Top ad

Top ad

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Ahmed Amour Ahmed ameipongeza Wilaya ya Kinondoni kwa kuwa na jitihada chanya za kuiunga mkono Serikali ya awamu ya tano yenye lengo la kukuza Uchumi kupitia viwanda.
Pongezi hizo zimekuja baada ya Mwenge Wa Uhuru Wilaya ya Kinondoni kutembelea kiwanda cha Ngozi kilichopo Salasala Kata ya Kunduchi ambacho kinajishughulisha na utengenezaji wa bidhaa bora za ngozi.
Kiwanda hicho chini ya Uongozi wake WOISO kimejikita katika shughuli za utengenezaji wa bidhaa kama vile viatu vya shule mabegi ya shule pamoja na mabegi ya kusafiria.
Bidhaa nyingine zinazopatikana kiwandani hapo ni Mikanda ya suruali, majaketi ya Mvua na ya baridi, viatu vya ngozi,viatu vya wazi, Sandos pamoja na Masofa.
Katika hatua nyingine kiwanda hicho kimeajiri watanzania wazawa 224, wakiwemo wanawake 136 na wanaume 88 wote wakijishughulisha na bidhaa za ngozi kutoka Tanzania.
Mwenge wa Uhuru upo Jijini Dar es Salaam kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, ambapo siku ya leo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Salum Hapi amekabidhiwa Mwenge huo ukitokea Wilaya ya Ilala.


0 comments:

Post a Comment

 
Top