Top ad

Top ad

 

MGOGORO WA ARDHI ENEO LA CHASIMBA, CHACHUI ,CHATEMBO PAMOJA NA KIWANDA CHA SARUJI CHA WAZO WAFIKIA TAMATI

Posted On: March 13th, 2021

Mgogoro huo wa kiwanja chenye ukubwa wa hecta 224.8 uliodumu kwa takribani Miaka Saba ukihusisha wananchi wapatao 4000 kutoka   cha simba  chatembo, chachui pamoja na kiwanda cha saruji cha Wazo umemalizika leo.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mhe.William lukuvi kukutana na wananchi katika mkutano wa hadhara na kutoa mapendekezo yaliyofikiwa katika mazungumzo ya muda mrefu kati ya Serikali na bodi ya kiwanda cha saruji kuhusiana na mstakabali wa wananchi katika  eneo  ambalo thamani yake ni takribani bilioni 60 za kitanzania.

Amesema " Leo tunabadilisha historia ya kuitwa wavamizi , na kuwa wamiliki halali baada ya kila mmoja wenu kutimiza wajibu wake unaompasa ndani ya miezi sita kuanzia Sasa, utakaompa kila mwananchi haki ya kumiliki kihalali baada ya taratibu  zote za umilikishwaji kukamilika. Hii ndio Serikali ya Dr.John Pombe Joseph Magufuli inayojali wananchi wanyonge" Mhe. William Lukuvi..

Aidha amesisitiza kuwa lengo la Serikali si kuingilia muhimili wa mahakama, bali ni kutafuta suluhu yenye lengo la kunufaisha pande zote mbili kwa mstakabali wa nchi yetu.

Ameongeza kuwa kukamilika kwa wajibu wa kila mwananchi  kutafuatiwa na taratibu za umilikishwaji wa ardhi kihalali na upatikanaji wa  maeneo muhimu kama vile maeneo ya makazi, biashara, huduma za Jamii, maeneo ya shule, zahanati, ofisi chekechea, makanisa na masoko.

Katika hatua nyingine Mhe. Lukuvi ameruhusu Manispaa ya Kinondoni kupeleka huduma muhimu za Jamii Kama vile shule, zahanati, vituo vya afya pamoja na kuboresha mtandao wa barabara utakaowarahisishia wananchi hao katika shughuli zao za kila siku.

Mkutano huo umehudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wakiwemo wa vyama na Serikali kwa lengo la kuongeza nguvu ya pamoja Katika kuhakikisha Sera ya Serikali ya awamu ya tano ya kutetea wanyonge inatekelezwa. 

Imeandaliwa na

Kitengo Cha Habari na Uhusiano.

Manispaa ya Kinondoni.

0 comments:

Post a Comment

 
Top