DC CHONGOLO AAGIZA WATA ALAMU WA AFYA KUTOA ELIMU YA KUJIKINGA NA CORONA KWA WANANCHI Posted On: March 19th, 2020 NI KATIKA VITUO VYA DALADALA, NYUMBA ZAIBADA Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo, amewaagiza wata alaamu wa Afya Wilayani hapo kuanza mara moja kutoa elimu ya kujikinga na virusi vya Corona kwenye nyumba za Ibada ikiwemo Makanisani na Misikitini. Aidha Mhe. Chongolo ameagiza pia elimu hiyo kutolewa kwenye vituo vya daladala ili kuwasaidia wananchi kutambua namna ya kutumia na kujikinga na Virusi hivyo. Mhe. Chongolo ametoa agizo hilo leo katika kikao cha zarura kilichofanyika katika ukumbi wa Afya ambapo kimehusisha Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Idara ya Afya, watendaji pamoja na viongozi wa Dini . Amesema kuwa lengo la kikao hicho cha zarura ilikuwa ni kujadili namna na hatua zitakazo chukuliwa katika kudhibiti virusi hivyo ili visiweze kusambaa pamoja na kutoa elimu ya kutosha kwa watumishi sambamba wananchi katika Wilaya hiyo. Amesema kutokana na kuingia kwa Virusi hivyo vya Corona katika jiji la Dar es Salaam, wataalamu hao wa Afya wa Wilaya hiyo wanapaswa kutoa elimu madhubuti kwenye maeneo ambayo ni lazima wananchi kuyatumia kama vile Vituo vya daladala ikiwemo vya mwendokasi, nyumba zaibada kuhusu namna ya kujikinga na virusi hivyo. Amefafanua kuwa katika elimu hiyo pia itajikita katika kuelimisha wananchi namna ya kutumia vifaa vya kujikinga na maambukizi hayo kama vile vifaa vya kusafishia mikono, Gloves na Barakoa (Mask ) za kufunika pua na mdomo. “ Hili jambo tunapaswa kulichukulia kwa tahadhari kubwa, muwaelimishe wananchi kuhusu namna ya kujikinga na Virusi hivyo, pamoja na kutumia hivyo vifaa ,mnapopita kwenye hayo maeneo hakikisheni kwamba mnawaelimisha vizuri ili wajue ni wakati gani wanapaswa kuvitumia, pia kusafisha miko mara kwa mara” amesema Mhe. Chongolo. “ Lakini pia tuwasaidie wananchi kutoka kwenye presha waliyo kuwa nayo hivi sasa, tunafahamu kuwa watanzania wengi wamepata taharuki juu ya Vizuri hivi, tusipojitahidi tutajikuta tatizo la presha lina adhiri wananchi kuliko Vizuri vya Corona. Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo amewaeleza viongozi wadini kwamba mikusanyiko isiyokuwa ya lazima haipaswi kuwepo ila kwa ambao wanataka kufunga ndoa wafungishwe lakini kwa kufuata utaratibu ambao utaepusha mikusanyiko ya watu. Awali Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo, John Kijumbe amesema kuwa hadi sasa wameshachukua tahadhari na kama vile kutoa elimu katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwa watumishi na wahudumu wa Afya pamoja na kugawa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo. Hata hivyo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imejidhatiti kikamilifu katika kujikinga na virusi hivyo kwakuweka visafisha mikono kwenye mageti yote ya kuingia ikiwa ni katika kuhakikisha kuwa kila mwananchi anayefika kupata huduma mbalimbali wanakuwa salama. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. DC CHONGOLO AAGIZA WATA ALAMU WA AFYA KUTOA ELIMU YA KUJIKINGA NA CORONA KWA WANANCHI Posted On: March 19th, 2020 NI KATIKA VITUO VYA D... + Read more »
