Top ad

Top ad

DC CHONGOLO AFANYA ZIARA SOKO LA MAGOMENI NA TANDALE KWA LENGO LA KUJIONEA MAENDELEO YA UJENZI

Posted On: October 23rd, 2019
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni , Mhe. Daniel Chongolo leo amefanya ziara katika soko la Tandale na Magomeni kwa lengo la kuangalia maendeleo ya ujenzi na kusikiliza maoni mbalimbali  waliyonayo wafanyabishara hao kuhusiana na ujenzi unaoendelea.

Mhe. Chongolo amesema kuwa ameridhishwa na namna hatua ya ujenzi wa masoko hayo mawili unavyokwenda kwa kasi na kuwaeleza kuwa majengo hayo ni kwa ajili ya wafanyabiashara hivyo lazima wawe sehemu ya mradi.

Aidha  amefurahishwa na ushirikiano uliotolewa na wafanyabiashara hao ikiwemo kupisha kwa hiyari yao eneo ambalo linafanyika ujenzi wa soko hilo na kuwahakikishia kuwa Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Magufuli  iko pamoja nao.
"Ninawapongeza sana wafanyabishara kwa moyo mliounyesha, mmekaa pembeni , hamna shida najua mnasubiri kwa hamasa kubwa kukamilika kwa jengo hili ili muweze  kufanya biashara zenu,Kikubwa napita kwa ajili ya kujiridhisha na kile kinachoendelea ili tusije kujenga miundombinu ambayo sio rafiki kwenu.” amesisitiza.

DC amewaeleza wafanyabiashara hao kuwa Mhe. Rais Dk. John Magufuli ametoa zaidi ya shilingi bilioni 18 kwaaajili ya ujenzi wa masoko hayo mawili ya Tandale na Magomeni ili kuboresha mazingira ya wao kufanyia biashara.

Akizungumzia soko la Tandale ambalo linauwezo wa kuchukua wafanyabishara zaidi ya 1000, Mhe. Chongolo amesema kuwa kulingana na idadi hiyo kubwa ambayo wengi wanamatamanio ya kufanya shughuli zao kwenye ghorofa ya chini, wana angalia namna ya kutengeneza mazingira ili  wote waweze kupata eneo bila kuwepo na malalamiko.

Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano

0 comments:

Post a Comment

 
Top