoria katika Manispaa yetu, tumesaini mikataba mikubwa miwili kutoka kampuni mbili tofauti , mikataba hii nisehemu kubwa ya mradi wa DMDP, ambao unakwenda kutatua changamoto ya barabara kwenye Halmashauri yetu , hivyo ninampongeza sana Mkurugenzi wetu Kagurumjuli” amesema Meya Sitta. Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa DMDP ambaye pia ni Kaimu Mhandisi wa Manispaa, Mkelewe Tungaraza amesema kuwa mradi huo utaanza Aprili mwaka huu na unatarajiwa kukamilika kwa muda wa miezi 15. Imeandaliwa na Kitengo Cha habari na Mahusiano Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAINGIA MKATABA NA KAMPUNI MBILI UJENZI WA BARABARA, BILIONI 34.2 KUTUMIKA. Posted On: March 10th, 2020 Halmashauri ya Manisp... + Read more »
KINONDONI YA ADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI Posted On: March 9th, 2020 Shehere ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yamefanyika leo katika viwanja vya Lidas ambapo kimkoa mwenyeji na muandaaji wa ma adhimisho hayo ni Wilaya ya Kinondoni. Katika ma adhimisho hayo, mgeni rasmi ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Poul Makonda ambapo alisindikizwa na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Daniel Chongo, Katibu Tawala Bi. Stella Msofe , Kaimu Mkurugenzi Dk. Patricia Henjewele, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii pamoja na watumishi wanawake wa Halmashauri hiyo. Aidha Mhe. Makonda aliambatana na wageni wengine ambao ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Dk. Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sarah Msafiri na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Bi. Sipora Liana. Madhimisho hayo yalibeba ujumbe ulioeleza kuwa KIZAZI CHA USAWA KWA MAENDELEO YA TANZANIA YA SASA NA YA BAADAE. Imeandaliwa na kitengo cha Habari na Uhusiano Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni KINONDONI YA ADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI Posted On: March 9th, 2020 Shehere ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yamefan... + Read more »
KINONDONI YAPONGEZWA KUONGOZA MARA NNE MFULULIZO KIMKOA Posted On: February 24th, 2020 NI KATIKA KUFANYA VIZURI KWENYE MATOKEO YA KIDATO CHA NNE CHA PILI Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ,imepongezwa kwa kufanya vizuri katika matokeo ya kidato Cha nne na cha pili kwa miaka minne mfululizo kwa mkoa wa Dar es Salaam. Pongezi hizo zimetolewa na Afisa Elimu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwana Hamis Lissu wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa walimu na shule zilizofanya vizuri kwa matokeo hayo kitaifa na kimkoa kwa mwaka 2019 ,2020. Lissu amesema kuwa Halmashauri hiyo imekuwa ikifanya vizuri na kwa ufanisi mkubwa kwa kila eneo ikiwemo Elimu, Afya na mazingira, Michezo na maeneo mengine na kusema kuwa mafanikio hayo yanatokana na kuwa na Mkurugenzi mwenye juhudi za kufanya kazi inayoendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano inayo ongozwa na Dk. John Pombe Magufuli. Lissi amefafanua kuwa Mkoa wa Dar es Salaam unajumla ya Halmashauri tano lakini Halmashauri ya Kinondoni inayo ongozwa na Mkurugenzi wake Aron Kagurumjuli imekuwa ikifanya vizuri katika sekta ya elimu ambapo imeongoza kuwa na matokeo mazuri kwa miaka minne mfululizo katika mkoa huo. " Kinondoni imekuwa