WALIOJENGA KWENYE MAENEO YA WAZI NA MILIKI YA BARABARA KINONDONI KUBOMOA MARA MOJA.
Ni agizo lake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Alli Hapi alipofanya ziara ya ukaguzi wa maeneo ya wazi na miliki za barabara zilizovamiwa.
Amesema haya ni maeneo ya Umma, yanayotakiwa kutumika kwa manufaa ya Umma, hivyo kwa kupora maeneo hayo ya wazi ni uvunjivu na ukiukwaji wa Sheria unaotakiwa kuchukuliwa hatua.
"Baadhi ya watu wameweka makuta makubwa, na wengine wameweka vitegauchumi vya kibiashara, ambavyo wanavipangisha na wanakusanya fedha kinyume cha sheria,... Kwahiyo naagiza kuanzia leo, Halmashauri Mainjinia wote, pamoja na TARURA kufanya uhakiki wa kukagua road reserve zetu.. na watu wote waliopora maeneo hayo yabomolewe ndani ya mwezi mmoja " Ameagiza Hapi.
Aidha Mkuu huyo wa wilaya amewataka wale wote waliojenga kwenye maeneo hayo kutii sheria kwa kuondoa majengo yao bila bugudha yeyote ili kuondokana na usumbufu na athari zinaoweza kutokea.
Kwa upande wake Meneja wa TARURA Eng Leopold Runji aahidi kutekeleza agizo la Mkuu huyo wa Wilaya na kuwataka walioendeleza maeneo ya hifadhi ya barabara kuwasilisha uhalali wa vibali vyao ndani ya Wiki moja kuanzia leo, kinyume cha hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Mkuu huyo wa Wilaya ametembelea maeneo ya wazi ya Masaki, Oysterbay, na Mikocheni na kutoa maagizo na Maelekezo yanayotakiwa kutekelezwa ndani ya mwezi mmoja kuanzia Leo.
Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
0 comments:
Post a Comment