Top ad

Top ad

TUITHAMINI SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI KAMA JAMII, ILI TUWE SEHEMU YA KUIENZI KWA VITENDO

Posted On: October 11th, 2018
Ni maneno yake katibu Tawala Wilaya ya Kinondoni Bi.Stella Msofe alipokuwa akizungumnza katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike,  yenye kauli mbiu isemayo "Imarisha uwezo wa mtoto wa kike, tokomeza ukeketaji, mimba, na ndoa za utotoni" yaliyofanyika katika viwanja vya Tanganyika packers, vilivyoko Kata ya Kawe Manispaa ya Kinondoni.
Amesema siku inayoadhimishwa tarehe 11/10 kila mwaka,  inatakiwa kuenziwa kwa jamii kuwa sauti ya kukemea uovu na kupinga unyayasaji wa mtoto wa kike, hasa unapohisi mazingira aliyopo mtoto huyo,  mifumo iliyopo katika jamii husika,  si rafiki kwa maisha na afya yake
"Kuwa mtoto wa kike kwanza ni neema na zawadi kutoka kwa Mungu, lakini pia ni ushindi tosha kwani akielimika mmoja, ni jamii nzima imeelimika, hivyo kusikufanye kushindwa kitimiza ndoto zako, mtoto wa kike unapaswa kujiamini, weka bidii katika vitu unavyoviamini kuwa vya maendeleo katika maisha yako na jamii inayokuzunguka na hakikisha unayasimamia" Amesisitiza Katibu Tawala Msofe.
Ameongeza kuwa Jamii inayonafasi kubwa ya kuhakikisha haki, misingi na wajibu kwa mtoto wa kike vinazingatiwa na kupinga vikali ukiukwaji wa mifumo na tamaduni zinazowakandamiza watoto wa kike.
Awali akitoa taarifa mbele ya katibu tawala huyo, Mratibu wa mradi wa ulinzi na usalama wa mtoto Manispaa ya Kinondoni Bi.Haika Harison,  amezitaja changamoto  zinazowakabili watoto wa kike kuwa ni ukeketaji, mimba za utotoni na ndoa za utotoni, na kuitaka jamii kuhakikisha inakuwa mstari wa mbele katika kumlinda mtoto wa kike.
Maadhimisho hayo yaliyoadhimishwa kwa kushirikiana na mashirika binafsi ya Save the Children, na People's development forum yamekutanisha wanafunzi 180 kutoka shule 5 za Manispaa ya Kinondoni ambazo ni shule ya Sekondari Mikocheni, kawe, Mbezi ndumbwi pamoja na shule ya Msingi Changanyikeni na Makongo juu.

Imeandaliwa na
kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.

0 comments:

Post a Comment

 
Top