ikifanya vizuri sana kwenye mambo mengi, binafsi mnanikosha na utendaji wenu uliotukuka ,niwasihi nguvu hii mliyokuwa nayo muendelee nayo ili kuendelea kuwa na rekodi nzuri kwa kuwa mfano bora kwa Halmashauri nyingine zilizopo katika mkoa wetu" amesema Bwana Lissu. Lakini pongezi hizi pia zimuendee zaidi Mkurugenzi Kagurumjuli, Kinondoni mmepata Mkurugenzi bora, anafanya vizuri sana kwenye Halmashauri yake,na uchapakazi huu ndio anaoutaka Mhe. Rais wetu Dk. Magufuli, tukiwa na wachakazi kama hawa, hakika kwenye mkoa wetu tutakuwa na matokeo makubwa zaidi kwenye kila eneo” ameongeza Bwana Lissu. Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari, wa Halmashauri hiyo, Bwana Leornad Msigwa amesema katika matokeo ya kidato cha nne Kinondoni ilishika nafasi ya 39 kati ya Halmashauri 195 na hivyo kufanya kupanda nafasi tatu kitaifa ukilinganisha na mwaka 2018 ambapo ilishika nafasi ya 42 na kuendelea kuongoza kwa kishindo kwa miaka mine mfufulizo katika mkoa wa Dar es Salaam. Msigwa ameongeza kuwa tathmini ya matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2019 inaonyesha kuwa ufaulu umeongezeka kwa silimia 0.59 ukilinganisha na mwaka 2018 ambapo ufaulu umekuwa kwa asilimia 81.21 ambapo mwaka 2019 ufaulu ulikuwa kwa asilimia 81.80. Kwa upande wa matokeo ya kidato cha pili , Msigwa ameeleza kuwa tathmini ya upimaji wa matokeo ya kidato cha pili kwa mwaka 2019 , ufaulu ulikuwa kwa silimia 94.04 na hivyo kufanya Halmashauri ya Kinondoni kushika nafasi ya 24 kitaifa kati ya Halmashauri 184 na hivyo kupanda nafasi 10 kitaifa ukilinganisha na mwaka 2018. Msigwa amefafanua kuwa, katika matokeo hayo mwaka 2019 watahiniwa walikuwa 9,340 ambapo waliofaulu mtihani huo kati ya daraja 1-1V walikuwa 8,783 sawa na asilimia 94.04. Amefafanua kuwa kati yao waliopata alama za ufaulu wa daraja la kwanza ni 1,682, daraja la piIi ni 1,216, daraja la tatu 1,556, daraja la nne 4,329 huku jumla ya watahiniwa 557 walipata alama ya sifuri. Katika hatua nyingine Msigwa amewaeleza walimu wa shule za Sekondari waliokuwa katika hafla hiyo kuendelea kujituma zaidi kwa kutumia mbinu mbalimbali za ufundishaji ili kuwezesha Halmashauri hiyo kuendelea kufanya vizuri zaidi kitaifa na kimkoa. Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Uhusiano Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAPONGEZWA KUONGOZA MARA NNE MFULULIZO KIMKOA Posted On: February 24th, 2020 NI KATIKA KUFANYA VIZURI KWENYE MATOKEO YA KIDAT... + Read more »
KINONDONI YA TUMIA BIL. 1.5 UJENZI WA MADARASA YA SHULE ZA MSINGI Posted On: February 4th, 2020 WALIMU WASEMA MKURUGENZI KAGURUMJULI ANATEKELEZA IPASAVYO SERA YA ELIMU BILA MALIPO. Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imetumia kiasi cha shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi na ukaratabati wa vyumba 107 vya madarasa pamoja na matundu ya choo 157 kwa wanafunzi wa shule za msingi zilizopo katika Halmashauri hiyo. Hayo yamebainisha na Afisa elimu msingi wa Halmashauri hiyo Kiduma Mageni wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya shule iliyokuwa na lengo la kuona maendeleo ya miradi hiyo ambayo inatekelezwa kwa kutumia Force Account. Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa ziara hiyo, Ndugu Mageni amesema kuwa katika fedha hizo zilizotumika kujenga na kukarabati vyumba hivyo vya madarasa pamoja na matundu ya choo, shilingi milioni 771, 520,000 zinatokana na makusanyo ya ndani, shilingi milioni 455,140,000 ni pesa kutoka serikali kuu kupitia mpango wa EP4R. Aidha Mageni ameongeza kuwa katika fedha hizo pia kiasi cha shilingi milioni 210, 004, 726 ni pesa kutoka mpango wa madarasa 100 ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Daniel Chongolo, na kiasi cha shilingi milioni 4, 140,000 nipesa zinazotokana na nguvu za wananchi. Sambamba na hivyo, ndugu Mageni amebainisha madarasa yaliyojengwa ni 58, yaliyokarabatiwa ni 42 na kwamba kwa vyumba vilivyokarabatiwa vimeanza kutumika na wanafunzi huku vile vinavyojengwa vikiwa vimekamilika kwa asilimia 95. Mageni amesema Halmashauri ya Kinondoni kupitia Mkurugenzi Aron Kagurumjuli pamoja na Mkuu wa Wilaya Mhe. Daniel Chongolo wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa inajenga na kukarabati madarasa hayo ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira mazuri. Ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya tano inayo ongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli inatoa elimu bure na kwamba viongozi hao Mkurugenzi Kagurumjuli na Mkuuwa Wilaya Chongolo wanaitekeleza kikamilifu sera hiyo. “ Niwapongeze sana kwa kazi nzuri wanayoifanya, tumejionea wenyewe wanafunzi wanakaa kwenye majengo mazuri,ya kisasa ,mengine bado yapo kwenye hatua ya mwisho kukamilika na muda sio mrefu yatakabidhiwa ili watoto wetu wa anze kuyatumia. “Nampongeza sana Mhe. Chongolo, Kagurumjuli na timu yake yote wanafanya kazi kubwa, inaonekana, Rais wetu Dk. Magufuli ametoa elimu bure na sisi tunaitekeleza, nasio kwamba tunaishia hapa, bado tutaendelea kutekeleza zaidi na zaidi ili watoto wetu wasome kwenye majengo safi” amesema Mageni. Mageni amesema ameridhishwa na ujenzi, ukarabati wa majengo hayo na hivyo kuwataka walimu hao kuwa wasimamizi wazuri wa miundombinu hiyo. Kwa upande wa mwalimu hao waliokuwa katika ziara hiyo wamempongeza Mkurugenzi Kagurumli kwa kuwezesha ujenzi wa madarasa hayo na kwamba wanafunzi watasoma kwa nafasi. Mmoja wa walimu hao ambaye ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mwenge, Janeth Mlenge alisema kuwa elimu bure inayotolewa na Rais Dk.Magufuli imetoa hamasa kwa wazazi na hivyo kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma. Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Nyakasanga amesema kuwa kupitia mradi huo katika shule yake amejengewa vyumba nane vya madarasa ofisi ya mwalimu mkuu pamoja na matundu 13 ya choo na hivyo kumpongeza Mkurugenzi Kagurumjuli,Mhe. Chongolo kwa kuwapatia majengo hayo. Hata hivyo walimu hao wameonyesha kufurahishwa na huduma hiyo ya kujengewa madarasa katika shule zao, sambamba na kukarabatiwa na kusema serikali kupitia Halmashauri ya Kinondoni inatekeleza vema sera ya Elimu bila malipo. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YA TUMIA BIL. 1.5 UJENZI WA MADARASA YA SHULE ZA MSINGI Posted On: February 4th, 2020 WALIMU WASEMA MKURUGENZI KAGURUMJULI AN... + Read more »
