Top ad

Top ad

Manispaa ya Kinondoni leo imepokea ujumbe wa Baraza la Madiwani kutoka Halmashuri ya Manispaa ya Ilemela waliokuja kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu katika maswala ya utendaji.
Ujumbe huo wa Baraza la Madiwani chini ya Mstahiki Meya wao Mh. Renatus Mulunga uliambatana pia na watendaji wa idara mbalimbali kutoka Halmashauri hiyo wakiwemo idara ya sheria, Afya, Utumishi, Mipangomiji, pamoja na mwandishi wa Mikutano.
Akiwakaribisha Kinondoni hapo Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mh Sitta amesema amefurahishwa sana na ujio wao kwani kwa kufanya hivyo ni hatua katika kujifunza na pia ni njia pekee katika kubadilishana uzoefu katika utendaji.
Mada zilizowasilishwa na Manispaa ya Kinondoni kwa wageni hao ni pamoja na Jinsi ya kupanga, kupima na kuendeleza miji ili kudhibiti makazi holela.
Mada nyingine ni mikakati inayotumiwa na Manispaa ya Kinondoni katika kukusanya, na kuondosha taka ngumu, vyanzo vya mapato vya Halmashauri pamoja na mbinu zitumiwazo kukusanya mapato.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Bw Aron Kagurumjuli amesema ujio wao umeonyesha imani kubwa kwa wanakinondoni, na kwamba wamefanya vema kuja kujifunza kwani ndio Halmashauri Mama Tanzânia kwa maswala ya ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mfumo.
Amesema kwa ujio wao ni mwanzo mzuri wa kujenga mahusiano ya kiutendaji yenye tija na yatakayoleta manufaa kwa wengine hasa ikizingatiwa Halmashauri lazima ikusanye mapato.
Katika hatua nyingine Manispaa ya Ilemela imefurahishwa na mbinu zinazotumiwa na Manispaa ya Kinondoni katika kukusanya Mapato ambapo hutumia mfumo wa Mashine za Kielektroniki
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
Mstahiki meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh Benjamini sitta akiwa karibisha wageni kipindi cha kufungua Kikao  cha mafunzo 
Timu ya wataalam Wa Manispaa ya Kinondoni 









0 comments:

Post a Comment

 
Top