Watanzania wametakiwa kuyaendeleza, kuyaenzi na kuyaishi yale mema yote waliyoyaishi katika mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Hayo yamesemwa na Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam shekhe Alhad Mussa Salum alipokuwa akizungumnza katika Futari iliyoandaliwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Benjamin Sitta na kufanyika katika viwanja vya Manispaa.
Amesema amani ndio nguzo Kuu, muhimu ya maendeleo na dini isiwe chanzo cha kugawa watanzania kwa misingi yeyote ile.
Naye kiongozi Mkuu wa dhehebu la Shiha Tanzania shekhe Hemedi Jalala amesema saumu inayofungwa ienee kwa watu wote.
Amesisitiza amani, utulivu, maelewano, na kuboresha mahusiano kwa watanzania.
Ameongeza kuwa funga ilete chachu ya kuondoa umaskini na kuwajali yatima, majirani na wajane.
Katika hatua nyingine Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mh.Benjamini Sitta amewashukuru wale wote walioungana naye kwa pamoja katika futari iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali ambapo leo ni chungu cha ishirini na tisa.
Imetolewa na
Kitengo cha UhusianoManispaa ya Kinondoni.
0 comments:
Post a Comment