DC CHONGOLO ASITISHA VIBALI VYA UCHIMBAJI MCHANGA MABONDENI Posted On: February 4th, 2020 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amesitisha vibali vya uchimbaji mchanga vilivyotolewa na Bodi ya Maji Bonde la Ruvu kutokana na kuleta madhara ya uharibifu wa mito na kusababisha athari kwenye makazi ya watu katika Halmashauri hiyo. Vibali vilivyositishwa katika ni vile vilivyotolewa kufanya shughuli hizo katika Bonde la mto Salasala, Mto mbezi, Ndumbwi, Nyakasangwe, na kusema kuwa mito hiyo inapita katikati ya makazi ya watu na kwamba baada ya kufanyika marekebisho utawekwa utaratibu upya wa kufanya shughuli hizo. Akizungumza mara baada ya kufanya ziara katika Bonde la mto Salasala (Mto Tegeta) Mhe. Chongolo amesema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya wakandarasi waliopewa vibali hivyo kuharibu mto huo na hivyo kuamuru kupandwa kwa Miti hiyo ambayo itasaidia kuzuia mmomonyoko wa udongo. Amesema kuwa kinachofanyika hivi sasa ni kurekebisha mito hiyo kwa kupanda miti, magugu pamoja na mianzi inayoshika ardhi ili kuzuia mmomonyoko wa undongo na hivyo kuweka mkakati wa kuratibu shughuli za utoaji mchanga kufanyika katika maeneo hayo. Mhe. Chongolo amesena kuwa katika Halmashauri hiyo ameruhusu kibali hicho kutolewa katika bonde la Mpigi kwa maelekezo ya kuhakikisha kuwa shughuli hizo zifanyike kwa ajili ya kusafisha mto ili kuondosha adhari kwani mchanga ukijaa sana husababisha maji kusambaa nje. “ Wakati tunafanya haya ni lazima tusitishe shughuli zote zinazofanyika hapa, tulifanya tathimini ya kuangalia athari kwa kuunda timu ambayo ilikamilisha majukumu yake na kuleta ripoti hiyo Disemba mwaka jana, mwezi wa kwanza mwaka huu tulianza mjadala na wale ambao walipewa kandarasi ya kutoa mchanga kwenye mito hii” amesema Mhe. Chongolo Nakuongeza kuwa “ baada ya majadiliano hayo, tulikubaliana nao kupanda Miazi, Miti na Magugu, na watu ambao mnawaona hapa asilimia 90 niliagiza kila mwenye kibali cha bonde anayekuja aje na watu 10 kwa ajili ya kushirikiana kupanda miti, na hii miti inayopandwa hapa sijanunua wameleta wao” ameongeza Mhe. Chongolo. Mhe. Chongolo amesisitiza kuwa “ kwanza mchanga usiondolewe kibiashara ,tutoe mchanga sehemu ambayo tunaona kuwa kunaongezeko ambalo linaweza kusababisha athari, ili turuhusu maji yapite bila kuleta madhara kwa wananchi waliopo pembezoni mwa mto na huyo anayetoa ahakikishe anafanya marekebisho ikiwemo kupanda miti, magugu na mianzi. Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo amesema kuwa " Tunachangamoto ya watu kufanya shughuli za kibinadamu kwenye maeneo ya maji, Serikali imeshaelekeza watu ambao wapo kwenye maeneo haya wanatakiwa kuwa umbali wa mita 60 kwa 60 , lakini hatufuati hiyo Sheria ya mazingira. Wananchi mliopo katika maeneo haya, niwasihi sana acheni kufanya shughuli hapa, leo tunapanda miti ili kunusuru bonde hili lisiendelee kukua, mchanga utatolewa kwa kibali kwa ajili ya kusafisha mto ila sio kuchimba mchanga kwa shughuli ya kibiashara ama nyingine, " amesema Mhe. Chongolo. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni DC CHONGOLO ASITISHA VIBALI VYA UCHIMBAJI MCHANGA MABONDENI Posted On: February 4th, 2020 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chong... + Read more »