DC CHONGOLO AWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA UGONJWA WA CORONA Posted On: March 17th, 2020 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo amewataka wakazi wa Wilaya hiyo kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa Homa ya Vizuri vya Corona ikiwa ni pamoja na kupokea wageni wasio wajuwa bila kuwa na uhakika wa afya zao. Mhe. Chongolo ametoa kauli hiyo leo wakati alipokuwa kwenye mkutano na wananchi uliokuwa na lengo la kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali hivyo kuwataka kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake sambamba na kuepuka kukaribisha wageni kienyeji. Ameongeza kuwa “ kuanzia leo nyinyi wenyewe muwe walinzi wa wenzenu, chukueni tahadhari, msije kupokea wageni wa aina yoyote ile kwa sababu wapo watu ambao wanaweza kutumia njia mbalimbali za kuleta vizuri hivyo katika maeneo yetu” amesisitiza Mhe. Chongolo. Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo amezindua Bandari Bubu iliyopo Mbweni nakuzitaka Malaka za Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuepusha changamoto kwa wananchi, wafanyabiashara wanaotumia bandari hiyo. Mhe.Chongolo amesema kila mamlaka husika zinapaswa kuwepo katika eneo pamoja na Taasisi nyingine ili kuwezesha wananchi na wafanyabiashara wanaotumia bandari hiyo kufanya shuguli zao kwa urahisi kulingana na mazingira rafiki yaliyopo. Amefafanua kuwa Nchi ilikuwa inakosa mapato mengi kupitia upitishaji wa magendo katika maeneo ya fukwe za Mbeni, Ununio, Kunduchi pamoja na maeneo mengine ya pembezoni mwa fukwe za bahari na hivyo kueleza kuwa tayari bandari hiyo imeruhusiwa kutumika na watu kufanyabishara zao. ”hapo awali tulikuwa hatupati fedha kwenye hii Bandari, ila hivi sasa tumeanza kupata fedha , naomba tushirikiane vizuri na nikiondoka hapa kwenye mkutano , mamlaka zote ambazo zinapaswa kuwepo hapa ziwepo ikiwemo TRA, tunataka mapato wao wasiwe kikwazo cha kutukosesha mapato. Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo amemtaka OCD wa Kawe kuhakikisha kuwa usalama kwa wafanyabiashara unakuwepo sambamba na kuwachukulia hatua wote ambao watakiuka na kushindwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa. Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Uhusiano Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. DC CHONGOLO AWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA UGONJWA WA CORONA Posted On: March 17th, 2020 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe... + Read more »
KINONDONI YAINGIA MKATABA NA KAMPUNI MBILI UJENZI WA BARABARA, BILIONI 34.2 KUTUMIKA. Posted On: March 10th, 2020 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni leo imesaini mkataba na Kampuni mbili za China kwa ajili ya ujenzi wa mradi mkubwa wa barabara zenye urefu wa kilomita 12 ambapo jumla ya kiasi cha Tsh. Bil. 34.2 zitatumika kwenye mradi huo. Kampuni ambazo Manispaa ya Kinondoni imeingia mkataba wa ujenzi huo mara baada ya kutangazwa tenda ni Stecol Corporation pamoja na China Ralway Seventh Group Limited. Mkataba huo umesainiwa na Mstahiki Meya Mhe. Benjamini Sitta, na kushuhudiwa na Kaimu Mkurugenzi Dk. Patricia Henjewele pamoja na Kaimu Mhandisi wa Manispaa Mkelewe Tungaraza. Akizungumza mara baada ya hafla ya utiwaji wa saini wa mkataba wa mradi huo, Meya Sitta amefafanua kuwa ujenzi huo utahusisha barabara ya Magomeni mapipa hadi urafiki ambayo inaurefu wa zaidi ya kilomita saba (7), Makumbusho, Mwanamboka, na barabara ya Muhimbili ambazo zinaurefu wa zaidi ya kilomita tano (5). Aidha Meya Sitta ameeleza kuwa ujenzi wa barabara ya Magomeni Mapipa na Urafiki inajengwa na Kampuni ya Stecol