Top ad

Top ad

BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAMPONGEZA RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE.DR.JOHN POMBE MAGUFULI

Posted On: December 14th, 2018
 NI KUFUATIA  MPANGO  WA UTOAJI WA VITAMBULISHO KWA WAMACHINGA UTAKAOWARAHISISHIA UFANYAJI KAZI ZAO BILA BUGUDHA.
Baraza la Madiwani  Manispaa ya Kinondoni chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni diwani wa kata ya Msasani Mhe. Benjamini Sitta, leo limempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dr.John Pombe Joseph Magufuli, kwa mpango wake mzuri, madhubuti na wezeshi wa kuwapatia vitambulisho wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama wamachinga vitakavyowasaidia katika shughuli zao.
Akitoa pongezi hizo  kwa niaba ya Baraza hilo, Meya Sitta amesema,  mpango huo mkakati wa vitambulisho ni mpango ulio rahisi, rafiki, na wezeshi utakaowawezesha wamachinga kufanya kazi zao mahali popote nchi hii bila kubughudhiwa alimradi wasivunje sheria.
Ameongeza kuwa vitambulisho hivyo pia vitawasaidia si tu mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)  kufanya kazi zao,bali pia kwa wamachinga kutambulika kuthaminiwa na kusajiliwa katika mfumo unaojulikana.
Akiainisha viambatishi rejea ili kupata kitambulisho hicho, katibu wa kikao hicho cha baraza, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg Aron Kagurumjuli amesema, kwa wale waliosajiliwa awali kwa kinondoni wanachotakiwa kufanya ni kurejesha kitambulisho cha awali, picha moja ya passportsize, kujaza fomu yenye taarifa zako, na kiasi cha fedha shilingi elfu ishirini tu.
Katika hatua nyingine, Meya Sitta amewataka wamachinga wa  Manispaa ya kinondoni kutokutumia vibaya vitambulisho hivyo kwani atakayebainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.

0 comments:

Post a Comment

 
Top