Top ad

Top ad

DC CHONGOLO ASIMAMA KIDETE NA WANAOZURUMU NYUMBA , ATOA ONYO KALI KWA WAHUSIKA, BI SHARIFA ARUDISHIWA NYUMBA YAKE

Posted On: November 11th, 2019
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo amesimamia haki na hivyo kuwezesha kurudishwa kwa  Nyumba ya mkazi wa Magomeni Mzimuni,Bi  Sharifa Mbaruku aliyenyang’anywa kwa muda wa miaka mitatu iliyopita.
Mhe. Chongolo alichukua maamuzi hayo leo alipofika kwenye nyumba ya Bi Sharifa ikiwa ni baada ya bibi huyo kupeleka malalamiko ya kudai kuzurumiwa na Bi Magrethi ambaye kwa sasa inadaiwa kuwa anaishi nje ya Nchi.
Akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kufika katika nyumba hiyo ,Mhe. Chongolo amesema kuwa aliyemuondoa kwenye nyumba hiyo mwaka 2016 alifanya makosa na kwamba hakuwa na haki ya kumiliki nyumba hiyo.
Amefafanua kuwa kazi ya serikali ya awamu ya tano ni kutetea wanyonge wanaozurumiwa haki zao na kwamba akiwa Mkuu wa Wilaya hiyo amerudisha umiliki wa nyumba hiyo kwa mhusika ambaye ni Bi Sharifa.
 “kuanzia hivi ninavyozungumza unarudi kwenye nyumba yako rasmi, wewe ndio mmiliki wa nyumba hii, kwahiyo nendeni mkaondoe mabati yote ambayo yamezungushiwa na sisi kama serikali tutawachukulia hatua wote waliohusika na mchezo huu" Amesisitiza Mhe Chongolo
Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo ametoa agizo na kuwataka wote wenye tabia ya kupora nyumba za watu hasa masikini na wanyonge kuacha mara moja kwani hatamuonea haya mtu yeyote aliyekuwa kwenye manispaa yake.
Kwaupande wake Bi Sharifa aliyezurumiwa nyumba hiyo,  amesema kuwa Disemba 27 mwaka 2016 akiwa amelala ilikuja gari ya polisi wakiwa na diwani wa Kata ya Magomeni wakati huo Ally Kondo pamoja na Kuruthumu Ramadhani walimtolea vitu nje na kumtaka kuondoka katika nyumba hiyo bila kutoa maelezo yoyote.
 “ Mhe. Mkuu wa Wilaya nakupongeza sana baba kwakutujali masikini, mungu akubariki na akupe maisha marefu , hata Mahakama pia inachangia kwakuwa awali ilikuja toleo la kwanza  lilionyesha 159 Block four, toleo la pili 159 Block eigth, toleo la tatu halikuwa na namba ya nyumba kwakweli huu ni uonevu” amesisitiza Bi Sharifa.

Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni    

0 comments:

Post a Comment

 
Top