Corporation kwa gharama ya Tsh. Bil. 18.7 huku barabara ya Makumbusho, Mwanamboka na Muhimbili ikijengwa na Kampuni ya China Ralway Seventh Group Limited kwa gaharama ya Tsh. Bil.15.5. Mhe. Sitta amemshukuru Mkurugenzi Aron Kagurumjuli kwa kuhakikisha barabara hizo zinajengwa na kwamba maendeleo ambayo yanafanyika katika Manispaa hiyo yanatokana na juhudi kubwa ya utendaji kazi wake. “ Nampongeza Mkurugenzi wetu, anafanya kazi kubwa leo hii tunakwenda kuleta maendeleo makubwa ya barabara katika Manispaa yetu, hivyo mradi huu utakuwa sehemu ya kutatua changamoto zilizopo katika Halmashauri yetu” amesema Meya Sitta. “ Leo ni siku ya kihistoria katika Manispaa yetu, tumesaini mikataba mikubwa miwili kutoka kampuni mbili tofauti , mikataba hii nisehemu kubwa ya mradi wa DMDP, ambao unakwenda kutatua changamoto ya barabara kwenye Halmashauri yetu , hivyo ninampongeza sana Mkurugenzi wetu Kagurumjuli” amesema Meya Sitta. Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa DMDP ambaye pia ni Kaimu Mhandisi wa Manispaa, Mkelewe Tungaraza amesema kuwa mradi huo utaanza Aprili mwaka huu na unatarajiwa kukamilika kwa muda wa miezi 15. Imeandaliwa na Kitengo Cha habari na Mahusiano Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAINGIA MKATABA NA KAMPUNI MBILI UJENZI WA BARABARA, BILIONI 34.2 KUTUMIKA. Posted On: March 10th, 2020 Halmashauri ya Manisp... + Read more »
KINONDONI YA ADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI Posted On: March 9th, 2020 Shehere ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yamefanyika leo katika viwanja vya Lidas ambapo kimkoa mwenyeji na muandaaji wa ma adhimisho hayo ni Wilaya ya Kinondoni. Katika ma adhimisho hayo, mgeni rasmi ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Poul Makonda ambapo alisindikizwa na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Daniel Chongo, Katibu Tawala Bi. Stella Msofe , Kaimu Mkurugenzi Dk. Patricia Henjewele, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii pamoja na watumishi wanawake wa Halmashauri hiyo. Aidha Mhe. Makonda aliambatana na wageni wengine ambao ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Dk. Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sarah Msafiri na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Bi. Sipora Liana. Madhimisho hayo yalibeba ujumbe ulioeleza kuwa KIZAZI CHA USAWA KWA MAENDELEO YA TANZANIA YA SASA NA YA BAADAE. Imeandaliwa na kitengo cha Habari na Uhusiano Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni KINONDONI YA ADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI Posted On: March 9th, 2020 Shehere ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yamefan... + Read more »
KINONDONI YAPONGEZWA KUONGOZA MARA NNE MFULULIZO KIMKOA Posted On: February 24th, 2020 NI KATIKA KUFANYA VIZURI KWENYE MATOKEO YA KIDATO CHA NNE CHA PILI Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ,imepongezwa kwa kufanya vizuri katika matokeo ya kidato Cha nne na cha pili kwa miaka minne mfululizo kwa mkoa wa Dar es Salaam. Pongezi hizo zimetolewa na Afisa Elimu wa mkoa wa Dar es Salaam Bwana Hamis Lissu wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa walimu na shule zilizofanya vizuri kwa matokeo hayo kitaifa na kimkoa kwa mwaka 2019 ,2020. Lissu amesema kuwa Halmashauri hiyo imekuwa ikifanya vizuri na kwa ufanisi mkubwa kwa kila eneo ikiwemo Elimu, Afya na mazingira, Michezo