Top ad

Top ad

MADIWANI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA KUJIFUNZA NAMNA YA UKUSANYAJI MAPATO KATIKA HALMASHAURI YA KINONDONI

Posted On: November 27th, 2019
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro  wamefanya ziara ya kujifunza namna ya ukusanyaji mapato katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
Madiwani hao waliokuwa wameambata na Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Regina Chonjo, Mstahiki Meya Amir Nondo wamepokelewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli na Mstahiki Meya Benjamini Sita.
Aidha madiwani hao pia wamepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo , Katibu Tawala Stela Msofe pamoja na watumishi wengine wa Idara na vitengo ambapo pamoja na mambo mengine walipata nafasi ya kutembelea miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo Soko la Kisasa la Magomeni linalojengwa kwa shilingi bilioni 8.9.
Awali kabla ya kutembelea miradi hiyo , madiwani hao walipata nafasi ya kujifunza mbinu mbalimbali za ukusanyaji wa mapato zilizotolewa na Msimamizi wa Mapato wa Halmashauri ya Kinondoni Zahoro Rashidi.
Akizungumzia ziara hiyo, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Morogoro Mhe. Nondo alisema kuwa wamekuja kujifunza namna ya ukusanyaji wa mapato kwakuwa Halmahauri ya Kinondoni imekuwa ikifanya vizuri kwenye ukusanyaji.
“ Tumekuja kujifunza namna ya ukusanyaji mapato, ukiangalia kwenye takwimu zetu sisi tupo nyuma, sasa leo tumekuja kuona wenzetu mnafanyaje hadi mnafikia malengo, wote ni wamoja tunategemeana ,tunaomba mtupatie ujuzi mliokuwa nao” alisema Mhe. Nondo.
Kwaupande wake Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Chonjo alisema aliishukuru Manispaa ya Kinondoni kwakuwapokea vizuri na kueleza kuwa wamefurahishwa na ukarimu waliopata kutoka kwa viongozi na watendaji wa Halmashauri hiyo.
“ Lengo letu na kuja hapa ni kujifunza, tunawashukuru mmetukaribisha , undugu tuliouanzisha hapa isiwe mwisho, karibuni na nyinyi Morogoro, hili tunalolifanya ndio lile linalotakiwa na Rais Dk. John Magufuli, asanteni kwa ushirikiano wenu” alisema Mhe. Chonjo.
Akiwakaribisha Madiwani hao, Mstahiki Meya . Mhe. Sita alisema kuwa Halmashauri ya Kinondoni ipo vizuri kwenye ukusanyaji wa mapato na kwamba anawakaribisha ili waweze kujinza kwa lengo la kutimiza adhma hiyo.
Naye Mhe. Chongolo ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo alisema kuwa ili kufikia malengo ,viongozi hawana budi kuweka juhudi na nia ya dhati katika kutekeleza majukumu yao na kwamba kila mmoja anapaswa kushiriki kikamilifu katika kutekeleza wajibu wake.
“ Bila kuweka malengo ya dhati kabisa, tunaweza kufanya ziara za kujifunza tukamaliza maeneo yote, natusipae kitu, kikubwa ni kuweka nia, kama ilivyo kwa wenzetu wa kabila la hehe wakisema wanajinyonga basi wanajinyonga kweli, inamana waliweka nia , kwahiyo nasisi viongozi tuwaige wahehe katika kuweka nia ya kuleta maendeleo.

Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.

0 comments:

Post a Comment

 
Top