KINONDONI YAPOKEA MIFUKO 400 YA CEMENTI KUTOKA KANISA LA INUKA UANGAZE Posted On: January 25th, 2019 Akipokea mifuko hiyo ya cementi kutoka kanisa la Inuka uangaze linaloongozwa na Mtume Boniface Mwamposa, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Daniel Chongolo amesema imekuja wakati muafaka kwani itasaidia kuleta hamasa ya nguvu ya wananchi katika kuhakikisha kunakuwepo na mafanikio ya utatuzi wa changamoto kubwa ya madarasa iliyoko Wilayani hapo. Amesema Serikali ya awamu ya tano dhamira yake kuu ni kuboresha miundombinu ya elimu pamoja na mfumo wake, hivyo mifuko hiyo imekuja kipindi ambacho Wilaya yake imepanga kufikia mwezi wa tatu mwaka huu iwe imekamilisha madarasa mia moja. "Tunamshukuru na kumpongeza Mchungaji na Mtume Mwamposa pamoja na kanisa lake lote, kuona umuhimu wa kuchangia swala la elimu, niseme tu kwamba Msaada huu wa mifuko ya cement umekuja wakati mwafaka, kwani tulishajiwekea malengo mkakati ya kutatua changamoto iliyopo mbele yetu ya vyumba vya madarasa kwa kushirikiana na nguvu za wananchi kuhakikisha tunajenga mdarasa mia moja ifikapo mwezi wa tatu, ikiwa ni hatua za awali za kuhakikisha tunakabiliana na upungufu wa vyumba vya madarasa katika Wilaya yetu.".Amebainisha Chongolo Ameongeza kuwa Jamii yetu inajengwa na taasisi mbalimbali ambazo kwa pamoja zikishirikiana na serikali zitaleta Matokeo chanya, hivyo tukio la leo limedhihirisha nia thabiti mliyonayo ya kumuunga mkono Mh. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ya kuboresha miundombinu ya elimu Nchini. Akikabidhi mifuko hiyo, Mchungaji na Mtume Boniface Mwamposa amesema ni katika kuunga mkono juhudi za Mh Rais katika kuboresha sekta ya Elimu, kadhalika ni kutekeleza agizo la Mungu, kwani hata biblia imeandika katika kitabu cha Mithali 4:13 kuwa "mkamate sana elimu, usimwache aende zake mshike, maana yeye ndo uzima wako" na kuahidi kuendelea kusaidia swala zima la elimu pale inapopasa. Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe Benjamin Sitta katika kushuhudia ugawaji huo wa mifuko ya cement ameupongeza uongozi mzima wa kanisa hilo kwa azma njema waliyonayo katika elimu, na kuzihamasisha taasisi nyingine kufanya hivyo ili kuleta tija katika sekta hii Muhimu ya Elimu katika Taifa letu. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAPOKEA MIFUKO 400 YA CEMENTI KUTOKA KANISA LA INUKA UANGAZE Posted On: January 25th, 2019 Akipokea mifuko hiyo ya cementi ku... + Read more »
MSTAHIKI MEYA MANISPAA YA KINONDONI APOKEA UJUMBE KUTOKA HONG KONG POLYTECHNIC UNIVERSITY (HKPU) Posted On: January 25th, 2019 HALMASHAURI YA MANIPAA YA KINONDONI Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamin Kawe Sitta leo amepokea ujumbe kutoka Hong Kong Polytechnic University ( HKPU) ambapo wamekutana na kufanya mazungumzo yenye lengo la kuanzisha Ushirikiano wa Kitaasisi utakaosaidia kuimarisha uwezo wa Taasisi zetu mbili za Kilimo Malolo na ufundi Wazo katika kutoa taaluma bora zaidi na hatimaye kuweza kufikia malengo ya manispaa ya Kuwawezesha Wanufaika wa Mikopo ya Wanawake na vijana kunufaika na Tekinolojia itakayotolewa katika vyuo hivyo. Ujumbe huo wa Chuo Kikuu cha HKPU Umeongozwa na Ndugu CHAN Stephen ,Mkuu wa Idara ya