Top ad

Top adMkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ali Hapi ametoa siku thelathini (30),kwa wataalam wa Mipangomiji na Ardhi Manispaa Ya Kinondoni kuhakikisha wanakamilisha uhakiki wa wenye mashamba katika maeneo ya Mabwepande,
Mji mwema na Mbopo.
Ametoa agizo hilo leo katika mkutano wa pamoja na wananchi wakaazi wa mabwepande uliofanyika katika eneo la Mji mpya.
Amesema uhakiki huu ni katika harakati za kutatua mgogoro uliopo kwa sasa na hasa ikizingatiwa Serikali ya awamu ya tano chini ya Mh John Pombe Magufuli imadhamiria kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa migogoro ya Ardhi na kwamba mkakati wa Wilaya uliopo ni kufuta mashamba na kuwa na viwanja vilivyopimwa katika Manispaa.
"Tunataka tuondoe kitu kinachoitwa mashamba, mashamba gani, mnalima nini?, tunataka tupange mji wetu katika viwanja "amesema Hapi.
Akiitaja kauli mbiu yake katika maswala ya migogoro ya ardhi ambayo ni "Tunasikiliza, tunatekeleza" amewataka wakaazi wa maeneo hayo kuwa wasikivu, na kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa wataalam wa Mipangomiji ili uhakiki uweze kufanikiwa kwa lengo lililokusudiwa.
Ameongeza kuwa kila mwenye shamba ahakikishe siku ya uhakiki anakuwa na nyaraka zake zote zinazomtambulisha uhalali wake na kila mtu asimame kwenye eneo lake.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya amesimamisha uendelezaji wa aina yeyote katika kipindi hiki ili kupisha zoezi la uhakiki.

0 comments:

Post a Comment

 
Top