Top ad

Top ad


WAZIRI WA ARDHI ARIDHISHWA NA HATUA ZA UFUNGAJI WA MFUMO WA ARDHI (ILMIS) KWA MANISPAA YA KINONDONI.
Waziri wa Ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh Willium Lukuvi aridhishwa na hatua iliyofikiwa ya ufungaji wa mfumo wa kuratibu shughuli za Ardhi (ILMIS) kwa Manispaa ya Kinondoni, ambao utamwezesha mteja kupata taarifa za ardhi pamoja na hati kwa muda mfupi.
Akiwa katika ziara yake ya kikazi Manispaa ya Kinondoni, Mh Lukuvi amepata fursa ya kushuhudia ufanyaji kazi wa mfumo huo katika hatua mbalimbali za utoaji na upokeaji wa taarifa, ulioenda sambamba na uandaaji wa hati hizo.
Akifafanua utendaji kazi wa mfumo huo Mh Lukuvi amesema mfumo huu ni shirikishi na wazi unaomtaka mteja kufuata taratibu zitakazomrahisishia kupatiwa haki yake kwa usahihi na muda mfupi.
Amesema kwa sasa hatua iliyofikiwa ni rafiki kabisa itakayomwezesha mtendaji kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya matumizi ya mfumo kutoka analogia kwenda digital
Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.0 comments:

Post a Comment

 
Top