Mafunzo kwa njia ya kujitolea na Profesa Grace Ngai ,Mkuu wa Idara ya Komputa ambapo Mstahiki Meya wa Kinondoni Pamoja na Mambo mengine ametumia fursa hiyo kuwakaribisha Tanzania na kuwashukuru kwa nia na dhamira ya Chuo hicho kuanzisha Ushirikiano wa Kitaasisi na vyuo vya Tanzania ikiwemo Kituo cha Mafunzo Malolo na Chuo cha Ufundi Wazo kinachotarajia kufunguliwa mwezi Februari mwaka huu 2019. Akizungumza na Ujumbe huo Mstahiki meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamini Kawe Sitta, amewataka Wakazi wa Manispaa ya Kinondoni hususani wanufaika wa Mikopo ya Wanawake na Vijana inayotolewa na Manispaa kujiunga kwa mafunzo mbalimbali ya ufundi katikia vituo hivyo viwili ili waweze kunufaika na ushirikiano wa Manispaa ya Kinondoni na chuo hiki Maarufu cha Hong Kong Polytechnic University. Kiongozi wa Ujumbe huo Ndugu CHAN Stephen Mkuu wa Idara ya mafunzo kwa njia ya kujitolea, katika mazungumzo yake amesema kuwa ziara yake hapa Nchini Tanzania inatokana na Fursa zilizopo za kutoa Huduma za Kijamii katika Nyanja za Kiteknolojia na ufundi kama wanavyofanya Nchini Rwanda hivyo ujio wake ni mwanzo mpya wa Mashirikiano katika nyanya hizo .Pia amewawakikishia Watanzania Kunufaika na Ushirikiano wa Kihistoria uliopo kati ya Tanzania na China. IMETOLEWA NA: KITENGO CHA HABARI, MAWASILIANO ITIFAKI NA MAHUSIANO HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI. MSTAHIKI MEYA MANISPAA YA KINONDONI APOKEA UJUMBE KUTOKA HONG KONG POLYTECHNIC UNIVERSITY (HKPU) Posted On: January 25th, 2019 HALM... + Read more »
WAKULIMA KINONDONI WAMETAKIWA KUELEWA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIA NCHI KATIKA SEKTA YA KILIMO ILI WAWEZE KUKABILIANA NAZO Posted On: January 18th, 2019 Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bi.Stella Msofe, alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tatu yaliyoendeshwa katika kituo cha kilimo malolo kwa lengo la kutoa elimu mahususi juu ya mabadiliko ya tabia nchi katika sekta ya kilimo na jinsi ya kukabiliana nayo. Amesema ni lazima wakulima hawa wapatiwe elimu ya kutosha itakayowawezesha kuepukana na athari hizo, kwani kilimo ndio uti wa Mgongo wa Taifa letu, hasa ikizingatiwa tunahitaji malighafi za kutosha kuendeshea viwanda vyetu, ambayo kwa sasa ndio sera ya Serikali ya awamu ya tano, Serikali ya viwanda. Amesema "Bahati nzuri Kinondoni tunayohazina ya wataalam wa sekta hii, tunacho kituo bora kabisa kwa ajili ya elimu hiyo, kwanini tushindwe kutoa elimu kwa walengwa?, kwanini wakulima wetu wasipate elimu, wataalam hawa wapo, na wanalipwa kwa kazi hiyo, hivyo watumieni, kwani jukumu lao ni kurudisha ujuzi, elimu na maarifa kwa jamii husika." Bi.Msofe. Awali akiainisha lengo zima la mafunzo hayo kwa Katibu Tawala huyo, Mkuu wa Idara ya kilimo na mifugo Manispaa ya Kinondoni, ambaye pia ni msimamizi wa kituo cha kilimo Malolo, Bw Salehe Hija amesema, mafunzo haya yaliyohusisha wakulima 40, kutoka Kata tano za Manispaa hiyo, yamelenga si tu kutoa uelewa, bali pia kuainisha njia sahihi za kupambana na changamoto zake, ili wakulima waweze kufanya kilimo chenye tija. Amezitaja Kata zilizoshiriki mafunzo hayo kuwa ni kata ya Mbweni, Bunju, Mabwepande, Wazo na