Top ad

Top ad

KAMATI YA MIPANGOMIJI NA MAZINGIRA MANISPAA YA KINONDONI YAKAGUA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Posted On: November 28th, 2018
Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni diwani wa Kata ya  Mwananyamala Mhe. Songoro Mnyonge, leo imekagua miradi mitatu ya maendeleo kwa lengo la  kujiridhisha utekelezaji wake, ikiwa ni pamoja na kukagua hatua za utekelezaji zilizofikiwa.
Akikagua miradi hiyo, Mhe.Songoro amesema kukamilika kwake kwa wakati ndio lengo lililokusudiwa, kwani maeneo haya ya mradi ni ya kimkakati, na wananchi wanahitaji huduma bora na zenye viwango.
"Haya yote ni maeneo ya kimkakati kwa maendeleo ya Halmashauri yetu, hivyo yatupasa kufanya na kupanga mikakati hii ili iendane sambamba na mabadiliko ya jamii yetu."Amesisitiza Mnyonge
Miradi hiyo iliyotembelewa ni  mradi wa ujenzi wa kiwanda cha uchakataji taka  Mabwepande chini ya mkandarasi CRJE,  mradi wa ujenzi wa barabara ya Tegeta nyuki urefu wa km 2.2 unaojengwa na TARURA, kwa kiwango cha lami, na mradi unaojishughulisha na utoaji wa namba za Mitaa (Post Code), ulioko Kijitonyama chini ya Manispaa kwa kushirikiana na TCRA.
Katika hatua nyingine, wajumbe wa kamati wameushukuru uongozi wa Manispaa, kwa uibuaji na  utekelezaji mzuri wa miradi ya  kimkakati  na kuelekeza ufanyikaji mzuri wa  maboresho utakaoleta tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.

0 comments:

Post a Comment

 
Top