KINONDONI YA SAINI MKATABA NA JWTZ UJENZI WA UWANJA W AKISASA, JENGO LA UTAWALA Posted On: January 27th, 2020 MEYA SITTA ASEMA MKURUGENZI KAGURUMJULI NI MSIKIVU. ya Manispaa ya Kinondoni leo imesaini mkataba na Jeshi la Wananchi (JWTZ) kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa wa kisasa wa mpira wa miguu pamoja na Jengo la kisasa la Utawala la Halmashauri hiyo. Mkataba huo umesainiwa leo na Mstahiki Meya wa Halmashauri hiyo Mhe. Benjamini Sitta pamoja na Luteni Kanali David Michael Luoga na kushuhudiwa na watendaji wa Halmashauri hiyo pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kinondoni Harlod Maruma. Akizungumza na wandishi wa habari wakati wa utiaji saini wa mkataba huo, Mhe. Meya Sitta amesema kuwa mradi wa ujenzi wa jengo la utawala utagarimu kiasi cha shilingi Bilioni 1.6 huku ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu ukigarimu kiasi cha shilingi Bilioni 2.7. Amefafanua kuwa uamuzi wa kutumia JWTZ umetokana na kufuata ushauri uliokuwa unatolewa na Mhe. Rais Dk. John Pombe Magufuli wakutumia Locol Fundi (Foce Account). Mhe. Meya amesema kuwa miradi hiyo mikubwa miwili iliyosainiwa leo itajengwa na Jeshi la Wananchi kwakuwa wana amini watafanya kazi hoyo kwa umakini mkubwa na wa haraka kulingana na mkataba huo ulivyoeleza. “ Tunamshukuru Mhe. Rais wetu mpendwa, Dk. Magufuli kwa kutuonyesha njia ya kufanya kazi kwa kutumia wanajeshi kwa kuwa itakamilika kwa wakati, hapa hakuna michakato, miradi hii mikubwa itafanywa na jeshi la JWTZ” amesema Meya Sitta. Aidha Mhe. Meya Sitta amesema “ tunampongeza Mkurugenzi wetu Aron Kagurumjuli, kwakweli tuna mkurugenzi makini, msikivu ,ambaye anafuata maelekezo na ni mchapakazi ndio mana leo Kinondoni yetu ipo hapa” ameongeza. Kwa upande wake Luteni Kanali Luoga ameipongeza Manispaa ya Kinondoni kwa kuwaamini kufanya kazi hiyo na kuahidi kukalimisha ujenzi huo kwa muda wa miezi sita. Luteni Luoga amesema katika ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu, awamu ya kwanza itakamilika kwa kipindi cha miezi mitatu na nusu na awamu ya pili itatumia miezi miwili na nusu. Ameongeza kuwa katika ujenzi huo ,licha ya kwamba Jeshi la Wananchi litafanyakazi hiyo,lakini pia litatoa nafasi kwa watu wengine ikiwemo Mama ntilie pamoja na vijana wengine lengo likiwa ni kila mwananchi apate kipato. “ Tunampongeza Mhe. Meya Sitta, Mkurugenzi Kagurumjuli kwa kutuamini, nasisi tunawahakikishia kuwa Jengo la utawala pamoja na uwanja tutakamilisha kwa kipindi cha miezi sita kama ilivyo kwenye mkataba wetu”amesema Luteni Kanali Luoga. Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Mhe. Harlod Muruma amefafanua kuwa ujenzi huo wa miradi mikubwa miwili iliyotiwa saini leo ni utekelezaji wa ilani CCM. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YA SAINI MKATABA NA JWTZ UJENZI WA UWANJA W AKISASA, JENGO LA UTAWALA Posted On: January 27th, 2020 MEYA SITTA ASEMA MKURUGE... + Read more »
BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LA PITISHA BAJETI YA BILIONI 170.9 Posted On: January 23rd, 2020 Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, katika Mkutano wake maalumu wa Baraza leo Alhamisi, tarehe 23 Januari 2020, limejadili na kuidhinisha kwa kauli moja bajeti yake ya Tshs 170, 918,524,100/= kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ambapo Tshs.42,951,312, 000/= ni za Mapato ya ndani ya Manispaa na Tshs. 127,967,212,100/= ni Mapato ya Ruzuku kutoka Serikali kuu zikijumuisha Tshs. 57,018,968,680/= kwa ajili ya mishahara,Tshs.1,689,501,000/= za matumizi mengineyo na Tshs. 69,258,742,520, /= za miradi ya maendeleo. Kiasi cha ,Tshs. 