NITAKUWA KAMA JICHO LA PILI KATIKA KUITAFUTA TIJA TUNAYOIKUSUDIA
Posted On: August 14th, 2018
Ni maneno yake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Daniel Geofrey Chongolo alipokuwa akizungumnza na watumishi wa Manispaa ya Kinondoni kwa lengo la kujitambulisha na kutoa miongozo ya utendaji katika uongozi wake.
Amesema Mtumishi kila anao wajibu wa kusimamia makubaliano na misingi ya kazi inayomtaka kuwajibika kwa ufanisi katika kuhakikisha tija inapatikana kwa kile kilichokusidiwa.
"Mtumishi unapoajiriwa, unasaini mkataba wa utekelezaji wa majukumu, simamieni hilo, Mimi nitakuwa kama jicho la pili katika kutafuta tija tunayoikusudia "
Naye Mkurugenzi wa Manispaa hiyo alipokuwa akimkaribisha Mkuu huyo wa Wilaya amesema Kinondoni inayo idara 15, na vitengo 9, vilivyo tayari kusikiliza, kutekeleza maagizo na kushirikiana naye katika shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha uzalendo katika uwajibikaji unazingatiwa ili kuleta tija inayokusudiwa.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mh Benjamin Sitta, wakuu wa idara na vitengo pamoja na watendaji mbalimbali walioko makao Makuu, Mkurugenzi Kagurumjuli pia alimtambusha Katibu Tawala mpya wa Wilaya ya Kinondoni Bi Stella Msofe, na kumkaribisha Afisa Tarafa mpya wa Tarafa ya Kinondoni.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na habari.
Manispaa ya Kinondoni.
0 comments:
Post a Comment