Kunduchi, na kuwataka wakulima hao kuwa mabalozi kwa wakulima wengine kwa elimu waliyoipata, ili elimu ienee na kuweza kuleta tija. Akishukuru uongozi wa Manispaa ya kinondoni kwa kuendesha mafunzo hayo, kwa niaba ya wakufunzi wengine, Mwenyekiti wa wakulima waliopatiwa mafunzo hayo Bw John Malekela amesema elimu hii ni hazina tosha kwa sekta nzima kwa Wilaya yetu, kwani tunaahidi kuitendea kazi ili waweze kuepukana na changamoto hizo za mabadiliko ya tabia nchi na waweze pia kujiongezea thamani ya mazao yao. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Manispaa ya Kinondoni. WAKULIMA KINONDONI WAMETAKIWA KUELEWA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIA NCHI KATIKA SEKTA YA KILIMO ILI WAWEZE KUKABILIANA NAZO Posted On: Ja... + Read more »
MKURUGENZI WA MANISPAA YA KINONDONI AMEWATAKA WAKANDARASI WANAOFANYA KAZI YA KUZOA TAKA KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA MANISPAA HIYO KUFANYA KAZI HIYO KWA KUZINGATIA MIKATABA YAO. Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Ndugu Aron Kagurumjuli ametoa kauli hiyo leo alipokutana na wakandarasi hao kwenye ukumbi wa Manispaa kwa lengo la kuzungumza nao kufuatia kuwepo kwa malalamiko kutoka kwenye baadhi ya mitaa Kuwa kuna wakandarasi ambao hawafanyi majukumu yao kikamilifu hali inayopelekea uchafu kuzagaa kwenye baadhi ya maeneo. Amesema wakandarasi hao wameomba zabuni ya kuzoa taka katika kata na mitaa jukumu lao la msingi ni hilo hivyo hakuna sababu yoyote kwao kuacha majukumu yao ya msingi kwa kigezo Cha kuwepo kwa utaratibu mpya wa ukusanyaji mapato kwani utaratibu huo hauathiri na Wala hautaathiri malipo yao kwa mujibu wa mkataba. Akitoa ufafanuzi juu ya utaratibu mpya wa ukusanyaji wa mapato ya taka, Mkurugenzi Amesema kuwa wamefikia uamuzi wa kutumia utaratibu huo baada ya kufanya upembuzi yakinifu na kujiridhisha kuwa utaratibu huo utasaidia kudhibiti mapato ambayo hapo awali yalikuwa yakipotea. Utaratibu wa sasa unamuacha mkandarasi na jukumu moja tuu la kuzoa taka na jukumu la kukusanya mapato linabaki kwa serikali ya mtaa, na mkandarasi atalipwa kwa mujibu wa kiwango Cha tripu (awamu) za taka alizozoa. Aidha Mkurugenzi amewaagiza watendaji wa kata na mitaa kusimamia kikamilifu zoezi la uzoaji wa taka katika kata na mitaa yao huku akiwataka kutenga maeneo maalumu ambayo taka zitakusanywa hapo kwa siku maalum ili ziweze kufikiwa kwa urahisi na magari ya kuzolea taka. Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe Benjamin Sitta amewasisitiza wakandarasi hao kushirikiana bega kwa bega na Halmashauri katika shughuli hizi za uzoaji taka kwani nia ya Halmashauri kuboresha namna ya ukusanyaji wa mapato ni njema kabisa na Halmashauri ipo tayari kupokea maboresho yoyote yatakayoonekana yanastahili. Imeandaliwa naKitengo Cha Habari na UhusianoManispaa ya Kinondoni. +7 MKURUGENZI WA MANISPAA YA KINONDONI AMEWATAKA WAKANDARASI WANAOFANYA KAZI YA KUZOA TAKA KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA MANISPAA HIYO KUFA... + Read more »