na maeneo mengine na kusema kuwa mafanikio hayo yanatokana na kuwa na Mkurugenzi mwenye juhudi za kufanya kazi inayoendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano inayo ongozwa na Dk. John Pombe Magufuli. Lissi amefafanua kuwa Mkoa wa Dar es Salaam unajumla ya Halmashauri tano lakini Halmashauri ya Kinondoni inayo ongozwa na Mkurugenzi wake Aron Kagurumjuli imekuwa ikifanya vizuri katika sekta ya elimu ambapo imeongoza kuwa na matokeo mazuri kwa miaka minne mfululizo katika mkoa huo. " Kinondoni imekuwa ikifanya vizuri sana kwenye mambo mengi, binafsi mnanikosha na utendaji wenu uliotukuka ,niwasihi nguvu hii mliyokuwa nayo muendelee nayo ili kuendelea kuwa na rekodi nzuri kwa kuwa mfano bora kwa Halmashauri nyingine zilizopo katika mkoa wetu" amesema Bwana Lissu. Lakini pongezi hizi pia zimuendee zaidi Mkurugenzi Kagurumjuli, Kinondoni mmepata Mkurugenzi bora, anafanya vizuri sana kwenye Halmashauri yake,na uchapakazi huu ndio anaoutaka Mhe. Rais wetu Dk. Magufuli, tukiwa na wachakazi kama hawa, hakika kwenye mkoa wetu tutakuwa na matokeo makubwa zaidi kwenye kila eneo” ameongeza Bwana Lissu. Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari, wa Halmashauri hiyo, Bwana Leornad Msigwa amesema katika matokeo ya kidato cha nne Kinondoni ilishika nafasi ya 39 kati ya Halmashauri 195 na hivyo kufanya kupanda nafasi tatu kitaifa ukilinganisha na mwaka 2018 ambapo ilishika nafasi ya 42 na kuendelea kuongoza kwa kishindo kwa miaka mine mfufulizo katika mkoa wa Dar es Salaam. Msigwa ameongeza kuwa tathmini ya matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2019 inaonyesha kuwa ufaulu umeongezeka kwa silimia 0.59 ukilinganisha na mwaka 2018 ambapo ufaulu umekuwa kwa asilimia 81.21 ambapo mwaka 2019 ufaulu ulikuwa kwa asilimia 81.80. Kwa upande wa matokeo ya kidato cha pili , Msigwa ameeleza kuwa tathmini ya upimaji wa matokeo ya kidato cha pili kwa mwaka 2019 , ufaulu ulikuwa kwa silimia 94.04 na hivyo kufanya Halmashauri ya Kinondoni kushika nafasi ya 24 kitaifa kati ya Halmashauri 184 na hivyo kupanda nafasi 10 kitaifa ukilinganisha na mwaka 2018. Msigwa amefafanua kuwa, katika matokeo hayo mwaka 2019 watahiniwa walikuwa 9,340 ambapo waliofaulu mtihani huo kati ya daraja 1-1V walikuwa 8,783 sawa na asilimia 94.04. Amefafanua kuwa kati yao waliopata alama za ufaulu wa daraja la kwanza ni 1,682, daraja la piIi ni 1,216, daraja la tatu 1,556, daraja la nne 4,329 huku jumla ya watahiniwa 557 walipata alama ya sifuri. Katika hatua nyingine Msigwa amewaeleza walimu wa shule za Sekondari waliokuwa katika hafla hiyo kuendelea kujituma zaidi kwa kutumia mbinu mbalimbali za ufundishaji ili kuwezesha Halmashauri hiyo kuendelea kufanya vizuri zaidi kitaifa na kimkoa. Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Uhusiano Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YAPONGEZWA KUONGOZA MARA NNE MFULULIZO KIMKOA Posted On: February 24th, 2020 NI KATIKA KUFANYA VIZURI KWENYE MATOKEO YA KIDAT... + Read more »
