Top ad

Top ad

Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Kinondoni chini ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Amour Hamad Amour umetembelea, umezindua na kuweka jiwe la Msingi kwenye miradi Sabá (7) yenye thamani ya Tsh Bilion 8.9
Miradi hiyo ni kama ifuatavyo: Mradi wa Jengo la NHC wenye ghorofa nane, na vyumba vya makazi 26, Mradi wa ujenzi wa wodi ya wazazi Kijitonyama ambapo huduma za Afya ya Mama na mtoto hutolewa na Mradi wa kiwanda cha ngozi.
Miradi mingine ni Ujenzi wa Daraja la Ununio ulioko Kata ya Kunduchi, Mradi wa Kituo cha Polisi Mbweni, mradi wa jengo la Utawala shule ya Msingi Ally Hapi na Mradi wa uwezeshaji vijana kiuchumi.
Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Kinondoni utakesha katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe kuanzia saa 9:007Alasiri. Wanachi wote mnakaribishwa 

0 comments:

Post a Comment

 
Top