KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI AFYA NA ELIMU KINONDONI YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO.

Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Mhe Michael Urio ambae pia ni Diwani wa Kata ya Kunduchi imekagua Ujenzi wa Soko la kisasa la Tegeta Nyuki, Ujenzi wa madarasa sita shule ya sekondari mitimirefu, Ujenzi wa kiwanja cha mpira wa miguu Mwenge na Ujenzi wa kituo cha mabasi Mwenge.
Miradi mingine ni Ujenzi wa madarasa nane Katika shule ya sekondari Kijitonyama pamoja na kuangalia eneo la Ujenzi wa chumba cha kuhifadhia maiti katika kituo cha Afya Kigogo.
Kamati imeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikiwa ni Pamoja na hatua zilizofikiwa na kiwango cha ubora wake.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
0 comments:
Post a Comment