KINONDONI YAZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO TAKRIBANI 5000 KWA WAMACHINGA Posted On: December 11th, 2018 Akizindua zoezi hilo katika soko la Mwenge, Mkuu wa Wilaya ya Kinondonii Mh. Daniel Chongolo amesema, ni katika kutekeleza agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli, la kuwajengea mazingira mazuri wafanyabiashara wadogowadogo kwa kuwatambua na kuwapatia vitambulisho watakavyovitumia katika kazi zao. Amesema ni zoezi endelevu, kwani vitambulisho hivi vilivyotengenezwa na Ofisi ya Rais -TAMISEMI vimelenga wafanyabiashara wenye mtaji chini ya milioni nne na pia ni kwa lengo la kuwawezesha mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwa na idadi na takwimu sahihi itakayowawezesha kwa urahisi kufanya kazi yao ya kukusanya mapato. "Tumefanyia zoezi hili hapa Mwenge, kwani ndiko kuliko na wafanyabiashara wengi na vitambulisho hivi vimetolewa kwa lengo la kuwezesha mamlaka ya mapato Tanzania kutambua wafanyabiashara wadogowadogo, pia litawasaidia wafanyabiashara wetu kufanya biashara bila bugudha yeyote." Amesisitiza Mkuu huyo wa Wilaya. Naye Afisa Biashara wa Manispaa hiyo Bw. Mohamed Nyasama alipotakiwa kuzungumzia swala hilo amesema, hii ni neema kwa wamachinga kwani kitakachofanyika ni kuwatambua, kuwahakiki, na kuwapatia vitambulisho hivyo vitakavyowasaidia kufanya biashara sehemu yoyote nchini bila usumbufu wowote. Amesema kinachotakiwa kufanyika ni kwa wafanyabiashara waliokwisha hakikiwa kujaza fomu za usajili, kuwasilisha picha, na vitambulisho ambavyo walikwishapatiwa na Manispaa awali, ili waweze kupatiwa vipya na kwa wale wamachinga ambao hawana vitambulisho kuhakikiwa upya na kupatiwa vitambulisho kwa mujibu wa sheria. Aidha zoezi hili pia limehusisha wamachinga kutoka masoko ya Bunju A, na B, Morocco, Boko Basihaya, Mbezi samaki, Mbezi ya Chni,Tegeta, Kawe, Mwenge, Makumbusho, Magomeni, Mwananyamala na Tandale. Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wamachinga hao kuhakikisha wanazingatia sheria, kanuni, na taratibu katika matumizi ya vitambulisho hivyo, ili kuepukana na usumbufu wowote unaoweza kutokea na kuhakikisha kila muhusika ananufaika na zoezi hili. Imeandaliwa na Kitengo cha habari na Uhusiano. Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO TAKRIBANI 5000 KWA WAMACHINGA Posted On: December 11th, 2018 Akizindua zoezi hilo kati... + Read more »
BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAMPONGEZA RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE.DR.JOHN POMBE MAGUFULI Posted On: December 14th, 2018 NI KUFUATIA MPANGO WA UTOAJI WA VITAMBULISHO KWA WAMACHINGA UTAKAOWARAHISISHIA UFANYAJI KAZI ZAO BILA BUGUDHA. Baraza la Madiwani Manispaa ya Kinondoni chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni diwani wa kata ya Msasani Mhe. Benjamini Sitta, leo limempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dr.John Pombe Joseph Magufuli, kwa mpango wake mzuri, madhubuti na wezeshi wa kuwapatia vitambulisho wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama wamachinga vitakavyowasaidia katika shughuli zao. Akitoa pongezi hizo kwa niaba ya Baraza hilo, Meya Sitta amesema, mpango huo mkakati wa vitambulisho ni mpango ulio rahisi, rafiki, na wezeshi utakaowawezesha wamachinga kufanya kazi zao mahali popote nchi hii bila kubughudhiwa alimradi wasivunje sheria. Ameongeza kuwa vitambulisho hivyo pia vitawasaidia