Top ad

Top ad

TAMISEMI YARIDHISHWA NA MATUMIZI MAZURI YA FEDHA ZA MAPATO YA NDANI KATIKA MIRADI YA MAENDELEO KINONDONI

Posted On: June 25th, 2020

Hayo yamebainishwa na Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Josephat Kandege alipozuru Kinondoni kwa lengo la ukaguzi wa miradi ya maendeleo, kujiridhisha na hatua za utekelezaji wake unaoenda sambamba na thamani ya fedha na ukamilishaji wa viwango kwa wakati.

Amesema kuwa Manispaa hiyo ni mfano wakuigwa kwa kuwa imeonesha nidhamu nzuri katika matumizi ya fedha zinazotokana na vyanzo vya mapato ya ndani na kwamba miradi ambayo imetekelezwa kupitia fedha hizo inaendana na thamani halisia.

 “Kimsingi leo nimemaliza ziara yangu katika Halmashauri hii, na kikubwa nilikuwa nimelenga zaidi kuona fedha zinazokusanywa  na Halmashauri  na namna ambavyo zinatumika katika miradi ambayo inaonekana na kimsingi naomba niwapongeze sana Kinondoni,  mnazitendea haki fedha zenu mnazokusanya” amesema Mhe. Kandege.

Kadhalika Mhe. Kandege ameridhishwa na kiwango cha barabara zinazojengwa katika Halmashauri hiyo kupitia mradi wa DMDP na kusema kuwa kukamilika kwake kutaleta mafanikio makubwa kwa wananchi hususani watumiaji wa barabara ya Shekilango na kwamba itaondoa msongamano wa daladala na kuwawezesha wananchi kuondokana na adha ya foleni.

Amefafanua kuwa Mafanikio haya yanayoonekana leo Kinondoni ni kutokana na uongozi imara wa Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na usimamizi mzuri wa Mkurugenzi ndg. Aron Kagurumjuli ulioleta tija kwa Wananchi.

Katika hatua nyingine Mhe.Kandege ameipongeza Manispaa ya Kinondoni kwa kujenga kituo cha Afya katika Kata ya Kigogo na kusema kuwa walifanya mamuzi ya busara na yakujali wananchi kwakuwa eneo hilo halikuwa na Hospitali na kwamba litawasaidia wakazi hao kupata huduma bora ya afya.

 “Kinondoni mliona mbali kuweka kituo cha Afya pale Kigogo, mlitumia busara ya hali ya juu mkaona ni bora mnunue eneo kwa ajili ya kuwajengea wananchi kituo cha Afya, hivyo hata kwenye Kata ya Kawe kwa ujumla ukiondoa Kawe kama Kawe eneo lililobaki halikuwa na kituo cha Afya, pamoja na ujenzi wa Hopsitali ya Wilaya nilazima uwe navituo hivi ili hata mgonjwa wa eneo jirani apate huduma.

Katika ziara hiyo Mhe. Kandege ametembelea Barabara ya shekilango inayojengwa kwa kiwango cha lami kwa shilingi Bilioni 14. 8, mfereji wa Kilongawima uliyopo Jimbo la Kawe kwa shilingi Bilioni 3.1 pamoja na upanuzi wa Zahanati ya Bunju mradi unajongekwa cha shilingi Milioni 600.


Imeandaliwa na

Kitengo cha Habari na Mahusiano

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.


0 comments:

Post a Comment

 
Top