42,951,312,000/= kilichotengwa na Manispaa ya Kinondoni kutokana na makusanyo ya vyanzo vya ndani vya, Manispaa kinajumuisha Tshs.883,467,270/=, kwa ajili ya mishahara ,Tshs. 21,353,714,130,000/= kwa ajili ya matumizi mengineyo na Tshs. 20,714,130,000/= kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Azungumza wakati wa kupitisha Bajeti hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh Benjamin Sitta amebainisha kuwa ili kuboresha maisha ya wakazi wa Kinondoni, Manispaa imeandaa mpango wa mwaka 2020/2021 na mpango wa muda wa kati 2020/2021 – 2022/2023 unaolenga kukuza uchumi na kupunguza umaskini na kufikia maendeleo endelevu ya kijamii, kiuchumi,na kimazingira kwa wananchi wake. Meya Sitta ametanabaisha kuwa Ili kutekeleza dhana nzima ya ugatuaji wa madaraka , mpango huo umeshirikisha jamii katika mpango shirikishi kuanzia ngazi ya Mtaa kwa kuzingatia vipaumbele na mahitaji halisi ya Wananchi katika maeneo yao na kujielekeza katika kutoa kipaumbele maeneo yanayoweza kutoa matokeo ya haraka yatakayosaidia ukuaji wa uchumi kwa haraka na kwa kipindi kifupi. Ameyataja maeneo ya kipaumbele kuwa ni pamoja na kuboresha na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kuwekeza katika miradi mikubwa ya Kimkakati, kuboresha miundombinu ya Afya, na Elimu,kuboresha hifadhi ya mazingira na ukusanyaji wa taka, kuimarisha ushirikishaji wa jamii katika upangaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo, na uboreshaji wa mazingira ya wafanyabiashara wadogowadogo kwa kuwajengea masoko katika maeneo mbalimbali. Ili kufikia malengo yaliyokusudiwa, Mstahiki Meya amewataka viongozi na watendaji wote kusimamia uimarishaji wa mahusiano mazuri kati ya Serikali ,Mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau wengine, kujenga uwezo na ujuzi kwa watumishi katika utoaji wa huduma, kuimarisha utawala bora, uwajibikaji na uwazi sambamba na kujenga uwezo kwa viongozi wakiwemo waheshimiwa madiwani na wenyeviti wa Serikali za mitaa katika kusimamia shughuli za Wananchi. Aidha Mstahiki Meya amewashukuru wadau wote waliofanikisha bajeti hiyo zikiwemo kamati zote za kudumu za Manispaa, Serikali kuu iliyotenga kiasi kikubwa cha fedha kugharamia Miradi mikubwa ya kimkakati ya ujenzi wa soko la Tandale, Soko la Magomeni uboreshaji wa Fukwe za Cocobeach na miradi mingine ya sekta mbalimbali inayotekelezwa ndani ya Manispaa ya Kinondoni kwa Fedha kutoka Serikali kuu. Miradi iliyotengewa fedha kwa Mapato ya ndani ya Manispaa katika mwaka wa fedha 2020/2021 ni pamoja na ukamilishaji wa kituo cha kisasa cha daladala Mwenge kwa milioni 500, ukamilishaji ujenzi wa uwanja wa mpira Mwenge kwa milioni 500, ujenzi wa standi ya kisasa ya daladala na soko Tegeta nyuki kwa bilioni 3.5, ujenzi wa kituo cha kisasa cha daladala Bunju B kwa milioni 600,ujenzi wa maabara, famasia, rediolojia, na ununuzi wa gari la kubeba wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya Mabwepande kwa bilioni 1 na ujenzi wa incinerator kubwa kwa ajili ya kuchoma taka za vituo vyote vya kutolea huduma za afya kwa billion 1.5. Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Uhusiano Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LA PITISHA BAJETI YA BILIONI 170.9 Posted On: January 23rd, 2020 Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mani... + Read more »