Top ad

Top ad

MWENGE WA UHURU MWAKA 2019, WILAYA YA KINONDONI UMEZINDUA, UMEWEKA JIWE LA MSINGI NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO 8 YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI THEMANINI

Posted On: July 20th, 2019
Miradi iliyozinduliwa na mwenge wa Uhuru ni pamoja na mradi wa uwezeshaji wananchi kiuchumi wenye gharama ya zaidi ya Milioni 50. Mradi wa ujenzi wa Barabara ya Kilongawima kiwango Cha lami yenye urefu wa km 2 wenye thamani ya zaidi ya Bilioni 2, Mradi wa Ujenzi wa kituo Cha Afya kigogo wenye thamani ya Zaidi ya Milioni 700.
Miradi mingine ni mradi wa Ujenzi wa shule mpya ya Mivumoni uliogharimu Zaidi ya Milioni 200, Mradi wa Ujenzi wa Tanki la maji na miundombinu yake wenye gharama ya Zaidi ya Bilioni 75, Kiwanda cha ushonaji nguo wenye gharama ya kiasi Cha sh Milioni 500 na Ujenzi wa soko la Kijitonyama wenye gharama ya Zaidi ya  shillingi Milioni 100.
Aidha Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Mzee Mkongea Ally ameipongeza Kinondoni kwa kubuni na kusimamia vizuri miradi hiyo ya maendeleo ambayo itakuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi wa Kinondoni.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.

0 comments:

Post a Comment

 
Top