Top ad

Top ad

KINONDONI YAPOKEA UGENI TOKA ZANZIBAR KWA LENGO LA KUJIFUNZA MASUALA YA USHIRIKA

Posted On: November 25th, 2019
Halmashauri ya Manispaa ya kinondoni imepokea ugeni toka Zanzibar ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya kazi,Uwezeshaji, Wazee,Wanawake na  Watoto Bi Maua Rajab, Mrajis wa idara ya Ushirika pamoja na viongozi na watendaji wa FARAJA Union waliofika kwa lengo la kubadilishana uzoefu na changamoto na  wenzao wa kinondoni katika kuendesha vyama vya ushirika.
Bi Maua amesema wamechagua Kinondoni sababu wanaamini wapo vizuri katika kuendesha vyama vya ushirika hususan kwa kutumia mfumo laini kwaaajili ya usimamizi na upatikanaji wa taarifa za vyama kwa wakati na kwa usahihi.
Naye Mrajis wa Idara ya Ushirika Zanzibar Bw Hamis Daudi Simba amesema kuwa Zanzibar wana muungano wa vyama na saccos mbalimbali (FARAJA) hivyo wanaziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ambayo wamefanikiwa katika masuala ya Ushirika ili na wao waweze kuboresha Umoja wao.
Awali alitoa taarifa ya vyama vya ushirika kwa Manispaa ya kinondoni, Afisa Ushirika wa Manispaa Bi Scholastica Maganga amesema Kinondoni ina vyama vya ushirika 153 Kati ya hivyo vyama 137 Ni vya akiba na mikopo na 16 ni vya huduma mbalimbali ikiwemo chama Cha ujenzi wa nyumba.
Amesema vyama hivi vina jumla ya wanachama zaidi ya 54000 ambao wamewekeza hisa zaidi ya TShs 15 Bilioni na akiba zaidi ya Bilioni 64 na mikopo zaidi ya Bilioni 35.
Aidha sehemu ya Ushirika Manispaa ya Kinondoni kwa sasa inakamilisha mfumo laini kwaaajili ya usimamizi na upatikanaji wa taarifa za vyama kwa wakati na kwa usahihi.
Ugeni huo umepata fursa ya kutembelea wat saccos na chama Cha ujenzi wa Nyumba  Mwenge  vyama vya kijamii ambavyo vina mfano mzuri wa kuigwa hivyo ni sehemu nzuri kwao kujifunza Mambo mengi ya ushirika
Imeandaliwa na
Kitengo Cha habari na uhusiano
Manispaa ya kinondoni.

0 comments:

Post a Comment

 
Top