Top ad

Top ad

KINONDONI YA SAINI MKATABA NA JWTZ UJENZI WA UWANJA W AKISASA, JENGO LA UTAWALA

Posted On: January 27th, 2020
 MEYA SITTA ASEMA MKURUGENZI KAGURUMJULI NI MSIKIVU.
 ya Manispaa ya Kinondoni leo imesaini mkataba na Jeshi la Wananchi (JWTZ) kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa wa kisasa wa mpira wa miguu pamoja na Jengo la kisasa la Utawala la Halmashauri hiyo.
Mkataba huo umesainiwa leo na Mstahiki Meya wa Halmashauri hiyo Mhe. Benjamini Sitta pamoja na Luteni Kanali David Michael Luoga na kushuhudiwa na watendaji wa Halmashauri hiyo pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kinondoni Harlod Maruma.

Akizungumza na wandishi wa habari wakati wa utiaji saini wa mkataba huo, Mhe. Meya Sitta amesema kuwa mradi wa ujenzi wa jengo la utawala utagarimu kiasi cha shilingi Bilioni 1.6 huku ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu ukigarimu kiasi cha shilingi Bilioni 2.7.
Amefafanua kuwa uamuzi wa kutumia JWTZ umetokana na kufuata ushauri uliokuwa unatolewa na Mhe. Rais Dk. John Pombe Magufuli wakutumia Locol Fundi (Foce Account).
Mhe. Meya amesema kuwa miradi hiyo mikubwa miwili iliyosainiwa leo itajengwa na Jeshi la Wananchi kwakuwa wana amini watafanya kazi hoyo kwa umakini mkubwa na wa haraka kulingana na mkataba huo ulivyoeleza.
 “ Tunamshukuru Mhe. Rais wetu mpendwa, Dk. Magufuli kwa kutuonyesha njia ya kufanya kazi kwa kutumia wanajeshi kwa kuwa itakamilika kwa wakati, hapa hakuna michakato, miradi hii mikubwa itafanywa na jeshi la JWTZ” amesema Meya Sitta.
Aidha Mhe. Meya Sitta amesema “ tunampongeza Mkurugenzi wetu Aron Kagurumjuli, kwakweli tuna mkurugenzi makini, msikivu ,ambaye anafuata maelekezo na ni mchapakazi ndio mana leo Kinondoni yetu ipo hapa” ameongeza.
Kwa upande wake Luteni Kanali Luoga ameipongeza Manispaa ya Kinondoni kwa kuwaamini kufanya kazi hiyo na kuahidi kukalimisha ujenzi huo kwa muda wa miezi sita.
Luteni Luoga amesema katika ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu, awamu ya kwanza itakamilika kwa kipindi cha miezi mitatu na nusu na awamu ya pili itatumia miezi miwili na nusu.
Ameongeza kuwa katika ujenzi huo ,licha ya kwamba Jeshi la Wananchi litafanyakazi hiyo,lakini pia litatoa nafasi kwa watu wengine ikiwemo Mama ntilie pamoja na vijana wengine lengo likiwa ni kila mwananchi apate kipato.
“ Tunampongeza Mhe. Meya Sitta, Mkurugenzi Kagurumjuli kwa kutuamini, nasisi tunawahakikishia kuwa Jengo la utawala pamoja na uwanja tutakamilisha kwa kipindi cha miezi sita kama ilivyo kwenye mkataba wetu”amesema Luteni Kanali Luoga.
Kwa upande wake  Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Mhe. Harlod Muruma amefafanua kuwa ujenzi huo wa miradi mikubwa miwili iliyotiwa saini leo ni utekelezaji wa ilani  CCM.

Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

0 comments:

Post a Comment

 
Top