si tu mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kufanya kazi zao,bali pia kwa wamachinga kutambulika kuthaminiwa na kusajiliwa katika mfumo unaojulikana. Akiainisha viambatishi rejea ili kupata kitambulisho hicho, katibu wa kikao hicho cha baraza, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg Aron Kagurumjuli amesema, kwa wale waliosajiliwa awali kwa kinondoni wanachotakiwa kufanya ni kurejesha kitambulisho cha awali, picha moja ya passportsize, kujaza fomu yenye taarifa zako, na kiasi cha fedha shilingi elfu ishirini tu. Katika hatua nyingine, Meya Sitta amewataka wamachinga wa Manispaa ya kinondoni kutokutumia vibaya vitambulisho hivyo kwani atakayebainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. Imeandaliwa na Kitengo cha Uhusiano na Habari. Manispaa ya Kinondoni. BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAMPONGEZA RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE.DR.JOHN POMBE MAGUFULI Posted On: December 14th, 20... + Read more »
SEMINA ELEKEZI KWA WAGAWA DAWA ZA KINGATIBA YA MABUSHA, MATENDE NA MINYOO YATOLEWA KINONDONI Posted On: December 14th, 2018 Semina hiyo iliyohusisha wagawa dawa za kingatiba za magonjwa ya mabusha na matende kutoka kata zote 20 za Manispaa ya kinondoni, imefanyika leo katika ukumbi wa Roman Catholic ulioko Manzese. Akieleza malengo ya semina hiyo, mratibu wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele katika manispaa ya Kinondoni Dr. Neema Mlole amesema, lengo ni kuhakikisha elimu iliyosahihi juu ya kampeni hii inatolewa kwa usahihi na kueleweka, lakini pia ni katika kuzingatia baadhi ya vipengele vinavyompasa binadamu yeyote yule kumeza dawa vinafuatwa, kadhalika na kuhakikisha pia malengo yaliyokusudiwa ya kufikia wananchi takribani milioni 1.2 kwa kampeni hii pia yanafikiwa. "Ili tuweze kufikia malengo madhubuti, ni lazima elimu sahihi itolewe, lakini pia tunahitaji kuimarisha na kuhakikisha tunalinda nguvu kazi ya wananchi,na namna pekee ni kuboresha afya zao pale inapobidi kwa kuhakikisha wanashiriki kampeni hizi kwa uhakika a ufasaha mkubwa. Amesisitiza Dr Neema. Ameongeza kuwa kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto kitengo cha magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele itaendesha kampeni kuanzia tarehe 15/12/2018 na kuisha tarehe 20/12/2018 ,,hivyo wagawa dawa hawa ni watu muhimu sana katika kuhakikisha ufanisi huo unakuwepo na unazingatiwa. Katika semina hiyo pamoja na zoezi la usambazaji kingatiba kwa ajili ya kampeni hiyo iliyoambatana na ugawaji wa vifaa vitakavyotumika, pia wamejifunza namna thabiti ya utoaji huduma hiyo, vitu vya kuzingatia kabla na baada ya utoaji wake, na upi umri sahihi wa mtu kumeza dawa ikiwa ni pamoja na kupima urefu. Katika hatua nyingine, wagawa dawa hao wameishukuru Wizara pamoja na Halmashauri kwa kuendesha kampeni hii yenye manufaa kwa afya za wanadamu, na kuahidi ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha hilo linafanikiwa. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano. Manispaa ya Kinondoni. SEMINA ELEKEZI KWA WAGAWA DAWA ZA KINGATIBA YA MABUSHA, MATENDE NA MINYOO YATOLEWA KINONDONI Posted On: December 14th, 2018 Semina hiyo... + Read more »