KINONDONI YA TUMIA BIL. 1.5 UJENZI WA MADARASA YA SHULE ZA MSINGI Posted On: February 4th, 2020 WALIMU WASEMA MKURUGENZI KAGURUMJULI ANATEKELEZA IPASAVYO SERA YA ELIMU BILA MALIPO. Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imetumia kiasi cha shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi na ukaratabati wa vyumba 107 vya madarasa pamoja na matundu ya choo 157 kwa wanafunzi wa shule za msingi zilizopo katika Halmashauri hiyo. Hayo yamebainisha na Afisa elimu msingi wa Halmashauri hiyo Kiduma Mageni wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya shule iliyokuwa na lengo la kuona maendeleo ya miradi hiyo ambayo inatekelezwa kwa kutumia Force Account. Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa ziara hiyo, Ndugu Mageni amesema kuwa katika fedha hizo zilizotumika kujenga na kukarabati vyumba hivyo vya madarasa pamoja na matundu ya choo, shilingi milioni 771, 520,000 zinatokana na makusanyo ya ndani, shilingi milioni 455,140,000 ni pesa kutoka serikali kuu kupitia mpango wa EP4R. Aidha Mageni ameongeza kuwa katika fedha hizo pia kiasi cha shilingi milioni 210, 004, 726 ni pesa kutoka mpango wa madarasa 100 ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Daniel Chongolo, na kiasi cha shilingi milioni 4, 140,000 nipesa zinazotokana na nguvu za wananchi. Sambamba na hivyo, ndugu Mageni amebainisha madarasa yaliyojengwa ni 58, yaliyokarabatiwa ni 42 na kwamba kwa vyumba vilivyokarabatiwa vimeanza kutumika na wanafunzi huku vile vinavyojengwa vikiwa vimekamilika kwa asilimia 95. Mageni amesema Halmashauri ya Kinondoni kupitia Mkurugenzi Aron Kagurumjuli pamoja na Mkuu wa Wilaya Mhe. Daniel Chongolo wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa inajenga na kukarabati madarasa hayo ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira mazuri. Ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya tano inayo ongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli inatoa elimu bure na kwamba viongozi hao Mkurugenzi Kagurumjuli na Mkuuwa Wilaya Chongolo wanaitekeleza kikamilifu sera hiyo. “ Niwapongeze sana kwa kazi nzuri wanayoifanya, tumejionea wenyewe wanafunzi wanakaa kwenye majengo mazuri,ya kisasa ,mengine bado yapo kwenye hatua ya mwisho kukamilika na muda sio mrefu yatakabidhiwa ili watoto wetu wa anze kuyatumia. “Nampongeza sana Mhe. Chongolo, Kagurumjuli na timu yake yote wanafanya kazi kubwa, inaonekana, Rais wetu Dk. Magufuli ametoa elimu bure na sisi tunaitekeleza, nasio kwamba tunaishia hapa, bado tutaendelea kutekeleza zaidi na zaidi ili watoto wetu wasome kwenye majengo safi” amesema Mageni. Mageni amesema ameridhishwa na ujenzi, ukarabati wa majengo hayo na hivyo kuwataka walimu hao kuwa wasimamizi wazuri wa miundombinu hiyo. Kwa upande wa mwalimu hao waliokuwa katika ziara hiyo wamempongeza Mkurugenzi Kagurumli kwa kuwezesha ujenzi wa madarasa hayo na kwamba wanafunzi watasoma kwa nafasi. Mmoja wa walimu hao ambaye ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mwenge, Janeth Mlenge alisema kuwa elimu bure inayotolewa na Rais Dk.Magufuli imetoa hamasa kwa wazazi na hivyo kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma. Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Nyakasanga amesema kuwa kupitia mradi huo katika shule yake amejengewa vyumba nane vya madarasa ofisi ya mwalimu mkuu pamoja na matundu 13 ya choo na hivyo kumpongeza Mkurugenzi Kagurumjuli,Mhe. Chongolo kwa kuwapatia majengo hayo. Hata hivyo walimu hao wameonyesha kufurahishwa na huduma hiyo ya kujengewa madarasa katika shule zao, sambamba na kukarabatiwa na kusema serikali kupitia Halmashauri ya Kinondoni inatekeleza vema sera ya Elimu bila malipo. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. KINONDONI YA TUMIA BIL. 1.5 UJENZI WA MADARASA YA SHULE ZA MSINGI Posted On: February 4th, 2020 WALIMU WASEMA MKURUGENZI KAGURUMJULI AN... + Read more »
