Top ad

Top ad

JAMII YA KINONDONI YATAKIWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUTUMIA MAZIWA ILI KUIMARISHA AFYA YA MWILI NA AKILI KUELEKEA UCHUMI WA KATI WA VIWANDA

Posted On: May 24th, 2019
Kauli hiyo imetolewa leo na Mhe Diwani wa kata ya Kunduchi Mh. Michael Urio kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya unywaji wa maziwa mashuleni inayoratibiwa na Idara ya mifugo na uvuvi kwa Manispaa ya Kinondoni na kufanyika katika Shule ya Sekondari Kondo.
Amesema kuwa, serikali ya awamu ya tano inayo nia madhubuti na mwelekeo wa dhati katika kuijenga Tanzania ya Viwanda na uchumi wa Kati, hivyo inahitaji jamii ya watu wenye afya thabiti na akili ya kupambanua mambo kwa ufasaha ili waweze kuendana na sera hiyo.
"Maziwa yana virutubisho vyote mhimu vinavyotakiwa katika ujenzi wa mwili na akili hivyo badala ya kunywa pombe na vinywaji vingine tunyweni maziwa kwa wingi ili kuunga juhudi za serikali pia viwanda vyetu vya ndani" ameongeza  mhe Urio.
Aidha Quenter Mawinda kwa niaba ya msajili wa bodi ya maziwa amewashauri wanafunzi kutumia maziwa kwa wingi ili kuimarisha afya ya akili na mwili na waweze kuendana na Kasi ya Mhe Rais maana anahitaji vijana wachapakazi walioimara.
Mara baada ya uzinduzi huo , Manispaa ya Kinondoni kupitia idara ya mifugo na uvuvi imegawa maziwa katika shule tano za Sekondari ambazo ni Shule ya Sekondari Mbopo, Kondo, Mtakuja Beach, Boko na Bunju A, ambapo zaidi ya paketi 350 kwa kila shule zimegawiwa, lakini siku ya pili kwa idadi ya paketi hizo hizo itagawiwa kwa Shule tano za Msingi za Manispaa ya Kinondoni .
Uzinduzi huu unatarajiwa kitaifa kufanyika Mkoani Arusha kuanzia tar 28 mwezi wa tano hadi tarehe 1 mwezi wa sita.

Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.

0 comments:

Post a Comment

 
Top