DC CHONGOLO ASITISHA VIBALI VYA UCHIMBAJI MCHANGA MABONDENI Posted On: February 4th, 2020 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo amesitisha vibali vya uchimbaji mchanga vilivyotolewa na Bodi ya Maji Bonde la Ruvu kutokana na kuleta madhara ya uharibifu wa mito na kusababisha athari kwenye makazi ya watu katika Halmashauri hiyo. Vibali vilivyositishwa katika ni vile vilivyotolewa kufanya shughuli hizo katika Bonde la mto Salasala, Mto mbezi, Ndumbwi, Nyakasangwe, na kusema kuwa mito hiyo inapita katikati ya makazi ya watu na kwamba baada ya kufanyika marekebisho utawekwa utaratibu upya wa kufanya shughuli hizo. Akizungumza mara baada ya kufanya ziara katika Bonde la mto Salasala (Mto Tegeta) Mhe. Chongolo amesema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya wakandarasi waliopewa vibali hivyo kuharibu mto huo na hivyo kuamuru kupandwa kwa Miti hiyo ambayo itasaidia kuzuia mmomonyoko wa udongo. Amesema kuwa kinachofanyika hivi sasa ni kurekebisha mito hiyo kwa kupanda miti, magugu pamoja na mianzi inayoshika ardhi ili kuzuia mmomonyoko wa undongo na hivyo kuweka mkakati wa kuratibu shughuli za utoaji mchanga kufanyika katika maeneo hayo. Mhe. Chongolo amesena kuwa katika Halmashauri hiyo ameruhusu kibali hicho kutolewa katika bonde la Mpigi kwa maelekezo ya kuhakikisha kuwa shughuli hizo zifanyike kwa ajili ya kusafisha mto ili kuondosha adhari kwani mchanga ukijaa sana husababisha maji kusambaa nje. “ Wakati tunafanya haya ni lazima tusitishe shughuli zote zinazofanyika hapa, tulifanya tathimini ya kuangalia athari kwa kuunda timu ambayo ilikamilisha majukumu yake na kuleta ripoti hiyo Disemba mwaka jana, mwezi wa kwanza mwaka huu tulianza mjadala na wale ambao walipewa kandarasi ya kutoa mchanga kwenye mito hii” amesema Mhe. Chongolo Nakuongeza kuwa “ baada ya majadiliano hayo, tulikubaliana nao kupanda Miazi, Miti na Magugu, na watu ambao mnawaona hapa asilimia 90 niliagiza kila mwenye kibali cha bonde anayekuja aje na watu 10 kwa ajili ya kushirikiana kupanda miti, na hii miti inayopandwa hapa sijanunua wameleta wao” ameongeza Mhe. Chongolo. Mhe. Chongolo amesisitiza kuwa “ kwanza mchanga usiondolewe kibiashara ,tutoe mchanga sehemu ambayo tunaona kuwa kunaongezeko ambalo linaweza kusababisha athari, ili turuhusu maji yapite bila kuleta madhara kwa wananchi waliopo pembezoni mwa mto na huyo anayetoa ahakikishe anafanya marekebisho ikiwemo kupanda miti, magugu na mianzi. Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo amesema kuwa " Tunachangamoto ya watu kufanya shughuli za kibinadamu kwenye maeneo ya maji, Serikali imeshaelekeza watu ambao wapo kwenye maeneo haya wanatakiwa kuwa umbali wa mita 60 kwa 60 , lakini hatufuati hiyo Sheria ya mazingira. Wananchi mliopo katika maeneo haya, niwasihi sana acheni kufanya shughuli hapa, leo tunapanda miti ili kunusuru bonde hili lisiendelee kukua, mchanga utatolewa kwa kibali kwa ajili ya kusafisha mto ila sio kuchimba mchanga kwa shughuli ya kibiashara ama nyingine, " amesema Mhe. Chongolo. Imeandaliwa na Kitengo Cha Habari na Uhusiano Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni DC CHONGOLO ASITISHA VIBALI VYA UCHIMBAJI MCHANGA MABONDENI Posted On: February 4th, 2020 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chong... + Read more »